Search This Blog

Tuesday, November 22, 2011

WENGER ASHINDWA KUKANUSHA KUMHITAJI MARIO GOTZE


Kocha Arsene Wenger amekataa kupinga uvumi kwamba anajipanga kupeleka ofa ya kumnunua star wa Borussia Dortmund Mario Gotze.

Arsenal wanawakaribisha mabingwa wa Ujerumani katika uwanja wa Emirates kesho jumatano katika mchezo wao muhimu wa hatua ya makundi ya champions league, huku wakihitaji ushindi kujihakikishia nafasi ya kupita kucheza hatua ya mtoano.

Wenger anatambua uwezo wa Dortmund ambao walitoka nao sare ya 1-1 mwezi Septmber, alkini kocha huyu mfaransa mabingwa hao wa Bundesliga nguvu kubwa ipo kwa mchezaji tegemeo Mario Gotze, kiungo ambaye Wenger ameonekana kumhitaji katika kikosi chake.

“Tuna kikosi kikubwa na kwa muda huu hatuna mchezaji tunayemfuatilia. Gotze ni mchezaji mzuri na naelewa kwamba amekuwa akivizutia timu nyingi barani ulaya. Kwa upande wetu, sifikiri kama sasa ni muda muafaka kuongelea kuhusu kumsajili Gotze wakati kesho tunacheza dhidi ya Dortmund, hivyo inabidi tuweke umakini katika mchezo huo muhimu na sio uhamisho.”

Gotze anatajwa kuwa na thamani ya £30 million, fedha ambayo ipo nje ya sera ya ada ya uhamisho ya klabu ya Arsenal ambayo mpaka sasa mchezaji aliyeghali zaidi kwenye kikosi chao ni Andrey Arshavin aliyewagharimu kiasi cha £15million.

CHELSEA YAMTAKA GARY CAHIL KUTATUA TATIZO LA ULINZI .


Under fire Chelsea coach Andre Villas-Boas anajipanga kuvunja bank na kumnunua beki wa kati wa England na klabu ya Bolton Gary Cahil, ili kuweza kutatua matatizo ya safu ya ulinzi yanayoikabili timu yake.

Cahil, 25, anamaliza mkataba wake katika kipindi cha kiangazi kinachokuja hivyo thamni yake inaweza kupungua kufikia £8million wakati dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa mwezi Janaury mwakani.

Chelsea wameruhusu wavu wao kuguswa mara 17 katika mechi zao 12 za ligi msimu na wameweza kupata clean sheet mbili tu, wakiwa wanahangaika ku-adapt mbinu mpya za Andre Villa-Boas.

John Terry akiwa anaandamwa na matatizo ya kashfa ya ubaguzi wa rangi na kupoteza umakini, David Luiz akiwa out of form, na Alex akitegemewa kutaka kuondoka in January, Villa-Boas analazimika kuongeza options za mabeki

Bolton walikataa ofa mbalimbali kutoka Arsenal na Tottenham kipindi cha usajili kilichopita, lakini sasa wapo radhi kusikiliza ofa kwa ajili ya Cahil kuliko kumpoteza bure mkataba wake utakapoisha mwishoni mwa msimu huu.

UEFA CHAMPIONS LEAGUE MATCHES - TODAY



1: Manchester United vs Benfica

2: Otelul Galati vs FC Basel

3: CSKA vs Lille

4: Trabzonspor vs Inter Milan

5: Napoli vs Manchester City

6: Bayern Munich vs Villarreal

MSAADA TUTANI

KUTOKA KUSHOTO
JAMES KISAKA ( WA TATU ), ZAMOYONI MOGELLA ( WA SITA ) EBU SAIDIA KUTAJA HAO WENGINE NA HICHO KILIKUA KIKOSI CHA TIMU GANI ?

ENZI ZILE ZA KUBANDIKA MAPICHA UKUTANI!!!

AISEE NIMEPATA FURSA YA KUTEMBELEA 'GHETO' LANGU LA ZAMANI WAKATI HUO NAISHI KWA MZEE DAUDA....NA HIVI NDO LILIVYOKUA LINANG'AA,WAKATI HUO WEWE KWENYE KUTA ZA CHUMBA CHAKO ULIKUA UNABANDIKA PICHA ZIPI ?

