Search This Blog

Thursday, June 7, 2012

NINGEKUA YONDANI PIA NINGECHUKUA MZIGO !



Well done Kevin Yondani...hata mimi ningefanya hivyo hivyo...unachukua huku m20 kule m30....watapiga kelele weweeeee lakini mwishowe watapatana. watu wenyewe hawako serious tumewazoea. ingekuwa umesaini katika makampuni mawili serious kama Barrick na Vodacom labda...lakini hizi timu za Kariakoo...wala usihofu. wataelewana tu....hakuna jela hapo. kwanza ebu ona noti zenyewe zinatolewa kwa cash badala ya hundi au transactions zinazoeleweka!!! we live just once....

Yanga kiboko
hii jezi ya Kilimanjaro Lager na taifa Stars imetoka May this year, kwa hiyo ule mkataba wa miaka 17 na majina ya kinyumenyume ni zuga tuu.... Mohamed Shaban tuletee picha kama hii ili tujue kuwa mmemsajili kweli vinginevyo imekula kwenu.... Manji kaanza kazi Jangwani

Nina urafiki na wachezaji wengi wa yanga. Siba,azam na klabu nyingne za bongo hata wachezaji wa ndondo,kitu ambacho huwa nasema siku zote ni kwamba wachezaji wa kitanzania wana matatizo makubwa,of course its like the whole soccer family in bongo is fucked up,Yondani amesaini Yanga wakati akiwa na mkataba na Simba ambako alishasaini tunaambiwa sijui 6 months ago,in my opinion a contract has to be r...espected,sheria za mkataba kimataifa ziko hivi,mkataba ukibaki muda mfupi kuisha lazima mazungumzo yafanyike either kurenew au kuuzwa kwa timu nyingine,in between mchezaji hatakiwi hata kuzungumza na timu nyingine bila ridhaa ya timu ambayo tayari ana mkataba nayo ambayo kwa hali ya kawaida lazima itoe ruhusa mazungmzo yaendelee,in this saga Kelvin Yondani is in hot water for signng for two clubs kama ninachokisikia ni sahihi,pia viongozi wa yanga wana kosa kubwa ambalo ni kufanya mazungumzo kinyume cha taratibu na mtu ambaye tayari ana mkataba,viongozi wa simba kwa upande wao wana kosa la kutengeneza situation ya kumfreeze out yondani kwenye timu hali iliomfrustarte na kumfanya asaini timu nyingine,WHY ALWAYS TANZANIA vitu vya kipuuzi kama hivi vinatokea.


kwa uelewa wangu mdogo na hela hizo ni mil. 18



Pesa ya Manji hiyooooooooo
Kweli Manji agombee Yanga..Na Pesa yote hiyo aliyonayo?
Anatafuta nini? Kuna kitu......Ukiona mtu mzima kayavulia nguo ujue kuna jambo....kazi kwenu yanga.......

9 comments:

  1. kazi kwao watajuana wenyewe

    ReplyDelete
  2. Tatizo ni shule kwa wote! Mohd elhind

    ReplyDelete
  3. Duuuh ama kweli hii ndio Bongo wajameni. Yaani kama kaka Shafii na Jeff wanavyochambua kwenye SPORTS EXTRA kwamba tusilalamike kufungwa na timu kama IVORY COAST nakubaliana nao kabisa. Kwa hali hii hatutafika kabisa.

    ReplyDelete
  4. Kila msimu mambo haya kutifuana kwenye usajili lazima yatokee na hasa yanga kung'ang'ania wachezaji wa simba ni kwa nini lakini? ni wazuri sana au ndo upinzani wenyewe?

    ReplyDelete
  5. Ninachojua mimi ni kuwa Yondani hatacheza msimu huu na hii ni furaha kwa Kunguru maana atasema bora tukose wote. Yaani uchungu wa kufungwa goli 5 ni kulipiza kisasi kwa kuwaharibu wachezzaji. Siwezi kueleza kwa hhabari ya Manji, lakini ninachoamini ni kuwa kuifadhili Yanga ni mbinu ya kujisafisha katika jamii kwa scandol ya EPA. EPA itasimama daima hata kama ukijaribu kuighiribu jamii. Yanga wanapaswa kufahamu kuwa bila kujikomboa katika utumwa wa hao jamaa wataendelea na vita ile ya zamanai kabla jamaa hajajitokeza na kuwanunulia Hisa wanachama. Kumbuka kuna Pan African bado inadai dhuluma ile. Msiliangalie jambo hili kwa macho ya nyama lina chanzo chakke katika ulimwengu wa Roho- poleni msioelewa huo ulimwengu

    ReplyDelete
  6. mutani@usemayo ni swadakta

    ReplyDelete
  7. kama tumeamua ligi yetu iwe ya ndondo hamana tatizo kwa sababu madudu haya haya yanafanywa na yanga na simba ambao wana ukaribu na media ndio mana linageuka gumzo. lakini inawezekana mchezo huu upo siku zote. kingine kinachonikera zaidi ni kuona wachezaji wetu hawana washauri wala hawataki kuwa nao na ndo kama hivio wengi wao shule kidogo ni hadithi. kingereza shida mkataba anaosainiumeandikwa kiingereza what do you expect.hii ndio vodacom ndondo pre legue ya bongo.

    ReplyDelete
  8. Mbona kuna wachezaji wengi wazuri tu ambao wanachipukia, kwa nini Yanga na Simba wanagombania wachezaji ambao kwa kweli kwa kiasi fulani mpira wao na kasi yao ya mpira uwa imepungua sana. Sioni mantiki ya kulazimisha kusainisha mchezaji wa aina hii, tena kwa njia za uchochoroni. Fuateni kanuni. Mpira wetu hauwezi kuendelea kamwe kama hatutabadilika na mtindo huu. Wapo vujana wengi sana na wanaujua mpira vizuri, wasajilini kwa ajili ya mahitaji ya misimu ijayo. Acheni mambo yenu hayo ya kung'ang'ania wazee.

    ReplyDelete
  9. ivi kaka walioandaa mkataba huo na aliyesaini ambaye ni Kervin ndio 2naowategemea katika soka letu sababu mkataba unaonyesha ni ubabaishaji

    ReplyDelete