Search This Blog

Friday, November 18, 2011

SIMBA KUTIMIZA MIAKA 75, ASANTE KOTOKO YAALIKWA KATIKA SHEREHE


Klabu ya Simba inatarajia kufanya sherehe za kutimiza miaka75 ya klabu hiyo mapema mwezi ujao na itazialika klabu mashuhuri kwa ajili ya maadhimisho hayo baada ya kumalizika michuano ya Chalenji.

Ofisa Habari wa Klabu ya Simba, Ezekiel Kamwaga alisema jana kuwa shughuli hiyo itafanyika jijini Dar es Salaam ikiambatana na kusoma dua kwa wale waliotangulia mbele za haki walioitumikia Simba kwa njia moja ama nyingine.

Alisema kuwa wamekwishatuma mialiko mbalimbali kwa timu watakazoalika ikiwamo Asante Kotoko ya Ghana..

Hata hivyo, Kamwaga alisema kuwa ni mapema kufahamu ni timu zipi watazialika lakini wanatarajia kuanza mchakato wa kutuma barua za mialiko kwa baadhi ya timu hasa za ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati.

Wakati huo huo klabu ya Asante Kotoko ya nchini Ghana imethibitisha kucheza mchezo wa kirafiki na klabu za Simba na Yanga katika kutimiza miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.

2 comments:

  1. Jamani Simba yangu hizo pesa zitakazopatikana kwenye mechi za miaka 75 mzitumie angalau kwenye project ya uwanja wenu,mjifunze toka TP MAZEMBE.Sisi tumekuwa watu wa sherehe tu,kuanzia serikali mpk wananchi na wizara.

    ReplyDelete
  2. Sherehe pekee hazitoshi,onyesheni kukomaa kisoka kila siku malumbano timu ikifanya vibaya mchawi fulan,kwa staili hiyo ni kama walewale wa miaka 50 ya uhuru umaskin mpaka hauna dalili ya kuondoka.james veta mwanza

    ReplyDelete