EXCLUSIVE INTERVIEW YA DAVID BECKHAM BAADA YA KUNYAKUA UBINGWA

ADEBAYOR APIGA MBILI SPURS IKIIUA ASTON VILLA


T-A footyroom.com by footyroom

BOBAN AMUUDHI JULIO, MBIONI KUTEMWA KILI STARS


Kitendo cha kiungo Haruna Moshi kuchelewa kuripoti kwenye kambi ya timu ya taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ kimemkera Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.

Moshi maarufu kama Boban hadi jana mchana alikuwa hajaripoti kwenye kambi ya timu hiyo iliyopo Dar es Salaam kujiandaa na michuano ya Chalenji itakayoanza Ijumaa wiki hii.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Kihwelo alisema mchezaji huyo alimuaga anaenda Arusha kwa matatizo ya kifamilia, lakini mpaka sasa ameshindwa kujiunga na timu hiyo.

Alieleza kuwa kama asingejiunga na timu hiyo hadi jana jioni, basi angefunga mlango na hatampokea.

Kocha huyo alieleza kuwa Boban anapaswa kutambua kuwa kocha anaheshimu kazi yake hivyo hawezi tena kumvumilia ikiwa atashindwa kujiunga na wenzake kambini. “Nimempa nafasi Boban kwani ni mchezaji mzuri lakini asipojiunga na wenzake mpaka kufikia leo (jana) jioni, sitampokea tena,” alisema kocha huyo.

Julai mwaka huu, Boban aliitwa na Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 23, lakini alikataa kujiunga. Boban hakupatikana jana kuzungumzia kuchelewa kwake kuripoti kambini.

Kwa mujibu wa Julio tayari mshambuliaji Gaudence Mwaikimba amejiunga na kambi ya timu hiyo na jana asubuhi alijumuika na wenzake wakati wa mazoezi ya timu Uwanja wa Karume.

Kiungo Nizar Khalfani aliyekuwa ameitwa kwenye timu hiyo ameondoka kurudi Canada kusaini mkataba mpya wa kuichezea klabu yake ya Vancouver Whitecaps.

Julio alisema wachezaji wote wameshajiunga na kambi ya timu hiyo na ari yao iko juu kuelekea mchezo wao dhidi ya Rwanda Jumamosi hii.

Kilimanjaro Stars iko Kundi A na timu za Rwanda, Nambia na Djibout.

SIMBA YAITANDIKA 5-2 OLJORO, YATINGA NUSU FAINALI UHAI CUP


Timu za Simba na Toto African zimetinga nusu fainali ya michuano ya vijana wenye chini ya miaka 20.
Simba iliyokuwa ikicheza kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam jana iliifumua Oljoro JKT kwa mabao 5-2, wakati Toto African ikiisambaratisha JKT Ruvu mabao 4-3 kwenye Uwanja wa Azam, Chamazi.

Toto African na Simba zitakutana kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza kesho itakayopigwa kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.

Mshambuliaji Miraji Athuman aliifungia Simba mabao matatu kati ya matano na kuondoka na mpira huku jingine likifungwa na Rashid Ismail na la kujifunga kwa beki Adelayun Seif wa Oljoro.Kocha wa Simba Seleman Matola aliwasifu vijana wake kwa kuonyesha soka zuri na kupata ushindi waliostahili katika mechi hiyo.

Alisema sasa wanajipanga kwa mechi ya leo ambayo amesema wachezaji wake watapambana kufa na kupona ili kupata ushindi na kuingia fainali.

"Tumejiandaa vizuri kwa mechi ya leo, tunafahamu kwamba tunacheza na moja ya timu nzuri kwenye mashindano, lakini azma yetu ni kushinda mechi hii," alisema Matola mchezaji wa zamani wa Simba na timu ya Taifa, Taifa Stars.

Mabao ya Oljoro yalifungwa na Hans Mwaisela ambaye anaongoza kwa kuzifumania nyavu akiwa amepachika mabao matano na Salehe Ally aliyefunga kwa mkwaju wa penalti.

