Search This Blog

Saturday, November 19, 2011

GOLI LA TICK TAK LA ROONEY VS MAN CITY KUGOMBANIA TUZO YA FIFA

Goli la mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney alilolifunga dhidi ya Manchester City msimu uliopita limewekwa katika orodha ya magoli yanayoshindania tuzo ya goli la mwaka la FIFA.

Goli la Rooney ambalo lilitokana na krosi kutoka kwa Nani katika mechi ambayo United waliwafunga mahasimu wao City, lilimuacha Joe Hart akiwa hana la kufanya wakati mpira ukiingia pembeni mwa nyavu.

Mchezaji wa Tottenham Giovan dos Santos, Barcelona star Lionel Messi na mshambuliaji wa AC Milan Zlatan Ibrahimovic na mshambuliji wa Santos kinda Neymar, wote wametajwa katika kugombea tuzo hiyo maarufu kwa jina la Puskas award.

Dos Santos alifunga goli lake katika mechi kati ya Mexico dhidi ya United States, Messi na goli lake la kwanza dhidi ya Arsenal katika Champions league, Ibrahimovic akifunga katika mechi kati AC Milan vs Lecce, huku Neymar akiingia na goli alilofunga katika mpambano kati ya Santos na Flamengo.

FIFA 2011 Puskas award, ambayo hutolewa kwa heshima ya mchezaji wa Hungary Puskas, itatolewa mwezi January tarehe 9, na mchezaji aliyeshinda mwaka jana alikuwa Hamit Altintop

HAYA NDIO MAGOLI YALISHINDANA MWAKA JANA.

1 comment:

  1. Hi, this weekend is fastidious for me, for the reason that this time i am reading this great educational
    post here at my residence.
    Look into my weblog - pet insurance

    ReplyDelete