Search This Blog

Thursday, June 7, 2012

Euro 2012: UBAO WA TAKWIMU ZA WACHEZAJI!

Euro 2012 Focus: Player Stats Leaderboards
Euro 2012 Focus: Player Stats Leaderboards
Euro 2012 Focus: Player Stats Leaderboards
Euro 2012 Focus: Player Stats Leaderboards
Euro 2012 Focus: Player Stats Leaderboards

TETESI : JUMA NYOSO HUYOO YANGA

TAARIFA NILIZOZIPATA HIVI PUNDE BEKI WA SIMBA JUMA NYOSSO MUDA WOWOTE KUANZIA HIVI SASA HUENDA NAYE AKASINI KWA AJILI YA KUJIUNGA NA YANGA.
TAARIFA NILIZOZIPATA KUTOKA KWENYE CHANZO CHA KUAMINIKA KIKOSI KAZI CHA YANGA TAYARI KIPO KWENYE KAMBI YA TIMU YA TAIFA KWA AJILI YA KUMALIZANA NA BEKI HUYO .

EURO 2012: ITALIA NA SAFU YA USHAMBULIAJI YA WENDAWAZIMU CASSANO NA BALOTELLI.

Maneno ya Cesare Prandelli alipomrithi Marcello Lippi kama kocha wa timu ya taifa baada ya kombe la dunia mwaka 2010 ni kwamba ataifanya Azzuri ivutiwa kwa kucheza soka zuri la kushambulia. Kwa hakika amejitahidi sana huku akitambulisha utaratibu wa 'ethical code' (wachezaji wanaokuwa wamesimamishwa kwa makosa ya kinidhamu hawatoitwa timu ya taifa) na kusisitiza katika kuwapa nafasi zaidi viungo wenye ufundi zaidi katika timu yake. Wazo ni kuifanya Italia kucheza kwa staili yake ya mfumo wa tiki-taka, staili inayopendelewa zaidi na Wahispania.

Akiuacha mfumo wa siku nyingi wa kujenga ukuta wa chuma na kucheza kwa mashambulizi ya kushtukiza kwa ajili ya mfumo ambao unatumia na Spain, ambao mpaka sasa umeleta matokeo ya mchanganyiko. italy haikufungwa hata mechi moja kwenye hatua ya kufuzu, lakini wamekuwa wakifungwa kwenye mechi za kirafiki. Skendo ya upangaji wa matokeo ambayo inaliandama soka la nchi hiyo kwa miaka mingi sasa, haitegemewi kuwa na madhara makubwa sasa hivi kuliko ilivyokuwa katika miaka 1982 na 2006, sababu kubwa ni kwa kuwa ni wachezaji wachache wa kikosi cha sasa wameguswa na kashfa hiyo, lakini suala hilo bado linabakia kuwa sio zuri kwa wachezaji.

Droo ya group C haikuwa nzuri kwa Italy, lakini atleast mechi yao dhidi ya Spain itakuwa ya kwanza. Na kupata pointi kutoka kwenye mechi hiyo ni jambo ambalo linawezekana, kwa kuangalia Spain huwa na kawaida ya kuanza vibaya michuano mikubwa, ukiangalia kombe la dunia lilopita walipofungwa na Uswis katika mechi ya kwanza makundi. Baada ya mechi hiyo atleast kidogo mambo yanaweza kuwa mazuri dhidi ya Croatia na Ireland.

WACHEZAJI MUHIMU

Gianluigi Buffon
Nahodha amerudi kwenye kiwango chake baada ya majeruhi yaliyomkumba msimu wa  2010-11. Ukifikiria namna safu ya ulinzi ilivyokuwa dhaifu, Azzuri wanahitaji kuwa na Buffon mwenye kiwango cha juu ili kuepeuka balaa. Ni uchizi sasa kufikiri kwamba safu ya ulinzi ambayo siku zote imekuwa ndio nguzo ya timu ya taifa ya Italia, sasa hivi ndio ulipo udhaifu wao, lakini hapa ndipo tulipo, na sasa tumaini lote lipo kwa Buffon na mikono pamoja na miguu yake kutatua hilo tatizo.


Mario Balotelli
Mario Balotelli alisema hatoshangilia goli mpaka atakapofunga goli la ushindi kwenye world cup au Euro, hivyo hii ndio nafasi pekee kumuona Super Mario akicheza kwa furaha baada ya kutupia kambani. Tuache utani, huu ni muda wake kuweza kuonyesha kwanini makocha wamuamini na kumpa nafasi. Balotelli ana nguvu, ujuzi na kimo kizuri, Anachohitaji ni kutulia na kutumia vizuri nafasi atakazopata huku akijiepusha na suala la nidhamu mbovu. Akifanikiwa kwenye hayo atatisha.


Daniele De Rossi
Katika kiungo ambacho kimejaa wapiga pasi mafundi zaidi, De Rossi ndio kiumbe anayetegemewa kusambaza minguvu yake. Shujaa huyu wa Roma ndio sasa anaelekea kwenye kilele chake, akiwa ameshaji-commit kwenye klabu yake, sasa yupo huru kufikiria timu ya taifa tu. Atakuwa na shughuli ngumu katika kupambana na kuizuia safu ya ulizni wa timu ambayo ni dhaifu kutoguswa

 JE SAFU YA USHAMBULIAJI YA MACHIZI ITAFANYA VIZURI?
Mara tu Giueseppe Rossi alipoumia, mikono ya Prandelli ilikuwa imefungwa. Akawa hana chaguo lingine zaidi ya kuwatumia Balotelli na Antonio Cassano. Hii haihusu suala la uwezo  - -wachezaji wote wawili wana vipaji vikubwa tataizo ni nidhamu: wote wawili wana matukio mengi ambayo yanahusu ukosefu wa nidhamu na tabia nyingine tofauti,ndani na nje ya uwanja. Hivyo hilo ni tatizo ambalo Prandelli inabidi alitafutie suluhisho.

HUU NDO MKATABA WA KELVIN YONDANI NA SIMBA SC.


COPA COCA-COLA TAIFA KUANZA KUTIMUA VUMBI JUNI 24

Michuano ya Copa Coca-Cola ngazi ya Taifa inaanza kutimua vumbi Juni 24 mwaka huu kwenye mikoa ya Dar es Salaam na Pwani huku pambano la ufunguzi likiwa kati ya Kigoma na Lindi litakalofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.

