Search This Blog

Tuesday, November 22, 2011

WENGER ASHINDWA KUKANUSHA KUMHITAJI MARIO GOTZE


Kocha Arsene Wenger amekataa kupinga uvumi kwamba anajipanga kupeleka ofa ya kumnunua star wa Borussia Dortmund Mario Gotze.

Arsenal wanawakaribisha mabingwa wa Ujerumani katika uwanja wa Emirates kesho jumatano katika mchezo wao muhimu wa hatua ya makundi ya champions league, huku wakihitaji ushindi kujihakikishia nafasi ya kupita kucheza hatua ya mtoano.

Wenger anatambua uwezo wa Dortmund ambao walitoka nao sare ya 1-1 mwezi Septmber, alkini kocha huyu mfaransa mabingwa hao wa Bundesliga nguvu kubwa ipo kwa mchezaji tegemeo Mario Gotze, kiungo ambaye Wenger ameonekana kumhitaji katika kikosi chake.

“Tuna kikosi kikubwa na kwa muda huu hatuna mchezaji tunayemfuatilia. Gotze ni mchezaji mzuri na naelewa kwamba amekuwa akivizutia timu nyingi barani ulaya. Kwa upande wetu, sifikiri kama sasa ni muda muafaka kuongelea kuhusu kumsajili Gotze wakati kesho tunacheza dhidi ya Dortmund, hivyo inabidi tuweke umakini katika mchezo huo muhimu na sio uhamisho.”

Gotze anatajwa kuwa na thamani ya £30 million, fedha ambayo ipo nje ya sera ya ada ya uhamisho ya klabu ya Arsenal ambayo mpaka sasa mchezaji aliyeghali zaidi kwenye kikosi chao ni Andrey Arshavin aliyewagharimu kiasi cha £15million.

No comments:

Post a Comment