Kocha wa Simba, Seleman Matola alisema baada ya mchezo huo kumalizika kuwa vijana wake wamecheza kwa kujituma na nakufuata maelekezo yake.

“Tumecheza vizuri toka mwanzo wa mchezo mpaka mwisho naamini sisi ndio timu bora kwenye mashindano haya,” alisema Matola.

Alisema nguvu na akili wanazielekeza kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya Toto African iliyowafunga hatua ya makundi kwa bao 1-0 na kuhakikisha wanalipiza kisasi na kutinga fainali ya michuano hiyo.

COUNTDOWN TO CECAFA CHALLENGE CUP: VIKOSI VYA KENYA, UGANDA NA MALAWI


KIKOSI CHA MALAWI

Squad:

Goalkeepers: Charles Swini,Vincent Gona and Mac Donald Harawa

Defenders: Foster Namwera, Bashir Maunde, Emmanuel Zoya, John Lanjesi, Pililani Makupe, Steve Chagoma, Ndaziona Chilemba

Midfielders: Nafe Msasa, Joseph Kamwendo, Frank Banda, Ndaziona Chatsalira, Chimango Kaira, Malumbo Gondwe, Henry Kabichi, John Banda.

Strikers: Ishamael Thindwa, Divasoni Chilemba, Loti Chawinga, Gastin Simukonda and Kumbukani Mwambeni.

KIKOSI CHA KENYA

Squad: Goalkeepers: - Duncan Ochieng (Sofapaka), Jacktone Odhiambo (Ulinzi Stars)

Defenders - Mulinge Ndetto (Ulinzi Stars), Brian Mandela (Tusker), James Situma (Tirania, Albania), Jockins Atudo (Tusker), Pascal Ochieng (Rangers), Erick Masika (Gor Mahia), Dennis Odhiambo (Pretoria University, South Africa), Yusuf Juma (Thika United);

Midfielders: - Titus Mulama (Sofapaka), Humphrey Mieno (Sofapaka), Collins Okoth (Gor Mahia), Stephen Waruru (Ulinzi Stars), Jamal Mohammed (Targu Mures, Romania), Stephen Ochola (Ulinzi Stars);

Strikers - Bob Mugalia (Sofapaka), Paul Were (Tusker), Victor Ochieng (Chemelil Sugar), Kevin Kimani (Mathare United);

Management; Francis Kimanzi (coach), Francis Baraza (assistant coach), Yusuf Chippo (assistant coach), Haggai Azande (goalkeeper coach), Wycliffe Makanga (doctor), Enos Karani "Bigi" (physiotherapist).

KIKOSI CHA TIMU YAIFA YA UGANDA

Abbey Dhaira, Robert Odongkara, Ali Kimera, Simeon Masaba, Godfrey Walusimbi, Habibu Kavuma, Isaac Isinde, Andy Mwesigwa, Henry Kalungi, Mike Mutyaba, Sula Matovu, Moses Oloya, Vincent Kayizzi, Dan Wagaluka, Tonny Mawejje, Mussa Mudde, Patrick Ochan, Brian Umony, Emma Okwi, Mike Sserumaga, Robert Ssentongo.

Monday, November 21, 2011

EMMANUEL EBOUE AFANYIWA VITENDO VYA KIBAGUZI NA MASHABIKI WA BASIKTAS NCHINI UTURUKI - APIGWA NA CHUPA ZA MAJI.

UCHAGUZI WA CECAFA KUFANYIKA NOVEMBA 24


Uchaguzi wa viongozi wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) utafanyika Novemba 24 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa sasa Leodegar Tenga ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) anatetea nafasi yake. Mpinzani wa Tenga ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Djibouti, Fadoul Hussein.

Nafasi nne za Kamati ya Utendaji zinagombewa na watu wanane. Wagombea hao ni Abdiqani Saeed Arab wa Somalia, Tariq Atta Salih (Sudan), Justus Mugisha (Uganda), Tesfaye Gebreyesus (Eritrea), Hafidh Ali Tahir (Zanzibar), Sahilu Wolde (Ethiopia), Raoul Gisanura (Rwanda) na Abubakar Nkejimana (Burundi).