Upangaji ratiba (draw) umefanyika leo (Juni 7 mwaka huu) kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kushuhudiwa na waandishi wa habari, makocha wa timu za mikoa za Copa Coca-Cola na wadhamini kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola.

Makocha 35 wa timu za Copa Coca-Cola kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani wako kwenye kozi ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) inayoendeshwa na wakufunzi Ulric Mathiot wa FIFA kutoka Seychelles na wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Sunday Kayuni wa Tanzania.

Mikoa 28 ya kimpira ya Tanzania itashiriki katika mashindano hayo na imegawanywa katika makundi manne ya timu saba saba. Baadaye timu zitapambana katika hatua ya robo fainali, nusu fainali na fainali itakayofanyika Julai 15 mwaka huu.

Kundi A lina timu za Arusha, Ilala, Kigoma, Kusini Pemba, Lindi, Rukwa na Ruvuma. Kundi B ni Iringa, Kaskazini Pemba, Manyara, Mjini Magharibi, Morogoro, Mwanza na Tanga. Dodoma, Kaskazini Unguja, Kinondoni, Mara, Mbeya, Mtwara na Temeke ziko kundi C wakati kundi D ni Kagera, Kilimanjaro, Kusini Unguja, Pwani, Shinyanga, Singida na Tabora.

Viwanja vitakavyotumika katika mashindano hayo ambapo mechi zitakuwa zikichezwa asubuhi (saa 2.30) na jioni (saa 10.00) ni Uwanja wa Karume na Tanganyika Packers (Kawe) kwa Dar es Salaam. Viwanja vya Mkoa wa Pwani ni Tamco na Nyumbu. Timu zote katika mashindano hayo zitacheza katika viwanja hivyo.

Mbali ya Kigoma na Lindi, mechi nyingine za ufunguzi Juni 24 mwaka huu ni kundi B Morogoro na Manyara (saa 2.30 asubuhi Uwanja wa Kawe), kundi C ni Temeke na Kinondoni (saa 2.30 asubuhi Uwanja wa Nyumbu) na kundi D ni Kilimanjaro na Kusini Unguja (saa 2.30 asubuhi Uwanja wa Tamco).

Wachezaji wanaotakiwa kushiriki kwenye michuano hiyo ya umri chini ya miaka 17 ni wale waliozaliwa kuanzia Januari 1, 1996.

SAKATA HILI LA YONDANI KWA UPANDE MWINGINE LIMECHANGIWA NA SERA MBOVU YA USAJILI YA SIMBA!

Sakata la usajili wa Kelvin Yondani limetokea kuteka hisia za wengi katika kipindi cha masaa 48. Taarifa ambazo zimetapakaa kwenye vyombo ya habari zinasema kuwa Dar es salaam Young Africans imekamilisha usajili wa Yondani huku nakala ya mkataba wake alioingia na klabu hiyo ukionyesha kuwa amesaini kuichezea Yanga kwa miaka miwili huku akitia kibindoni kiasi cha Milioni 30 huku mshahara wake ukiwa laki nane kwa mwezi.
Upande wa pili wa sinema hii ambao ni klabu anayodaiwa kutoka Yondani ya Simba Sports unadai kuwa Yondani aliongeza mkataba wake wa awali na klabu hiyo kabla hata ya mwisho wa msimu huu uliopita.
Kikubwa kinachonitatiza ni sera ya usajili ya klabu ya Simba ambayo ndio hasa mjadala mkuu kwenye makala haya.
Tukirudi nyuma msimu uliopita Simba ilitangaza kumuacha beki wake wa kati Meshack Abel . Ukiangalia takwimu za michezo ya Simba kwa kipindi cha miaka miwili iliopita utagundua kuwa moja ya matatizo sugu imekuwa safu ya ulinzi, hata hivyo Meshack Abel ni mmoja ya mabeki wa kati shupavu ambao hata kwenye timu ya taifa wamekuwepo kwa kipindi kirefu. Baada ya kumuacha Abel simba iliwasajili Obadia Mungusa na Victor Costa. Hiki ni kipindi ambacho Kevin Yondani alikuwa froze out of the team (inasemekana alikuwa na beef na mmoja wa viongozi).  Smba pia kwa sababu zisizojulikana iliamua pia kumuacha beki wa pembeni kulia Haruna Shamte wakati ambapo alikuwa anachipukia na tayari alikuwa ameanza kuitwa kwenye timu ya taifa  pamoja na kuwa mdogo kiumri.
Mbdala wa Shamte alikuwa beki wa zamani Nasor Masoud Cholo aliyerudishwa toka JKT Oljoro na Shomari Kapombe ambaye awali alisajiliwa kama kiungo ilia ni uwezo wake au versatility yake ambayo imeshuhudia akirudishwa nyuma kucheza wakati mwingine kama beki wa kati na pembeni.
Tetesi ambazo tunazisikia sasa ni kwamba ,Juma Jabu,Obadia Mungusa na Victor Costa wameachwa huku Juma Nyoso naye akiwa mbioni kuachwa na sababu tunayoambiwa ni kwamba amekuwa akiigharimu timu mara kwa mara. Tubaki hapa kwa Nyoso kwanza , huyu ni mmoja wa wachezaji waliotokea kuwa kipenzi cha mashabiki wa Simba kutokana na umahiri kwenye eneo lake na hata ukiangalia kwenye timu ya taifa Nyoso amekuwa akiitwa mara kwa mara hali inayoonyesha kuthaminiwa kwa mchango wake , nyoso pia ni mmoja wa wachezaji ambao wameiwakilisha  Simba kwenye michezo karibu yote kwenye ligi na kimataifa . Nyoso pia ni nahodha wa tatu Simba baada ya Kaseja na Boban. Swali la kijiuliza ni je mchezaji huyu ambaye ametokea kuwa senior player Simba anastahili kutupiwa virago kweli? Eti wanasema kuwa anaigharimu timu kwa kadi nyekundu. ntakurudisha nyuma unakumbuka wakati Fernando Torres anacheza Liverpool,kuna wakati kwenye michezo mitano mfululizo ya United na Liverpool Torres alikuwa anafunga kwa kumpita Nemanja Vidic na zaidi ya hapo Vidic amewahi kuonyeshwa kadi nyekundu katika michezo mitatu mfululizo dhidi ya Liverpool,United ilimfukuza? Jibu ni hapana , kwa hali ya kawaida mwanadamu huwa anapima mema na mabaya au faida na hasara yaani profit vs losses kwa kufanya uwiano , Simba imetwaa ubingwa msimu huu hivyo kwa uwiano halisi tu kadi nyekundu kwa nyoso hata zingekuwa kumi bado sio sababu kwa kuwa Simba imemaliza kwa kutwaa taji.
Turudi kwa mtazamo wa jumla ,kuanzia kwa Meshack Abel,Costa,Jabu,Obadiah,Nyoso ,Haruna na Shamte labda na hili la Yondani,. Kuachwa kwa wote hawa kunamaanisha kuwa Simba inapoteza zaidi ya asilimia 70 ya backline yake baada ya kuwa imetwaa ubingwa na kumaliza nafasi ya pili msimu uliopita tena huku ikiwa sawa na timu iliyotwaa ubingwa ,je hii ni sera nzuri ya usajili ambayo inafanya kazi hapa ???
Tukiachana na hayo huku na kule kuna tetesi kuwa Salum Machaku anapelekwa timu nyingine kwa mkopo. Machaku amesajiliwa msimu uliopita toka Mtibwa. Amecheza Simba msimu mmoja ambao Simba imetwaa ubingwa huku ikifika hatua ya mbali kwenye michuano ya kimataifa . Of course tatizo la machaku limekuwa kushuka na kupanda kwa kiwango pasipo kuwa na muendelezo yaani consistency,lakini tusisahau kuwa huu ni msimu wake wa kwanza , ni vigumu kwa mchezaji ku-settle kwenye msimu wa kwanza ,kwanini amehukumiwa na kuonekana hapaswi kupewa nafasi ya pili ya kujidhatiti kwenye Timu.
Majibu ya maswali yote haya ni rahisi sana, Simba haina sera nzuri ya usajili,maamuzi ya kusajili na kuacha wachezaji yanafanyika kiholela holela sana , hata hili la Yondani ukichunguza kwa ukaribu chanzo ni Simba wenyewe , Yondani alikuwa nje ya timu kwa muda mrefu , taarifa zinasema kuwa klabu ilikuwa haimlipi mshahara , Yanga walionyesha interest ya kumsajili siku nyingi , kilichokuwa kinambana ni mkataba lakini alikuwa frustrated sana na ndio maana akasaini yanga baada ya kuonyeshwa fedha ambazo hakuwa amepewa na Simba . Ukiritimba kama huu ndio unaendelea kulihikumu soka la Tanzania na kwa mtaji huu maendeleo tutayasikia kwa wenzetu kina Mariga, Oliech na Obua.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

