Search This Blog

Thursday, June 7, 2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

   SIMBA SPORTS CLUB           
P.O.BOX 15318 | TEL+255 222183330 |FAX +255 222183330 |MSIMBAZI/MCHIKICHI STREET | DAR ES SALAAM | TANZANIA | EMAIL   simbasportsclub@yahoo.com|WEBSITE www.simba.co.tz| AFFILIATED TO TFF, DRFA and IDFA

                                
Simba Sports club imesikitishwa na kitendo cha Young Africans kuvunja taratibu za usajili kwa kumrubuni mchezaji wake Kelvin Patrick Yondani  kwa kuzungumza naye na baadae kwa ushahidi wa picha kuonekana wakimuandikisha makaratasi ambayo baadae imeripotiwa na vyombo vya Habari kwamba alikuwa akisaini mkataba wa kuichezea timu hiyo ya Young Africans.

Kwamba katika picha hiyo ameonekana mjumbe wa Young aliyejiuzuru bwana Seif Ahmed na hilo lilitoa shaka kama utaratibu huo umefanywa na klabu ya Young, lakini shaka hiyo imeondolewa pale ambapo tovuti ya Young imetangaza kumsajili mchezaji huyo wa Simba SC, lakini zaidi ya hilo picha inaonyesha fedha zikiwa zimewekwa mbele ya mchezaji jambo linaloonyesha mazingira ya kurubuniwa kwani kwa utaratibu wa kifedha, pesa nyingi kiasi hicho malipo yake yanashauriwa/yanapashwa kupitia benki.

Mbali ya hayo picha hiyo inamuonyesha Kelvin akiwa katika jezi ya mazoezi ya timu ya Taifa na yenye logo ya Kilimanjaro na kumbukumbu zinaonyesha mkataba kati ya TBL na TFF tarehe 9/5/2012, kwa haraka haraka tukio hilo limefanyika katika kipindi chini ya mwezi mmoja ingawa taarifa za ushahidi zinaonyesha tukio hilo limetokea jana tarehe 6/6/2012.
Simba Sports Club ilipenda kuamini kwamba tukio hilo haliihusu klabu ya Young kwani bwana Seif Ahmed alishajiuzuru kutoka kwenye kamati ya Young Africans, kwani Young ni klabu kongwe na inayojua taratibu zote za usajili.
Kwamba Simba Sports Club imeshawasiliana na jopo lake la mawakili na inajiandaa kuishtaki klabu ya Young katika chombo husika cha mpira na kudai adhabu ya kutopitisha majina yote ya usajili ya Young kwa mwaka 2012/2013 na miaka mingine miwili ijayo na Simba SC ipo tiyari kufuatilia suala hili hadi katika mahakama ya mpira ya FIFA.
Kelvin Yondani ni mchezaji halali wa Simba Sc aliye na mkataba hadi 31 mei 2014 mkataba ulioongezwa tarehe 23/12/2011 kuundeleza mkataba wa awali uliokuwa unaisha tarehe 31/5/2012. Sheria za FIFA za hadhi na uhamisho wa wachezaji ziko wazi  katika kipengele cha 5 kifungu kidogo cha 2 kinasema kwamba mchezaji atasajiliwa kuichezea timu moja tu kwa wakati mmoja.

Imetolewa leo tarehe 7/6/2012.

MH. ISMAIL ADEN RAGE (MB)
MWENYEKITI
SIMBA SPORTS CLUB

9 comments:

  1. kama simba wanategemea maelezo haya kumrudisha yondani kundini nina mashaka km watafanikiwa.kuna kujikanganya kwingi kwenye maelezo yenyewe.mfano anasema mkataba hauna uhalali kwa sababu huyo mjumbe wa yanga alishajiuzuru,kwa maana hamna mkataba unaoihusisha yanga hapo, wakati hohuo anadai ataishtaki yanga hata ikibidi kwa fifa! jamani,ni kwa lipi sasa wakati awali ulisema yanga haihusiki!simba jipangeni upya km mna nia ya kumrejesha jamaa kundini

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ataishtaki yanga coz wametangaza rasmi kumsajili yondani. Hakuna kujikanyaga hapo, soma vizuri

      Delete
  2. Safi sana mana ni kama yanga inaongozwa na wahuni tu(canavaro vs coastal)!zile goli tano zinawauma sana mpk wanashindwa kufata taratibu.ila nawashauri simba kuachana na yondani ingawa haina beki kwa sasa mana amekosa MSIMAMO!..

    ReplyDelete
  3. rage acha kuharisha unatoa habari za kitoto namna hiyo na wasiwasi na taaluma yako,

    ReplyDelete
    Replies
    1. shaffi mbona ushabiki unakuharibia umaarufu wako kaka!Yaani unaona sera mbovu unazozidai ndo chanzo cha mchezaji kusaini club nyingine ilhali mkataba wake haumuruhusu kufanya hivyo? au kile kipande cha mkataba kati ya simba na yondani kilichozungushiwa mstari hujakielewa kama yondani?Kwa hilo wenzako yanga na yondani wameenda chaka tena sana,maana walimsainishaje yondani bila kuwa na uhakika kumaliza mkataba na timu yake?
      Suala la simba kuwaacha wachezaji nijukumu la club wala wewe hilo halikuusu,maana haijalishi ya kwamba timu imebeba ubingwa mchezaji anayepwaya asiachwe,sijui umelifikilia kidogo hilo!alafu kaka wewe upo karibu na club hiyo unashindwa nini siku moja kutoa semina kwa timu zetu za bongo ambazo unadhani wanadidimiza soka we kama mdau wa soka au ni maneno tu redioni lakini vitendo hakuna!Tatizo kubwa ni upuuzi wa wachezaji wa bongo wanaotaka pesa na kusaini mikataba pasipo kusoma na kuielewa mikataba hiyo.Kuna haja ya wachezaji kwenda shule kwanza alafu soka au waombe mikataba yao iandikwe kwa kiswahili.

      Delete
  4. Kama Yondani ana mkataba na Simba unaotambulika kisheria kwamba unaisha mwaka 2014 basi imekula kwake,lakini kama ulishaisha na alikuwa huru basi Yanga watamtumia msimu ujao.


    Abraham Jesse
    DUCE

    ReplyDelete
  5. Aminia aden rage

    ReplyDelete
  6. Wapelekeni FIFA hao wahuni wasiojua sheria. Imekula kwao.

    ReplyDelete
  7. hizi timu za simba na yanga ni pasua kichwa.badala ya zenyewe kuwa mfano kwa timu nyingine zinabaki kulumbana kufukuzana vilabuni.timu hizi pamoja na ukongwe wake zimeshindwa kulipeleka soka letu pale tunapopataka.mimi naamini siku moja zikishuka daraja ndio mpira wa tanzania utakua maana huu ubabe wanaotuonyesha kwenye usajili wa wachezaji utaisha.

    NAWASILISHA

    HAMZA SATO

    ReplyDelete