Search This Blog

Thursday, June 7, 2012

SAKATA HILI LA YONDANI KWA UPANDE MWINGINE LIMECHANGIWA NA SERA MBOVU YA USAJILI YA SIMBA!

Sakata la usajili wa Kelvin Yondani limetokea kuteka hisia za wengi katika kipindi cha masaa 48. Taarifa ambazo zimetapakaa kwenye vyombo ya habari zinasema kuwa Dar es salaam Young Africans imekamilisha usajili wa Yondani huku nakala ya mkataba wake alioingia na klabu hiyo ukionyesha kuwa amesaini kuichezea Yanga kwa miaka miwili huku akitia kibindoni kiasi cha Milioni 30 huku mshahara wake ukiwa laki nane kwa mwezi.
Upande wa pili wa sinema hii ambao ni klabu anayodaiwa kutoka Yondani ya Simba Sports unadai kuwa Yondani aliongeza mkataba wake wa awali na klabu hiyo kabla hata ya mwisho wa msimu huu uliopita.
Kikubwa kinachonitatiza ni sera ya usajili ya klabu ya Simba ambayo ndio hasa mjadala mkuu kwenye makala haya.
Tukirudi nyuma msimu uliopita Simba ilitangaza kumuacha beki wake wa kati Meshack Abel . Ukiangalia takwimu za michezo ya Simba kwa kipindi cha miaka miwili iliopita utagundua kuwa moja ya matatizo sugu imekuwa safu ya ulinzi, hata hivyo Meshack Abel ni mmoja ya mabeki wa kati shupavu ambao hata kwenye timu ya taifa wamekuwepo kwa kipindi kirefu. Baada ya kumuacha Abel simba iliwasajili Obadia Mungusa na Victor Costa. Hiki ni kipindi ambacho Kevin Yondani alikuwa froze out of the team (inasemekana alikuwa na beef na mmoja wa viongozi).  Smba pia kwa sababu zisizojulikana iliamua pia kumuacha beki wa pembeni kulia Haruna Shamte wakati ambapo alikuwa anachipukia na tayari alikuwa ameanza kuitwa kwenye timu ya taifa  pamoja na kuwa mdogo kiumri.
Mbdala wa Shamte alikuwa beki wa zamani Nasor Masoud Cholo aliyerudishwa toka JKT Oljoro na Shomari Kapombe ambaye awali alisajiliwa kama kiungo ilia ni uwezo wake au versatility yake ambayo imeshuhudia akirudishwa nyuma kucheza wakati mwingine kama beki wa kati na pembeni.
Tetesi ambazo tunazisikia sasa ni kwamba ,Juma Jabu,Obadia Mungusa na Victor Costa wameachwa huku Juma Nyoso naye akiwa mbioni kuachwa na sababu tunayoambiwa ni kwamba amekuwa akiigharimu timu mara kwa mara. Tubaki hapa kwa Nyoso kwanza , huyu ni mmoja wa wachezaji waliotokea kuwa kipenzi cha mashabiki wa Simba kutokana na umahiri kwenye eneo lake na hata ukiangalia kwenye timu ya taifa Nyoso amekuwa akiitwa mara kwa mara hali inayoonyesha kuthaminiwa kwa mchango wake , nyoso pia ni mmoja wa wachezaji ambao wameiwakilisha  Simba kwenye michezo karibu yote kwenye ligi na kimataifa . Nyoso pia ni nahodha wa tatu Simba baada ya Kaseja na Boban. Swali la kijiuliza ni je mchezaji huyu ambaye ametokea kuwa senior player Simba anastahili kutupiwa virago kweli? Eti wanasema kuwa anaigharimu timu kwa kadi nyekundu. ntakurudisha nyuma unakumbuka wakati Fernando Torres anacheza Liverpool,kuna wakati kwenye michezo mitano mfululizo ya United na Liverpool Torres alikuwa anafunga kwa kumpita Nemanja Vidic na zaidi ya hapo Vidic amewahi kuonyeshwa kadi nyekundu katika michezo mitatu mfululizo dhidi ya Liverpool,United ilimfukuza? Jibu ni hapana , kwa hali ya kawaida mwanadamu huwa anapima mema na mabaya au faida na hasara yaani profit vs losses kwa kufanya uwiano , Simba imetwaa ubingwa msimu huu hivyo kwa uwiano halisi tu kadi nyekundu kwa nyoso hata zingekuwa kumi bado sio sababu kwa kuwa Simba imemaliza kwa kutwaa taji.
Turudi kwa mtazamo wa jumla ,kuanzia kwa Meshack Abel,Costa,Jabu,Obadiah,Nyoso ,Haruna na Shamte labda na hili la Yondani,. Kuachwa kwa wote hawa kunamaanisha kuwa Simba inapoteza zaidi ya asilimia 70 ya backline yake baada ya kuwa imetwaa ubingwa na kumaliza nafasi ya pili msimu uliopita tena huku ikiwa sawa na timu iliyotwaa ubingwa ,je hii ni sera nzuri ya usajili ambayo inafanya kazi hapa ???
Tukiachana na hayo huku na kule kuna tetesi kuwa Salum Machaku anapelekwa timu nyingine kwa mkopo. Machaku amesajiliwa msimu uliopita toka Mtibwa. Amecheza Simba msimu mmoja ambao Simba imetwaa ubingwa huku ikifika hatua ya mbali kwenye michuano ya kimataifa . Of course tatizo la machaku limekuwa kushuka na kupanda kwa kiwango pasipo kuwa na muendelezo yaani consistency,lakini tusisahau kuwa huu ni msimu wake wa kwanza , ni vigumu kwa mchezaji ku-settle kwenye msimu wa kwanza ,kwanini amehukumiwa na kuonekana hapaswi kupewa nafasi ya pili ya kujidhatiti kwenye Timu.
Majibu ya maswali yote haya ni rahisi sana, Simba haina sera nzuri ya usajili,maamuzi ya kusajili na kuacha wachezaji yanafanyika kiholela holela sana , hata hili la Yondani ukichunguza kwa ukaribu chanzo ni Simba wenyewe , Yondani alikuwa nje ya timu kwa muda mrefu , taarifa zinasema kuwa klabu ilikuwa haimlipi mshahara , Yanga walionyesha interest ya kumsajili siku nyingi , kilichokuwa kinambana ni mkataba lakini alikuwa frustrated sana na ndio maana akasaini yanga baada ya kuonyeshwa fedha ambazo hakuwa amepewa na Simba . Ukiritimba kama huu ndio unaendelea kulihikumu soka la Tanzania na kwa mtaji huu maendeleo tutayasikia kwa wenzetu kina Mariga, Oliech na Obua.