   SIMBA SPORTS CLUB           
P.O.BOX 15318 | TEL+255 222183330 |FAX +255 222183330 |MSIMBAZI/MCHIKICHI STREET | DAR ES SALAAM | TANZANIA | EMAIL   simbasportsclub@yahoo.com|WEBSITE www.simba.co.tz| AFFILIATED TO TFF, DRFA and IDFA

                                
Simba Sports club imesikitishwa na kitendo cha Young Africans kuvunja taratibu za usajili kwa kumrubuni mchezaji wake Kelvin Patrick Yondani  kwa kuzungumza naye na baadae kwa ushahidi wa picha kuonekana wakimuandikisha makaratasi ambayo baadae imeripotiwa na vyombo vya Habari kwamba alikuwa akisaini mkataba wa kuichezea timu hiyo ya Young Africans.

Kwamba katika picha hiyo ameonekana mjumbe wa Young aliyejiuzuru bwana Seif Ahmed na hilo lilitoa shaka kama utaratibu huo umefanywa na klabu ya Young, lakini shaka hiyo imeondolewa pale ambapo tovuti ya Young imetangaza kumsajili mchezaji huyo wa Simba SC, lakini zaidi ya hilo picha inaonyesha fedha zikiwa zimewekwa mbele ya mchezaji jambo linaloonyesha mazingira ya kurubuniwa kwani kwa utaratibu wa kifedha, pesa nyingi kiasi hicho malipo yake yanashauriwa/yanapashwa kupitia benki.

Mbali ya hayo picha hiyo inamuonyesha Kelvin akiwa katika jezi ya mazoezi ya timu ya Taifa na yenye logo ya Kilimanjaro na kumbukumbu zinaonyesha mkataba kati ya TBL na TFF tarehe 9/5/2012, kwa haraka haraka tukio hilo limefanyika katika kipindi chini ya mwezi mmoja ingawa taarifa za ushahidi zinaonyesha tukio hilo limetokea jana tarehe 6/6/2012.
Simba Sports Club ilipenda kuamini kwamba tukio hilo haliihusu klabu ya Young kwani bwana Seif Ahmed alishajiuzuru kutoka kwenye kamati ya Young Africans, kwani Young ni klabu kongwe na inayojua taratibu zote za usajili.
Kwamba Simba Sports Club imeshawasiliana na jopo lake la mawakili na inajiandaa kuishtaki klabu ya Young katika chombo husika cha mpira na kudai adhabu ya kutopitisha majina yote ya usajili ya Young kwa mwaka 2012/2013 na miaka mingine miwili ijayo na Simba SC ipo tiyari kufuatilia suala hili hadi katika mahakama ya mpira ya FIFA.
Kelvin Yondani ni mchezaji halali wa Simba Sc aliye na mkataba hadi 31 mei 2014 mkataba ulioongezwa tarehe 23/12/2011 kuundeleza mkataba wa awali uliokuwa unaisha tarehe 31/5/2012. Sheria za FIFA za hadhi na uhamisho wa wachezaji ziko wazi  katika kipengele cha 5 kifungu kidogo cha 2 kinasema kwamba mchezaji atasajiliwa kuichezea timu moja tu kwa wakati mmoja.

Imetolewa leo tarehe 7/6/2012.

MH. ISMAIL ADEN RAGE (MB)
MWENYEKITI
SIMBA SPORTS CLUB

TAARIFA KUTOKA TFF!

WAZIMBABWE KUCHEZESHA TAIFA STARS, GAMBIA
Waamuzi kutoka Zimbabwe ndiyo watakaochezesha mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia hatua ya makundi Kanda ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Gambia itakayochezwa Juni 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) mwamuzi wa kati atakuwa Ruzive Ruzive. Waamuzi wasaidizi ni Salani Ncube na Edgar Rumeck wakati mwamuzi wa akiba ni Norman Matemera.

