Search This Blog

Friday, November 18, 2011

FERGIE: SIMUUZI BERBATOV, ATAENDELEA KUWA HAPA MWAKA 1 ZAIDI.


Kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson amesema anataka kuendelea kumfundisha Berbatov at Carrington atleast kwa mwaka mmoja zaidi.

Berbatov ambaye alinunuliwa kwa ada iliyoweka rekodi kwa klabu hiyo ya £30.75million amejikuta akipoteza namba kwa makinda Javier Hernandez na Danny Welbeck katika msimu huu unaoendelea.

Hali hii imepelekea kuzuka kwa minong’ono kuwa Ferguson anatarajiwa kumuuza mshambuliaji huyo wakati wa dirisha dogo mwezi January.

Ingawa, United Boss amesisitiza hilo halitotokea.

Badala yakeinaonekana Fergie anataka kumuongezea mkataba Mbulgaria huyo kwa msimu mmoja zaidi.

“Dimitar yupo katika mipango yangu, Nimekuwa nikisoma baadhi ya magazeti kuwa nitamuuza lakini siioni sababu yoyote kwangu mimi kumuachia aondoke.

“Ni mchezaji mzuri na nitamuongeza mkataba wa mwaka mmoja zaidi. Ni bahati mbaya kwamba form ya Hernandez kuanzia last year imekuwa nzuri sana lakini anacheza vizuri na anajituma mazoezini.

“Hana manung’uniko yoyote. Huyu ni professional wa kweli na tuna furaha yupo hapa. Unahitaji washambuliaji wengi wazuri siku hizi. Kama utakumbuka mwaka 1999, tulikuwa na washambuliaji wanne wazuri na wote walitumika ipasavyo, ni hivyo ndivyo hali ya sasa.” –Alisema Ferguson.

No comments:

Post a Comment