Nayo kozi ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa ajili ya waamuzi watakaochezesha mashindano ya CECAFA Tusker Challenge Cup itafanyika Novemba 23 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Waamuzi walioteuliwa na CECAFA kuchezesha mashindano hayo ni Dennis Batte (Uganda), Bamlak Tessema (Ethiopia), Davis Omweno (Kenya), Wish Yabarow (Somalia), Israel Mujuni (Tanzania), Munyemana Hudu (Rwanda), Eric Gasinzigwa (Burundi) na Garvis Munyenziza (Rwanda).

Waamuzi wasaidizi ni Hassan Egueh (Djibouti), Clemence Erasmo (Tanzania), Idam Hamid (Sudan), Juma Ali Kombo (Zanzibar), Hamis Chang’walu (Tanzania), Yohanes Girmai (Eritrea), Brazan Mamati (Kenya), David Sagero (Kenya) na Mark Sonko (Uganda).

Pia waamuzi wote wa Tanzania wenye beji za FIFA nao watashiriki katika kozi hiyo.

CHELSEA YAFUNGWA NYUMBANI MFULULIZO KWA MARA YA KWANZA TANGU MIAKA 9 ILIYOPITA.


Chelsea 1 – 2 Liverpool 20-11-11 FULL HIGHLIGHTS... by garethbetty007


1 – Manchester City sasa ndio timu pekee ambayo haijafungwa katika Barclays premier league baada ya kuwa timu ya kwanza kuipa kipigo Newcastle United msimu huu.

2 – Ushindi wa Manchester United wa 1-0 dhidi ya Swansea City ulikuwa wa kwanza katika uwanja wa nyumbani wa timu inayotoka Wales katika mechi 9.

3 – Mshambuliaji wa Norwich City Steve Morison sasa amefunga katika mechi 3 za mwisho za EPL.

4 –Stoke City wamefungwa mechi zote nne za mwisho katika EPL, baada ya kufungwa na QPR 3-2 nyumbani kwao.

5 – Sunderland sasa wameshindwa kufunga katika mechi zao 5 za mwisho na Fulham kufuatia sare ya tasa katika uwanja wa Stadium of Light juzi Jumamosi.

6 – Straika wa Bolton Wanderers Ivan Klasnic sasa amefunga magoli sita katika mechi sita za mwisho za premier league alizoanza baada ya kufunga katika mechi waliyofungwa na 2-1 na West Bromwich Albion.

8 – Goli la penati la Mario Balotelli dhidi ya Newcastle United linamaanisha kuwa sasa amefunga magoli 8 katika mechi tisa zilizopita.

9 – Kufungwa 2-1 na Liverpool sasa kunamaanisha Chelsea wamefungwa mfululizo kwa mara ya kwanza katika miaka 6 na nusu tangu mwezi wanne na watano mwaka 2002 walipofungwa na Manchester United na Aston Villa @ Stamford Bridge.

31 – Magoli mawili ya Robin Van Persie at Norwich City yaliongeza idadi ya magoli kuwa 31 katika mwaka 2011, yakimfanya kuwa mchezaji wa tano wa pekee wa Premier league kufunga magoli 30 katika kalenda ya mwaka.

JULIO: BOBAN BADILI TABIA - ULITUMIKIE TAIFA LAKO VIZURI


Assistant coach wa timu ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Jamhuri Kihwelu 'Julio' amemtaka kiungo mshambuliaji wa Simba, Haruna Moshi 'Boban' kubadilika ili kuepukana na tuhuma mbalimbali zinazokua zikimkabili.

Mchezaji huyo amekuwa akikumbwa na kashfa mbalimbali, nje na ndani ya uwanja jambo ambalo linamfanya aonekana mtukutu machoni mwa wapenzi na mashabiki wa soka nchini huku wengine wakimuona kuwa ni mtovu wa nidhamu.

Julio alisema kuwa uwezo na kiwango cha Bobani ni cha juu na anastahili kuwa miongoni mwa wachezaji wa timu za taifa hata nchini lakini tabia yake ndiyo hasa inayomfanya ashindwe kupata nafasi hiyo.