Kamishna wa mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni ni Fanie Wallace Mabuza kutoka Swaziland wakati mtathmini wa waamuzi (referee assessor) ni Ali Baligeya Waiswa.

Waamuzi hao watawasili nchini kesho (Juni 8 mwaka huu) saa 1.20 usiku kwa ndege ya Kenya Airways wakati Kamishna wa mechi hiyo atawasili siku hiyo hiyo saa 12.50 jioni kwa ndege ya South African Airways. Mtathmini wa waamuzi atatua pia Juni 8 mwaka huu saa 7.55 mchana kwa ndege ya Kenya Airways.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inaendelea na mazoezi leo saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam chini ya Kocha Mkuu Kim Poulsen.

GAMBIA KUWASILI LEO USIKU
Timu ya Taifa ya Gambia (The Scorpions) ambayo awali ilikuwa iwasili nchini leo (Juni 7 mwaka huu) saa 1.40 asubuhi sasa itawasili leo saa 9.20 usiku kwa ndege ya Kenya Airways tayari kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars.

The Scorpions ilipaswa kubadili ndege Dakar, Senegal jana usiku lakini kukawa na ucheleweshaji (delay), hivyo ikashindwa kuwahi Nairobi, Kenya ambapo ingeunganisha kwa ndege ya alfajiri kuja Dar es Salaam.

Kikosi cha timu hiyo chenye wachezaji 22 wakiwemo tisa wanaocheza mpira wa kulipwa nje ya nchi hiyo kitafikia kwenye hoteli Sapphire iliyopo Mtaa wa Lindi na Sikukuu eneo la Kariakoo.

Wachezaji walioko katika msafara huo ni Musa Camara, Abdou Jammeh, Momodou Futty Danso, Lamin Basmen Samateh, Ousman Koli, Pa Saikou Kujabi, Mustapha Kebba Jarju, Yankuba Mal Ceesay na Demba Savage.

Wengine ni Saihou Gassama, Alieu Darboe, Momodou Ceesay, Pa Modou Jagne, Tijan Jaiteh, Bubacarr Sanyang, Christopher Allen, Musa Yaffa, Sulayman Marr, Mamut Saine, Hamsa Barry, Ali Sowe, Omar Colley na Saloum Faal.

PROGRAMU YA MAZOEZI YA GAMBIA

IJUMAA JUNI 8
01.00 asubuhi Mazoezi- Uwanja wa Karume
10.00 jioni   Mazoezi- Uwanja wa Taifa

JUMAMOSI JUNI 9
04.00 asubuhi  Mkutano na Waandishi wa Habari- Ukumbi wa TFF
10.00 jioni  Mazoezi- Uwanja wa Taifa

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

NINGEKUA YONDANI PIA NINGECHUKUA MZIGO !



Well done Kevin Yondani...hata mimi ningefanya hivyo hivyo...unachukua huku m20 kule m30....watapiga kelele weweeeee lakini mwishowe watapatana. watu wenyewe hawako serious tumewazoea. ingekuwa umesaini katika makampuni mawili serious kama Barrick na Vodacom labda...lakini hizi timu za Kariakoo...wala usihofu. wataelewana tu....hakuna jela hapo. kwanza ebu ona noti zenyewe zinatolewa kwa cash badala ya hundi au transactions zinazoeleweka!!! we live just once....

Yanga kiboko
hii jezi ya Kilimanjaro Lager na taifa Stars imetoka May this year, kwa hiyo ule mkataba wa miaka 17 na majina ya kinyumenyume ni zuga tuu.... Mohamed Shaban tuletee picha kama hii ili tujue kuwa mmemsajili kweli vinginevyo imekula kwenu.... Manji kaanza kazi Jangwani

Nina urafiki na wachezaji wengi wa yanga. Siba,azam na klabu nyingne za bongo hata wachezaji wa ndondo,kitu ambacho huwa nasema siku zote ni kwamba wachezaji wa kitanzania wana matatizo makubwa,of course its like the whole soccer family in bongo is fucked up,Yondani amesaini Yanga wakati akiwa na mkataba na Simba ambako alishasaini tunaambiwa sijui 6 months ago,in my opinion a contract has to be r...espected,sheria za mkataba kimataifa ziko hivi,mkataba ukibaki muda mfupi kuisha lazima mazungumzo yafanyike either kurenew au kuuzwa kwa timu nyingine,in between mchezaji hatakiwi hata kuzungumza na timu nyingine bila ridhaa ya timu ambayo tayari ana mkataba nayo ambayo kwa hali ya kawaida lazima itoe ruhusa mazungmzo yaendelee,in this saga Kelvin Yondani is in hot water for signng for two clubs kama ninachokisikia ni sahihi,pia viongozi wa yanga wana kosa kubwa ambalo ni kufanya mazungumzo kinyume cha taratibu na mtu ambaye tayari ana mkataba,viongozi wa simba kwa upande wao wana kosa la kutengeneza situation ya kumfreeze out yondani kwenye timu hali iliomfrustarte na kumfanya asaini timu nyingine,WHY ALWAYS TANZANIA vitu vya kipuuzi kama hivi vinatokea.


kwa uelewa wangu mdogo na hela hizo ni mil. 18



Pesa ya Manji hiyooooooooo
Kweli Manji agombee Yanga..Na Pesa yote hiyo aliyonayo?
Anatafuta nini? Kuna kitu......Ukiona mtu mzima kayavulia nguo ujue kuna jambo....kazi kwenu yanga.......

YANGA YAANZA MAZUNGUMZO NA MAXIMO

Taarifa zisizo rasmi nilizozipata hivi punde klabu ya Yanga ipo kwenye mazungumzo na aliyekua kocha wa Taifa Stars Mbrazil Marcio Maximo.
Kama mazungumzo hayo yatafanikiwa basi Maximo atarejea kwa mara nyingine tena hapa nchini kuja kuifundisha Yanga.

UFARANSA: HAIJASHINDA MECHI YOYOTE KWENYE EURO WALA WORLD CUP TANGU 2006: ITAFANYA NINI KWENYE EURO 2012.

