Search This Blog

Tuesday, November 22, 2011

CHELSEA YAMTAKA GARY CAHIL KUTATUA TATIZO LA ULINZI .


Under fire Chelsea coach Andre Villas-Boas anajipanga kuvunja bank na kumnunua beki wa kati wa England na klabu ya Bolton Gary Cahil, ili kuweza kutatua matatizo ya safu ya ulinzi yanayoikabili timu yake.

Cahil, 25, anamaliza mkataba wake katika kipindi cha kiangazi kinachokuja hivyo thamni yake inaweza kupungua kufikia £8million wakati dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa mwezi Janaury mwakani.

Chelsea wameruhusu wavu wao kuguswa mara 17 katika mechi zao 12 za ligi msimu na wameweza kupata clean sheet mbili tu, wakiwa wanahangaika ku-adapt mbinu mpya za Andre Villa-Boas.

John Terry akiwa anaandamwa na matatizo ya kashfa ya ubaguzi wa rangi na kupoteza umakini, David Luiz akiwa out of form, na Alex akitegemewa kutaka kuondoka in January, Villa-Boas analazimika kuongeza options za mabeki

Bolton walikataa ofa mbalimbali kutoka Arsenal na Tottenham kipindi cha usajili kilichopita, lakini sasa wapo radhi kusikiliza ofa kwa ajili ya Cahil kuliko kumpoteza bure mkataba wake utakapoisha mwishoni mwa msimu huu.

No comments:

Post a Comment