"Hakuna mwenye wasiwasi na uwezo wa Boban, kila mmoja anayefuatilia soka anaijua soka yake, lakini tabia yake ndiyo tatizo hivyo anapaswa kubadilika na kuangalia mafanikio zaidi katika maisha yake ya soka.

"Kwa uwezo alionao hapaswi kuendelea kuwa hapa nchini hivyo namuomba ayatumie mashindano ya Chalenji kujitangaza na vilevile kuisaidia Tanzania Bara kutetea ubingwa wake," alisema Kihwelu ambaye kwa kauli hiyo, ni wazi wameshampitisha kuitumikia timu hiyo katika michuano ya Chalenji.

Katika hatua nyingine; Julio alisema kuwa ana matumaini makubwa na Boban pamoja na wachezaji wengine kuhakikisha Tanzania Bara inatetea ubingwa wake kwenye mashindano ya Chalenji yanayoanza kutimua vumbi Jumamosi ijayo Novemba 25.

Katika mashindano hayo Tanzania itaanza kutetea ubingwa wake kwa kupambana na Rwanda, Ethiopia na Djibouti katika hatua nya makundi.

FINALLY DAVID BECKHAM AMALIZA MKATABA WAKE NA LA GALAXY NA KOMBE

BABA NA MAMA YAKE BECKHAM WAKIWA NA MJUKUU WAO WAKIANGIALIA MECHI YA LA GALAXY NA HOUSTON DYNAMO
DAVID BECKHAM AKISHANGILIA UBINGWA WA MLS NA FAMILIA YAKE.

DAVID BECKHAM AKISHANGILIA PAMOJA NA WACHEZAJI WENZAKE.




HIGHLIGHTS YA LOS ANGELES GALAXY 1-0 HOUSTON DYNAMO

Sunday, November 20, 2011

SIMBA NA AZAM ZATINGA ROBO FAINALI UHAI CUP


Michuano ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 kwa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom imeingia hatua ya robo fainali ambayo itachezwa kesho (Novemba 21 mwaka huu) kwenye viwanja vya Karume na Azam ulioko Chamazi.

Oljoro JKT na Simba zitapambana saa 3 kamili asubuhi kwenye Uwanja wa Karume wakati katika muda huo huo kwenye Uwanja wa Azam kutakuwa na mechi kati ya JKT Ruvu Stars na Toto African.

Mechi nyingine zitachezwa saa 10 kamili jioni ambapo Serengeti Boyz (timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17) itaumana na Villa Squad kwenye Uwanja wa Karume. Uwanja wa Azam utashuhudia mechi kati ya Moro United na Azam.

Nusu fainali ya michuano hiyo itachezwa Novemba 23 mwaka huu Uwanja wa Karume ambapo mechi ya kwanza itakuwa saa 3 kamili asubuhi wakati ya pili itaanza saa 9.30 alasiri. Fainali itachezwa Uwanja wa Karume, Novemba 25 saa 9 kamili alasiri ikitanguliwa na mechi ya kutafuta mshindi wa tatu itakayoanza saa 3 kamili asubuhi.

Bingwa wa michuano hiyo inayodhamini na kampuni ya S.S. Bakhresa kupitia maji Uhai atapata sh. milioni 1.5, mshindi wa pili sh. milioni moja wakati wa tatu atapata sh. 500,000. Mbali ya fedha hizo, bingwa atapata medali za dhahabu, makamu bingwa medali za fedha na mshindi wa tatu medali za shaba.

Mchezaji bora sh. 400,000, mfungaji bora (sh. 300,000), kipa bora (sh. 300,000) na timu yenye nidhamu sh. 300,000.

KELVIN YONDAN BADO KIVUTIO KWENYE USAJILI YANGA


Wakati beki Kelvin Yondani akiandika barua ya kutaka kurejea Simba, bado ameendelea kuwa kivutio kwa klabu ya Yanga, ambayo kupitia Kamati ya Usajili imepanga kuanza mikakati ya kumsajili katikati ya mwaka ujao.