Laurent Blanc anaichukua Ufaransa kwenda nayo kwenye Euro 2012 huku akiiongoza timu hiyo kutofungwa katika michezo 20, ambayo inahusisha ushindi dhidi ya Ujerumani, England na Brazil. Lakini kocha huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa bado haipi nafasi kubwa timu. Ufaransa haijashinda mechi yoyote ya mwisho ya michuano mikubwa yenyewe tangu mechi ya nusu fainali ya World Cup 2006 (haikushinda mechi yoyote kwenye Euro 2008 na WOZA 2010), huku wakishika nafasi ya 16, nafasi tisa nyuma ya wapinzani wao England wanaoshika nafasi ya saba kwenye ubora wa viwango wa FIFA.

Blanc bado na maumivu ya kichwa kuhusu upangaji wa kikosi hasa kwenye nafasi ya beki wa kushoto, ambapo Gael Clichy ameonyesha kiwango kizuri kwenye mchi dhidi ya Serbia siku chache baada ya Evra kucheza chini kiwango dhidi ya Iceland. Kiungo mkabaji Yann M'Vila pia ana majeruhi ya enka ambayo yatamfanya asicheze mchezo wa kwanza na Alou Diarra anategemewa kumbadili.

Lakini hiki ni kikosi tofauti sana na kile kilichoenda kwenye kombe la dunia 2010 chini Raymond Domenech nchini South Africa. Golikipa Hugo Lloris sasa ni nahodha, lakini Phillipe Mexes, M'Vila na Karim Benzema ambaye yupo kwenye form sasa hivi, wote waliikosa michuano ya WOZA 2010 hivyo hawakuwemo kwenye aibu iliyopita. Lakini hili haliwezi kusemwa linapojitokeza jina la Frank Ribery, ambaye kwa sasa yupo desparate kuweza kurudisa imani na upendo wa wafaransa. Baada ya miaka 3 bila kufunga bao, Ribery alifunga mara mbili katika mechi 2 za kirafiki zilizopita. Ikiwa ataanza japo kuileta nusu ya uwezo anaonyesha Bayern Munich akiwa kwenye jezi za Blue, then Les Bleus wanaweza kuwashangaza wengi.

WACHEZAJI MUHIMU

Karim Benzema
Tumaini kubwa la soka la Ufaransa lilikuwa na mwanzo mmbaya kwenye career yake ndani ya timu ya taifa ya Ufaransa kwenye michuano ya Euro 2008, pale alipotuhumiwa kwa pamaja na Samir Nasri kwa kutokuwa na heshima kwa wachezaji wakubwa na kwa kutompasia mipra mingi Thierry Henry. Akaachwa kwenye kombe la dunia 2010, lakini amekuwa ndio mfungaji bora wa Ufaransa chini ya Blanc, akifunga mabao matano katika mechi 17, likiwemo goli la ushindi dhidi ya Brazil. Huku akiwa amemaliza msimu wa mafanikio na Real Madrid akifunga mabao 32, huku akitamba kwamba amekuwa mchezaji mzuri zaidichini Jose Mourinho. Na kama hayo maneno yataonekana kwenye vitendo basii Ufaransa itaifadika sana.


Samir Nasri
Mpaka aliposhinda kombe la premier league na Manchester City mwezi uliopita, Nasri alikuwa ameshinda kombe moja tu kwenye maisha yake ya soka la kulipwa: alipofunga goli la ushindi kwenye fainali ya Euro 2004 kwa timu ya vijana wa miaka 17. Nasri ni moja ya sehemu ya kundi 'Kizai cha 87' kinachowahusisha wachezaji waliozaliwa mwaka 1987 na kwa sasa wakiwa ndio wanaelekea kwenye vilele vya viwango vyao wakiwa kwenye timu ya taifa ya wakubwa. Kundi hilo lilikuwa linawahusisha Benzema, Hatem Ben Arfa, Jelemu Menez na Blaise Matuidi - wote walicheza kwenye Euro 2004, na sasa wapo kwenye Euro 2012 ya wakubwa. Kama kiungo mchezeshaji Nasri anayo nafasi ya kuifanya timu ikacheza soka zuri la kushambulia na ahatimaye kuiletea timu ushindi. Ni jukumu ambalo amekuwa alilitumikia siku nyingi, sasa hivi anayo nafasi ya kuonyesha kama kweli anastahili.

Yann M'Vila
Kiungo mkabaji anatarajiwa kuuzwa kwa mapesa mengi mara baada ya michuano hii, na klabu yake. Rennes, inaweza ikataka kuongeza beikama atacheza vizuri kwenye Euro.M'Vila alikuwa na bahati kuikosa world cup, alitoswa na Domenech lakinii chini ya Blanc amejihakikishia nafasi ya kudumu. Akiwa na miaka 21, amekuja kuwa mchezaji muhimu wa Ufaransana kwa jinsi inavyocheza, kuvunja mashambulizi ya wapinzani na kushambulia kutokea kwenye kiungo huku akiwa na uwezo mkubwa wa kupiga pasi. Ameshajulikana kwamba ataikosa mechi yake ya kwanza ya Euro dhidi ya England na anategemewa kurudi dimbani kwenye mechi ya Ukraine.

EXCLUSIVE: SIMBA YAKAMILISHA USAJILI WA SALUM KINJE WA AFC LEOPARDS


Salum Kinje
Taarifa rasmi za uhakika kutoka ndani ya uongozi na kamati ya ufundi ya klabu ya Simba ni kwamba timu hiyo imefanikiwa kukamilisha usajili wa mchezaji bora wa nafasi ya kiungo kwenye ligi kuu ya soka nchini Kenya, Salum Kinje ambaye anaichezea AFC Leopards.
Nikiwa na Salum Kinje nilipotembelea Kenya mwezi uliopita.
Kinje ambaye ni mtanzania amesajiliwa na Simba kwa kiasi cha fedha ambacho hakijawekwa wazi na pande zote mbili, lakini amesaini mkataba wa kuitumikia Simba kwa miaka 2 na siku chache zijazo ataanza mazoezi na timu yake mpya inayojiandaa kushiriki michuano ya Kagame Cup inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Wednesday, June 6, 2012

SAKATA LA KELVIN YONDANI: YANGA YATOA USHAHIDI WA PICHA

Mchezaji Kelvin Yondani akisaini mkataba wa usajili mbele ya kiongozi wa Yanga Seif Ahmed usiku huu, katika picha hii Yondani anaonekana akiwa amevaa fulana na timu ya taifa ambazo zimeanza kutumika mwezi mmoja uliopita baada ya stars kuingia mkataba na TBL KUPITIAKilimanjaro.
Taarifa nilizozipata hivi punde Yondani amefuatwa kwenye kambi ya timu ya Taifa iliyopo kwenye Hotel ya Tansoma jijini Dar Es Salaam.

