Search This Blog

Friday, November 18, 2011

MAN CITY YAVUNJA REKODI KWA HASARA YA £195 MILLION.


Klabu ya Manchester City imetangaza imepata hasara ya kiasi cha £195.9 million.

Hasara hii imevunja rekodi kwa kuwa kubwa kuwahi kutokea kwa vilabu vya premier league, ikionyesha namna ya uwekezaji mkubwa wa Sheikh Mansour katika kuitoa City kuwa kuwa klabu ya kawaida in 2008 mpaka kuwa viongozi wa EPL kwa msimu huu.

City hawana budi kushukuru mungu, kwa kuwa figures hizi hazitokuweza kuguswa na sheria mpya ya UEFA juu ya matumizi ya pesa kwasababu matumizi haya yalifanyika kabla ya kupitishwa kwa sheria hii ambayo itaanza kutumika kwa vilabu vyote vinavyoshiriki michuano ya ulaya kuanzia msimu wa 2014-15.

UEFA wata-monitor akaunti za vilabu katika miaka mitatu kuelekea msimu huo wa 2014-15 – ukianza na msimu huu unaoendelea.

Katika sheria hiyo, vilabu vinaruhusiwa kupata hasara isiyozidi £38.5m kwa jumla ndani ya miaka 3. Hii ni moja ya njia ya UEFA kuweza kupunguza matumizi katika ada za usajili na mishahara ambayo imekuwa ikitolewa na vilabu.

City chini ya Billionea wa biashara ya mafuta kutoka Uarabuni Sheikh Mansour wameoata hasara ambayo imeweza kuifunika ya Roman Abromavich ya £141 in 2005, mwaka wa pili tangu ainunue Chelsea.

Hasara ya City imetokana na kuwekeza fedha nyingi katika kununua wachezaji wa daraja la dunia kama Edin Dzeko £27m, David Silva £26m, Yaya Toure £24m, Kolarov £19m, Mario Balotelli £24 na James Milner £26m, jumla ya fedha zilizotumika kwa wachezaji hawa ni £156m.

No comments:

Post a Comment