Yondani bado ana mkataba na klabu ya Simba unaotarajia kumalizika katikati ya mwezi ujao, lakini hata hivyo ameshindwa kucheza muda mrefu kutokana na matatizo na uongozi wa klabu yake.

Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Yanga Salim Rupia alisema, wameshindwa kumsajili Yondan katika kipindi hiki kwa sababu bado ana mkataba na klabu yake.

“Tulikuwa na nia hiyo ya kumsajili Yondan baada ya kupata taarifa kuwa hataki kuichezea timu ya Simba. Hata hivyo baada ya kufuatilia tuligundua ana mkataba na Simba na tukiamua kumsajili muda huu tutalazimika kulipa dau kubwa,” alisema Rupia.

Rupi alisema wanaheshimu mapendekezo ya kocha wao Mserbia Kostadin Papic, ambaye ndiye mwenye dhamana katika mambo yote ya usajili na wao watabaki kuwa washauri tu.

Aidha, Rupia alisema Papic amefanya mazungumzo na kiungo wa zamani wa timu hiyo, Athuman Idd ‘Chuji’ lengo likiwa ni kuangalia uwezekano wa kumrudisha kikosini kwa vile bado ana uwezo iwapo atafanya mazoezi vizuri.

“Kuna uwezekano mkubwa Chuji kurejea Yanga wakati wa duru la pili la Ligi Kuu. Kocha Papic ameshafanya mazungumzo na mchezaji huyo na kumpa masharti ili aweze kurejesha,” alisema Rupia.

Hata hivyo Rupia hakuwa tayari kusema aina ya masharti aliyopewa Chuji na Papic. “Waliyoongea na Chuji kama sehemu ya masharti yanabaki kuwa siri kati ya Chuji na kocha mwenyewe,” alisema zaidi.

AC MILAN YASHIKWA NA FIORENTINA


Ίντερ - Κάλιαρι 2-1 by buitre9

INTER MILAN 2-1 CAGLIARI


Ίντερ - Κάλιαρι 2-1 by buitre9

VAN 'MAGOLI' PERSIE AZIDI KUIPASHA ARSENAL


Norwich 1 vs 2 Arsenal Barclays Premier League by somaliflag

BAYERN MUNICH WACHAPWA NA DORTMUND


Bayern Munich 0 – 1 Borussia Dortmund 19-11-11... by sagolerbaccha

MAN CITY HAWASHIKI, YAICHAPA 3-1 NEWCASTLE


Man City 3 vs 1 Newcastle Barclays Premier... by somaliflag

CHICHARITO AIPA USHINDI MAN UNITED DHIDI YA SWANSEA


swansea v mu motd by unitedzonetv

REAL MADRID 3-2 VALENCIA, BARCA 4-0 ZARAGOZA



Saturday, November 19, 2011

GOLI LA TICK TAK LA ROONEY VS MAN CITY KUGOMBANIA TUZO YA FIFA

Goli la mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney alilolifunga dhidi ya Manchester City msimu uliopita limewekwa katika orodha ya magoli yanayoshindania tuzo ya goli la mwaka la FIFA.

Goli la Rooney ambalo lilitokana na krosi kutoka kwa Nani katika mechi ambayo United waliwafunga mahasimu wao City, lilimuacha Joe Hart akiwa hana la kufanya wakati mpira ukiingia pembeni mwa nyavu.

Mchezaji wa Tottenham Giovan dos Santos, Barcelona star Lionel Messi na mshambuliaji wa AC Milan Zlatan Ibrahimovic na mshambuliji wa Santos kinda Neymar, wote wametajwa katika kugombea tuzo hiyo maarufu kwa jina la Puskas award.

Dos Santos alifunga goli lake katika mechi kati ya Mexico dhidi ya United States, Messi na goli lake la kwanza dhidi ya Arsenal katika Champions league, Ibrahimovic akifunga katika mechi kati AC Milan vs Lecce, huku Neymar akiingia na goli alilofunga katika mpambano kati ya Santos na Flamengo.