KWANINI MANJI ANAUTAKA UONGOZI WA YANGA?

*NI KWELI ANATAKA KUIMILIKI YANGA?

*NA KAMA AKIFANIKIWA KUWA MMILIKI ATAIFANYIA NINI YANGA?

*KWANINI BAADHI YA WANACHAMA HAWAMTAKI?


Kwa kipindi kirefu sasa tangu mfanyabiashara maarufu Bwana Manji ajiingize katika kuifadhili klabu ya Dar Young Africans kumekuwepo na mgawanyiko mkubwa wa kifikra miongoni mwa wanamichezo, wanachama na wapenzi wa Yanga, juu ya madhumuni hasa kabisa ya mfanyabiashara huyo kuisadia Yanga.

Huku baadhi ya watu wakisema Manji ana nia ya dhati kabisa ya kuisadia Yanga na kuifanya kuwa klabu ya kisasa kabisa,huku wengine wakibaki kusema kwamba mmiliki huyo wa Quality Group of Companies anataka kuitumia Yanga kibiashara na kujinufaisha binafsi kwa kutumia brand ya Yanga.

Katika kipindi cha awamu mbili za uongozi tofauti pale Yanga, kuanzia kwa Wakili Iman Madega mpaka uongozi huu uliopinduliwa wa mwanasheria Lloyd Nchunga, Yusuph Manji amekuwa akitajwa kuhusika na migogoro mikubwa iliyojitokeza ndani ya klabu hiyo.

Hivi karibuni baada ya baadhi ya wanachama wa klabu ya Yanga hasa wakiongozwa na wazee wa klabu hiyo, waliongoza mapinduzi ya kuuondoa uongozi halali wa bwana Lloyd Nchunga, ambaye mara ya kwanza  alijaribu kutuna lakini mwishowe akaachia ngazi mwenyewe baada ya kuandamwa sana kiasi cha kuanza kupokea vitisho na kufanyiwa vurugu. Wazee wakachukua timu huku wakitamba wana zaidi ya millioni 750 za kufanya usajili, lakini TFF ikairudisha timu chini ya uongozi wa katibu mkuu Celestine Mwesiga huku wakiagiza ufanyike uchaguzi kama katiba ya klabu inavyosema.

Uchaguzi ukaitishwa kwa mujibu wa kanuni, na kamati ya uchaguzi ikaanza kutoa fomu za nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Yanga.


Katika hali ya kushtusha siku ya jumatatu mfanyabiashara na mdhamini wa klabu hiyo, Manji akachukua fomu ya kugombea uenyekiti wa klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya jangwani,huku akimchukulia mmoja wa wajumbe wa kamati ya usajili Abdallah Ahmed Bin Kleb fomu ya kugombea ujumbe wa kamati ya utendaji, na hatimaye leo Manji alikuwa mmoja ya wanachama 29 wa Yanga waliorudisha fomu za kugombea nafasi za uongozi mbalimbali ndani ya Yanga.

Kitendo cha Manji kuutaka ubosi wa klabu ya Yanga umeibua hofu na maswali mengi juu ya nia hasa ya mfanyabiashara huyo dhidi ya Yanga, baadhi ya wanachama wa klabu hiyo ambao siku zote wamekuwa wakimpinga Manji kwa namna moja au nyingine wakidai hana nia nzuri ya klabu yao, wameongea exclusively na shaffihdauda.com na kutoa hoja nyingi sana zinazojaribu kuelezea kwanini hawana imani na mpango wa Manji kuwa mwenyekiti wa klabu yao.

1:MANJI VS IMANI MADEGA NA LLOYD NCHUNGA

Wakati wakili Iman Madega anataka kuingia Yanga alikuwa akipigwa tafu kubwa sana na bwana Manji mpaka akafanikiwa kuutwa uongozi wa klabu hiyo. Lakini baada ya muda kupita kukatokea kutokuelewana baina ya watu hao wawili. Hii ilikuwa ni baada ya Manji kuleta wazo la kutaka Yanga iendeshwe na kampuni. Kwa maana ingeanzishwa kampuni ambayo ingenunua asilimia 51 za Yanga, na asilimia 49 zinazobakia zingekuwa zinamilikiwa na wanachama ambao wangekopeshwa kiasi cha billioni 3 na Manji kwa mkopo wa mwaka mmoja tu, huku akiwawekea sharti kwamba kama wangeshinda kuzilipa billioni 3 zake alizowakopesha ndani ya kipindi walichokubaliana kulipwa na mkopo huo , basi Manji ndio angekuwa mtu wa kwanza kuuziwa hisa zile zile ambazo walishindwa kuzilipia.
Pia katika zile hisa asilimia 51, hakukuwa na sheria zozote za kumkataza mtu yoyote kununua hisa hizo, uwe mwanachama au la ungeweza kununua hisa, hata Manji mwenyewe kama angejisikia kufanya hivyo pia alikuwa na uhuru wa kununua.
Baada ya kuupitia vizuri mpango huo Iman Madega hakuweza kukubaliana na mpango huo kwa hofu, kwamba ule ni mpango ambayo ungeidhuru Yanga.

Baada ya kumshindwa Madega ambaye alifanikiwa kumaliza kipindi chake cha Uongozi, klabu hiyo ikafanya uchaguzi na kupata uongozi mpya chini ya Lloyd Nchunga ambaye naye alipoletewa mpango wa kuanzishwa kwa kampuni na Manji akakataa na matokeo yake timu ikahujumiwa kitu kilichopelekea migomo ya wachezaji, na hivyo timu kufanya vibaya kwenye ligi. Inasemekana baada ya Nchunga kuvimba na kukataa kujiuzulu baada ya kipigo cha 5-0 kutoka watani wao Simba, ndipo bosi Manji alipoanza kutoa mkwanja kwa baadhi ya viongozi na kuwaambia wajiuzulu huku akiwatumia wazee kumtia mshikemshike Nchunga ambaye mwishowe akaamua kujiuzulu na kupelekea kuitishwa kwa uchaguzi mpya.