7 comments:

  1. Hata kwa mtaji wa wachambuz kama ww hatuwez kuendelea! Tafuta kaz ya kufanya soka waachie akina jeff na edo!

    ReplyDelete
  2. he he he kiongozi umefunguka,soka bongo maroroso kibao,utumbo utumbo tu

    ReplyDelete
  3. Ndg Shafih,ukiwa mwandishi pia inabidi uwe na uzalendo angalau,kwa uchambuzi wa namna hii nawe hatutafika mbali pia.

    ReplyDelete
  4. Mi ni shabiki wa simba sanaaa kaka hapa upo sahihi kweli kabisa.

    ReplyDelete
  5. Kaka naunga mkono hoja kwa asilimia zote.

    Mchangiaji ulietangulia ushabiki usikufanye ujenge uhasama, hata kama haukatazwi kucomment kwa namna yoyote ile.

    Kama timu ya taifa imekuwa ikiwategemea kwa kila hali mabeki hawa (Nyosso na Yondani) na badala yake wanaingizwa kwenye 'stress' hizi za usajili na mimi nathubutu kusema Simba kwa hapo wanachangia kuuwa soka la Tanzania. Unadhani ni mchezaji gani anaweza kuhimili stress kama hizo na kuendelea kubaki kwenye kiwango? Kila taifa linapotengeneza wachezaji (hasa mabeki)klabu zinaanzisha majadiliano ya kijinga na baadae kuwapoteza wachezaji wale.Mihimili yote ya Tanzania (walinzi wa kati)kwa miaka ya hivi karibuni ukiachia Salum Sued basi wote wameingizwa kwenye mizozo isiyona ulazima na hatimae kukosa mustakabali mzuri wa kudumu kwa kiwango kwenye timu.
    Kama kwa sasa walinzi tunaowategemea (Nyosso na Yondan) wanaingizwa kwenye masakata yasiyostahili just kwa matakwa/manufaa/chuki/uzembe wa watu fulaniunadhani soka letu litaelekea wapi? Au ndio migogoro ikianza Yanga lazima ihamie na Simba? Musitake niamini kuwa migogoro imekuwa kama kitu cha kupokezana kwa Simba na Yanga!

    Tunaomba Simba Sports ikae na iliangalie hili kwa mapana yake, si tu hii issue ya Yondani bali na mengine kama alivyoyaainisha kaka Shaffih. Kama umenunua wachezaji kwa gharama kubwa baadae unamuachwa hata msimu haujaisha na bila ya kuleta manufaa yoyote kwa club hiyo obvious inakuwa hasara kwa club, kama ni hivyo club itakuwa inaelekea wapi?

    Kama club imelenga kujiendesha kisasa, ni lazima iwe na mipango na sera za kisasa za kimichezo na kiuchumi pia.

    Mungu Ibariki Simba (Taifa kubwa), Mungu Ibariki Tanzania.

    Mo de Bebeto.

    ReplyDelete
  6. Ulichoongea ni ukweli mtupu kaka.Hakuna hata chembe ya lisilo kweli hapo.Big up!

    ReplyDelete
  7. yaaaaaah gud article lakin kaka simba inaitaji mabek imara je meshack kipind chote amecheza cmba ni kwel alionyesha kiwango cha kusema apewe namba...KILA SICKU MLISEMA cmba inatatizo la beki bt toka ameondoka owino cmba hajasattle kwenye bek...Na huwa mnashaur kuwa wawe wanackiriza report ya mwalimu je unafikir cmba ndio imechukua jukumu la kuwaacha wachezaj au mwalimu ndio ameshaur?...TURUDI KWA SWALA LA YONDAN YEYE KAAJILIWA NA CMBA ANATAKIWA KUESHIMU MKATABA YONDAN AMETOROKA SIMBA MUDA GANI JE ALITAKIWA AENDELEE KUPEWA MSHAHARA WAKAT HAMFANYIIIIIIII KAZ MUAJILIWA WAKE?2we makin kila timu ipo focused kuendeleza michezo yondani ni m2 mzima hakuweza kukataaaaaa kufanya contract extesion wakat cimba wamemtaka afanye ivyo?na wakat yy hayuko willing kucheza cmbaaaaaa....me naona unataka cmba ionekane wabaya ofoz cio kila m2 ataona mema ambayo cmba inafanya ila kwa swala la kuacha wachezaj c cmba 2 hata ulaya 2nayaona victor,obadia,unataka wakae simba kwa mpira gan waliouonyesha....costa amepewa nafac mungusa amepewa nafas lakin hawajamuimprec mwalimu so how blame directed 2 cmba as if it is player...i think t iz players fault when they come to big club they get complacent...and eventually their perfomanc decrease and wot da club doing is right just 2 ofload ol player who seems looks like barden 2 the club....

    ReplyDelete