FIFA 2011 Puskas award, ambayo hutolewa kwa heshima ya mchezaji wa Hungary Puskas, itatolewa mwezi January tarehe 9, na mchezaji aliyeshinda mwaka jana alikuwa Hamit Altintop

HAYA NDIO MAGOLI YALISHINDANA MWAKA JANA.

GIGGS, ZIDANE, MESSI, GERRARD WATAJWA KAMA WACHEZAJI BORA WA HISTORIA YA CHAMPIONS LEAGUE

Welsh wizard: Giggs is the best British player to feature in the tournament

Winga wa Manchester United Ryan Giggs ametajwa kama mchezaji aliyeshika nafasi ya 6 katika listi ya wachezaji bora wa muda wote ligi ya mabingwa wa ulaya, kutokana na jarida rasmi la michuano hiyo.

The Welshman ndio muingereza aliyeshika nafasi ya juu katika listi hiyo inaundwa na wachezaji 50 ambayo Steven Gerrard nae amaeshika nafasi ya 10, huku wachezaji wengine wa United Paul Scholes na David Beckham wakiwemo katika 20 bora.

Giggs ambaye amelibeba kombe la ulaya mwaka 1999 na 2008 ndio mchezaji mwenye umri mkubwa kufunga bao katika michuano hiyo na maefunga katika misimu mingi zaidi kuliko mchezaji yoyote.

Mchezaji aliyeshika nafasi ya kwanza ni Zinedine Zidane ambaye goli lake kwa Madrid dhidi ya Bayern Leverkusen katika fainali ya 2002 litakumbukwa kama bao bora katika historia ya michuano hiyo.

Lionel Messi mshindi wa mara mbili wa kombe hilo akiwa na Barcelona, anafuatia katika nafasi ya pili, huku Paolo Maldini, Xavi na Raul - mfungaji bora anayeongoza akiwa na magoli 71 wakikamilisha top 5.

LISTI KAMILI IPO KAMA IFUATAVYO.

1. Zinedine Zidane
2. Lionel Messi
3. Paolo Maldini
4. Xavi
5. Raul
6. Ryan Giggs
7. Clarence Seedorf
8. Luis Figo
9. Samuel Eto'o
10. Steven Gerrard
11. Andres Iniesta
12. Oliver Kahn
13. Andriy Shevchenko
14. Paul Scholes
15. Javier Zanetti
16. Alessandro Del Piero
17. Iker Casillas
18. David Beckham
19. Thierry Henry
20. Ronaldo
21. Carlos Puyol
22. Edwin van der Sar
23. Andrea Pirlo
24. Didier Deschamps
25. Alessandro Nesta


26. Fernando Redondo
27. Wayne Rooney
28. Frank Rijkaard
29. Kaka
30. Cristiano Ronaldo
31. Ruud van Nistelrooy
32. Roberto Carlos
33. Marcel Desailly
34. Jari Litmanen
35. Peter Schmeichel
36. Flippo Inzaghi
37. Dejan Savicevic
38. Gaizka Mendieta
39. Roy Keane
40. Claude Makelele
41. Fernando Hierro
42. Edgar Davids
43. Gianluigi Buffon
44. Stefan Effenberg
45. Ronaldinho
46. Deco
47. Lothar Matthaus
48. Frank Lampard
49. Fernando Morientes
50. Paulo Sousa



Friday, November 18, 2011

FERGIE: SIMUUZI BERBATOV, ATAENDELEA KUWA HAPA MWAKA 1 ZAIDI.


Kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson amesema anataka kuendelea kumfundisha Berbatov at Carrington atleast kwa mwaka mmoja zaidi.

Berbatov ambaye alinunuliwa kwa ada iliyoweka rekodi kwa klabu hiyo ya £30.75million amejikuta akipoteza namba kwa makinda Javier Hernandez na Danny Welbeck katika msimu huu unaoendelea.

Hali hii imepelekea kuzuka kwa minong’ono kuwa Ferguson anatarajiwa kumuuza mshambuliaji huyo wakati wa dirisha dogo mwezi January.

Ingawa, United Boss amesisitiza hilo halitotokea.

Badala yakeinaonekana Fergie anataka kumuongezea mkataba Mbulgaria huyo kwa msimu mmoja zaidi.