 KIVIPI?

Kiuhalisia tu shilingi billioni 3 ni fedha nyingi sana kwa wanachama wa kawaida wa Yanga ambao ndio wapo wengi kuweza kumudu kuzilipa ndani ya kipindi mwaka mmoja. Hata kama wangemudu kuzilipa basi isingekuwa rahisi unless kuwe kuna mkono wa mtu nyuma yao, na kama wangeumudu kwa uwezo wao basi ni wachache sana wangeweza kufanya hivyo, hivyo mwisho wa siku hisa nyingi sana zingerudi mikononi mwa Manji.
Huku pia kwenye asilimia 51 za kampuni  Manji alikuwa na uhuru wa kununua hisa, hivyo kama Manji akazipata labda asilimia 40 ya hisa alizowalipia wanachama kwa mkopo na wakashindwa kuzilipa na huku kwenye kampuni akanunua japo asilimia 15 tu, kwa maana hiyo angekuwa ndio majority shareholder hivyo kumfanya kuwa mmiliki wa Yanga SC.

2: KWANINI HAWATAKI MANJI AIMILIKI YANGA?
Anti-Manji wanasema hawana imani kabisa na Manji kwamba anaitaka Yanga ili kuisadia iwe klabu na yenye mafanikio, bali ni kwa maslahi yake binafsi.
Kwanza wanajenga hoja kwamba Manji hakuingia Yanga kwa mapenzi binafsi bali  alisukumwa na sababu za kisiasa kwa kuifanya klabu hiyo inayosadikika kuwa na wapenzi wengi zaidi nchini kuwa kichaka cha kujifunikia madhambi yake baada ya kukumbwa na kashfa ya EPA.
Wanasema Manji tofauti na wadhamini wengine waliowahi kuidhamini na kuisadia Yanga kama akina Gulamali na Mohamed Vilani, ambao walikuwa wakitoa fedha nyingi kuisadia timu yao bila kuidai chochote, lakini Yusuf Manji siku zote amekuwa akiwasainisha kwenye vitabu vya kumbukumbu viongozi kwa niaba ya Yanga kila anapotoa fedha labda ya usajili au kuisadia pale timu inapokwama kiuchumi, na hilo limeshathibitishwa na Manji mwenyewe pale alipokaririwa mara kadhaa akisema anaidai Yanga fedha nyingi bila kuweka wazi ni kiasi gani. Kwa hiyo hawajui ni lini atawadai fedha anazoidai klabu hiyo na kama watashindwa kulipa je atafanya nini?

Anti-Manji wanaendelea kujenga hoja zao kwa kusema kuwa wanahisi kwamba Manji ambaye pia ni mfanyabiashara ambaye anamiliki majengo mengi ya kibiashara hapa nchini anachokihitaji kutoka Yanga kwanza ni kujilipa fedha zote alizotumia kuisaidia klabu hiyo pamoja na zile ambazo zipo nje ya vitabu alizotumia kupata wafuasi waliochini ya himaya yake ndani ya klabu hiyo.

Wanasema wasiwasi wao ni kwamba ikiwa Manji atakuwa mmiliki wa Yanga, ataitumia brand ya klabu hiyo pamoja na assets zake ili kujilimbikizia fedha nyingi kwa kipindi labda cha miaka 3 mpaka mitano na baadae ataliuza tu jina la Yanga ikiwemo timu, na yeye kubaki na assets za Yanga yakiwemo majengo mawili ambayo yote yapo kwenye eneo la kibiashara la kariakoo pamoja na eneo kubwa wanalolimiliki Yanga la Jangwani makao makuu ambapo imegundulika Yanga inahodhi eneo kubwa sana ambalo kwa sasa limevamiwa na baadhi ya majirani wanaoishi karibu na makao makuu ya Yanga-Jangwani.

Endapo Manji ataliuza jina la Yanga na kubaki na assets za klabu hiyo kisha kuzitumia kwa matumizi mengine, klabu hiyo itapoteza sehemu ya historia yake kubwa iliyojijengea.


3: ANTI-MANJI WALIVYOPOKEA TAARIFA ZA MANJI KURUDISHA FOMU BILA TEGEMEO LAO IDD KIPINGU KUSHINDWA KUCHUKUA FOMU.

Baada ya Manji kuchukua fomu za kugombea uenyekiti wa Yanga, kundi la wanachama wanaompinga Manji kwa sababu zao waliamua kutafuta njia za kuweza kupambana nae. Inasemekana wakajaribu kumtumia mtoto wa kigogo wa nchi ambaye nae ana nguvu na ufuasi mkubwa ndani ya klabu hiyo,  ili aweze kumshawishi Kanali Iddi Kipingu agombee nafasi hiyo, lakini baada ya Kipingu kushindwa kuhakikishiwa kupewa sapoti ya asilimia 100 ya kuweza kupambana na tajiri Manji akaona bora asijiingize kwenye vita mabayo itaweza kumshushia heshima yake kubwa aliyojijengea kwenye tasnia ya michezo nchini kwa kuangushwa vibaya na Sheikh Mansour wa Tanzania.

NB: HUU SIO MTAZAMO WANGU BALI NI MTAZAMO WA WANACHAMA WA YANGA WANAOMPINGA MANJI. NIMEWASILISHA. BY SHAFFIH DAUDA.

YANGA YATANGAZA KUMSAJILI KEVIN YONDAN HUKU SIMBA IKIMUONGEZEA MKATABA KELVIN YONDANI.

Leo hii klabu ya Yanga imetangaza kumsajili kinda raia wa Tanzania Kevin Patrick Yondan mwenye umri wa miaka 17,Yondan ambaye anacheza nafasi ya beki wa kati hajajulikana ametokea Klabu gani alizaliwa 9/10/1994.Mkataba wa Yanga na kinda huyo ni wa miaka miwili na unataraji kumalizika msimu wa 2013/2014.


hapa chini ni sehemu ya mkataba wa beki huyo na klabu ya Yanga yenye maskani yake mitaa ya Twiga na Jangwani.

Wakati huo huo Simba Sc imetangaza kumuongezea mkataba wa miaka miwili beki wake wa kati Kelvin Patrick Yondani, mkataba huo mpya ulisainiwa tangia mnamo 23/12/2011 ikiwa ni maboresho ya mkataba wa awali uliokua unafika kikomo mwishoni mwa mwezi uliopita yaani 31/05/2012. Yondani mwenye umri wa miaka 27 pia ni beki wa kimataifa wa Tanzania.