“Dimitar yupo katika mipango yangu, Nimekuwa nikisoma baadhi ya magazeti kuwa nitamuuza lakini siioni sababu yoyote kwangu mimi kumuachia aondoke.

“Ni mchezaji mzuri na nitamuongeza mkataba wa mwaka mmoja zaidi. Ni bahati mbaya kwamba form ya Hernandez kuanzia last year imekuwa nzuri sana lakini anacheza vizuri na anajituma mazoezini.

“Hana manung’uniko yoyote. Huyu ni professional wa kweli na tuna furaha yupo hapa. Unahitaji washambuliaji wengi wazuri siku hizi. Kama utakumbuka mwaka 1999, tulikuwa na washambuliaji wanne wazuri na wote walitumika ipasavyo, ni hivyo ndivyo hali ya sasa.” –Alisema Ferguson.

MAN CITY YAVUNJA REKODI KWA HASARA YA £195 MILLION.


Klabu ya Manchester City imetangaza imepata hasara ya kiasi cha £195.9 million.

Hasara hii imevunja rekodi kwa kuwa kubwa kuwahi kutokea kwa vilabu vya premier league, ikionyesha namna ya uwekezaji mkubwa wa Sheikh Mansour katika kuitoa City kuwa kuwa klabu ya kawaida in 2008 mpaka kuwa viongozi wa EPL kwa msimu huu.

City hawana budi kushukuru mungu, kwa kuwa figures hizi hazitokuweza kuguswa na sheria mpya ya UEFA juu ya matumizi ya pesa kwasababu matumizi haya yalifanyika kabla ya kupitishwa kwa sheria hii ambayo itaanza kutumika kwa vilabu vyote vinavyoshiriki michuano ya ulaya kuanzia msimu wa 2014-15.

UEFA wata-monitor akaunti za vilabu katika miaka mitatu kuelekea msimu huo wa 2014-15 – ukianza na msimu huu unaoendelea.

Katika sheria hiyo, vilabu vinaruhusiwa kupata hasara isiyozidi £38.5m kwa jumla ndani ya miaka 3. Hii ni moja ya njia ya UEFA kuweza kupunguza matumizi katika ada za usajili na mishahara ambayo imekuwa ikitolewa na vilabu.

City chini ya Billionea wa biashara ya mafuta kutoka Uarabuni Sheikh Mansour wameoata hasara ambayo imeweza kuifunika ya Roman Abromavich ya £141 in 2005, mwaka wa pili tangu ainunue Chelsea.

Hasara ya City imetokana na kuwekeza fedha nyingi katika kununua wachezaji wa daraja la dunia kama Edin Dzeko £27m, David Silva £26m, Yaya Toure £24m, Kolarov £19m, Mario Balotelli £24 na James Milner £26m, jumla ya fedha zilizotumika kwa wachezaji hawa ni £156m.

SIMBA KUTIMIZA MIAKA 75, ASANTE KOTOKO YAALIKWA KATIKA SHEREHE


Klabu ya Simba inatarajia kufanya sherehe za kutimiza miaka75 ya klabu hiyo mapema mwezi ujao na itazialika klabu mashuhuri kwa ajili ya maadhimisho hayo baada ya kumalizika michuano ya Chalenji.

Ofisa Habari wa Klabu ya Simba, Ezekiel Kamwaga alisema jana kuwa shughuli hiyo itafanyika jijini Dar es Salaam ikiambatana na kusoma dua kwa wale waliotangulia mbele za haki walioitumikia Simba kwa njia moja ama nyingine.

Alisema kuwa wamekwishatuma mialiko mbalimbali kwa timu watakazoalika ikiwamo Asante Kotoko ya Ghana..

Hata hivyo, Kamwaga alisema kuwa ni mapema kufahamu ni timu zipi watazialika lakini wanatarajia kuanza mchakato wa kutuma barua za mialiko kwa baadhi ya timu hasa za ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati.

Wakati huo huo klabu ya Asante Kotoko ya nchini Ghana imethibitisha kucheza mchezo wa kirafiki na klabu za Simba na Yanga katika kutimiza miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.