Kelvin Patrick Yondani

First name:Kelvin Patrick
Last name:Yondani
Nationality:Tanzania
Date of birth:10 October 1984
Age:27
Place of birth:

 Baadhi ya michezo ambayo Kelvin Patrick Yondani ameichezea timu ya Taifa ya Tanzania.

TareheNyumbanimatokeo Ugenini
2012-06-02Côte d'Ivoire
2 - 0
Tanzania
2012-05-26Tanzania
0 - 0
Malawi
2012-02-23Tanzania
0 - 0
Congo DR
2011-11-15Tanzania
0 - 1
Chad
2011-11-11Chad
1 - 2
Tanzania
2010-06-07Tanzania
1 - 5
Brazil
2010-01-04Tanzania
0 - 1
Côte d'Ivoire

BIN KLEB ARUDISHA FOMU YAKE NA MANJI JANGWANI


ABDALLAH Ahmad Bin Kleb amerudisha fomu yake ya kugombea Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, lakini inadaiwa alikuwa ana fomu nyingine tatu, ambazo inadaiwa kuwa ni za Yussuf Manji kugombea Uenyekiti, Isaac Chanji, Makamu Mwenyekiti, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakhim Masu. Pichani Bin Kleb akikabidhi fomu hizo.




Anaondoka

Source: Binzubeiry

TANZANIA YAPANDA VIWANGO VYA FIFA


KIINGILIO MECHI YA TAIFA STARS, GAMBIA 3,000/-
Kiingilio cha chini ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Gambia (The Scorpions) itakayochezwa Jumapili (Juni 10 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 3,000.

Watazamaji watakaolipa kiingilio hicho ni watakaokaa kwenye viti vya rangi ya bluu na kijani ambavyo ni 36,693 kati ya jumla ya viti 57,558 vilivyopo katika uwanja huo wa kisasa. Kiingilio kwa viti vya rangi ya chungwa ni sh. 5,000.

Kwa upande wa VIP C watalipa sh. 10,000 wakati VIP B ni sh. 20,000. Kiingilio kwa jukwaa la VIP A ambalo linachukua watazamaji 748 tu ni sh. 30,000 kwa mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni.

Tiketi zitaanza kuuzwa Jumamosi (Juni 9 mwaka huu) kuanzia saa 2 asubuhi kwenye vituo vya Mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Ohio na Samora, Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Soko Kuu la Kariakoo na Uwanja wa Taifa. Siku ya mechi pia mauzo yatafanyika katika vituo hivyo na baadaye kuhamia Uwanja wa Taifa.

GAMBIA YATARAJIA KUINGIA LEO DAR ES SALAAM
Timu ya Taifa ya Gambia (The Scorpions) inatarajia kuwasili nchini wakati wowote kuanzia leo (Juni 6 mwaka huu) tayari kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars.

Kamati ya Maridhiano inayoendesha Chama cha Soka Gambia (GFA) hadi leo mchana ilikuwa haijatuma taarifa rasmi kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) juu ya ujio wake.

Lakini vyombo vya habari vya Gambia vimeripoti kuwa timu hiyo ikiwa na wachezaji 23 na viongozi tisa ilitarajiwa kuondoka huko leo kuja Dar es Salaam tayari kwa ajili ya mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu na washabiki wengi nchini.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa GFA aliyekaririwa na vyombo vya habari vya nchi hiyo, Bakary Balder, msafara wa timu hiyo utaongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Vijana na Michezo, Malang Jassey. .

Mbali ya Jassey, viongozi wengine katika msafara huo ni Ofisa Utawala wa timu Modou Sowe, Kocha Luciano Machini, makocha wasaidizi Peter Bonu Johnson na Lamin Sambou, Kocha wa makipa Alhagie Marong, mtaalamu wa tiba mbadala (physiotherapist) Pa Matarr Ndow, Mtunza vifaa Sanna Bojang na Daktari wa timu Kalifa Manneh.

Wachezaji ni Musa Camara, Abdou Jammeh, Momodou Futty Danso, Lamin Basmen Samateh, Ousman Koli, Pa Saikou Kujabi, Mustapha Kebba Jarju, Yankuba Mal Ceesay, Demba Savage, Saihou Gassama, Alieu Darboe, Momodou Ceesay, Pa Modou Jagne, Tijan Jaiteh, Bubacarr Sanyang, Christopher Allen, Musa Yaffa, Sulayman Marr, Mamut Saine, Hamsa Barry, Ali Sowe, Omar Colley na Saloum Faal.

TANZANIA YAPANDA VIWANGO VYA FIFA
Tanzania imepanda kwa nafasi sita kwenye orodha ya viwango ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) iliyotolewa leo (Juni 6 mwaka huu) na shirikisho hilo.

Kwa viwango vya Mei mwaka huu, Tanzania ambayo timu yake ya Taifa (Taifa Stars) inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ilikuwa namba 145 hivi sasa imefika nafasi ya 139 ikiwa na pointi 214.

Mei 26 mwaka huu Taifa Stars ilicheza mechi ya kirafiki na Malawi na kutoka suluhu. Malawi yenye pointi 324 imeporomoka kwa nafasi tano kutoka ya 102 hadi 107.

Ivory Coast ambayo katika mechi yake ya mwisho Juni 2 mwaka huu iliifunga Taifa Stars mabao 2-0 imeporomoka kwa nafasi moja kutoka ya 15 hadi 16 ikiwa na pointi 943. Hata hivyo ndiyo inayoongoza kwa upande wan chi za Afrika katika viwango hivyo.

PROGRAMU YA TAIFA STARS KWA MECHI YA GAMBIA

JUMATANO JUNI 6
01.00 asubuhi  Mazoezi- Uwanja wa Karume
10.00 jioni       Mazoezi- Uwanja wa Taifa

ALHAMISI JUNI 7
10.00 jioni   Mazoezi- Uwanja wa Taifa

IJUMAA JUNI 8
10.00 jioni   Mazoezi- Uwanja wa Taifa

JUMAMOSI JUNI 9
04.00 asubuhi  Mkutano na Waandishi wa Habari- Ukumbi wa TFF
11.00 jioni  Mazoezi- Uwanja wa Taifa

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)