Search This Blog

Wednesday, December 14, 2011

TFF: SIMBA ISINGEACHANA NA BASENA SISI TUNGEMSIMAMISHA



Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema lilikuwa mbioni kumsimamisha aliyekuwa kocha wa Simba, Mganda Mosses Basena kwa madai ya kutokuwa na vyeti vya taaluma vya kazi hiyo.

Akizungumza kwenye makao makuu ya shirikisho hilo jana, Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah alisema waliwasiliana na Simba zaidi ya mara tatu kuwaomba wawasilishe vyeti vya
kocha huyo, lakini walishindwa kufanya hivyo.

“Tuliwaomba watuletee vyeti vya kocha wao zaidi ya mara tatu lakini hawakufanya kama tulivyowaagiza,” alisema Osia.

Alisema wakiwa mbioni kumsimamisha kocha huyo, ndipo uongozi wa Simba ukatangaza kumtupia virago kocha huyo.

Osiah aliongeza huwa hawana utaratibu wa kukimbilia kutoa adhabu na badala yake wanaanza kufanya mawasiliano na upande unaohusika kuhusiana na jambo lenyewe ikishindikana ndipo hutoa adhabu.

Kocha huyo kutoka Uganda aliweza kufanya kazi zaidi ya miezi mitatu bila kuwa na vyeti vya kazi ya ukocha, ambapo Simba ilimaliza mzunguko wa kwanza ikiwa inaongoza ligi hiyo.

Hivi karibuni uongozi wa Simba ulimleta kocha Milovan Cirkovic kutoka Serbia wakati bado una mkataba na Basena.

Viongozi wa Simba walidai Basena bado kocha wao na kuwa walifikia uamuzi huo kwa vile kocha huyo Mganda hakuwa amewasilisha vyeti vyake na kwamba walichokifanya ni kusitisha mkataba wake, huku kocha huyo akisisitiza Simba imlipe fungu lake kwa kuvunja mkataba.


ZANZIBAR KUSHIRIKI KOMBE LA DUNIA


TIMU ya Soka ya Zanzibar 'Zanzibar Heroes' kwa mara ya kwanza itashiriki fainali za Kombe la Dunia la Viva kwa nchi ambazo si wanachama wa Shirikisho la Soka la Dunia (Fifa).

Zanzibar Heroes imealikwa kushiriki mashindano hayo yaliyoandaliwa na Shirikisho la Bodi la Vyama Soka visivyokuwa mwanachama wa Fifa (NBF). Michuano itafanyika Juni nchini Iraq na kushirikisha nchi nane.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu msaidizi wa ZFA, Masoud Attai alisema tayari ZFA wamepokea mwaliko mashindano hayo ya kila baada ya miaka miwili.Attai alisema baada ya kupokea mwaliko huo viongozi wa ZFA watakutana mapema wiki ijayo ili kujadili ushiriki.

"Hii ni nafasi nzuri kwa timu yetu kuchuana katika mashindano makubwa kama haya, ni jambo la kheri na sisi kama viongozi tutakutana wiki ijayo ili kujadili ushiriki wetu ambao unahitaji maandalizi ya kina," alisema Attai.

Mara ya mwisho mashindano hayo yalifanyika Gozo katika visiwa vya Malta na timu ya Padania iliibuka mabingwa.

Nafasi ya pili ilichukuliwa na Iraq Kurdistan na ile ya tatu kwenda Occitania, mashindano yalifanyika katika Uwanja wa Gozo uliopo Xewkija na Sannat Ground uliopo Sannat.

Mwaliko huo wa NFB kwa ZFA umekuja ikiwa ni miezi michache imepita tangu Fifa walipoikataa ZFA kuwa mwanachama wake.

EXCLUSIVE: WACHEZAJI WA MAN UTD WASHINDANA KWA PAMBA NA MADEMU WAKALI.

BEKI NA NAHODHA MSAIDIZI WA UNITED PATRICE EVRA AKIWASILI NA MKEWE NA KATIKA PARTY KUCHANGIA MFUKO MAALUM WA UNICEF JANA JIJINI MANCHESTER-UK.






Manchester United's English midfielder Michael Carrick and his wife Lisa arrive for the UNICEF dinnerAshley Young and Nicky Pike attend Manchester United 'United for UNICEF'

ASHLEY YOUNG NA MICHEAL CARRICK NANI ANA DEMU MKALI?





Unlikely partners: Rafael and Fabio da Silva smile for the camera


MAPACHA WAWILI WA MAN UNITED: NANI KAMFUNIKA MWENZIE?







Ryan Giggs at the UNICEF dinnerManchester United's English defender Rio Ferdinand arrives for the UNICEF dinner





Stalwarts: Albert Morgan (left), the Manchester United kit-man, with Sir Alex Ferguson (right)

HAPA BABU SIR ALEX FERGUSON NAONA KAMA AMEKALISHWA NA MSAIDIZI WAKE. AU NYIE MNAONAJE WADAU?








Match: Federico Macheda and girlfriend Sophie Larissa Houghton


FEDERICO MACHEDA AKIWA ANAWASILI NA DEMU WAKE KATIKA HAFLA YA UNICEF ILIYOFANYIKA JANA JIJINI MANCHESTER.


.



Trio: Jonny Evans (left) with Darron Gibson (right) and Danielle Carter (centre, Darron's girlfriend)

Trio: Jonny Evans (left) with Darron Gibson (right) and Danielle Carter (centre, Darron's girlfriend)











David de Gea at the UNICEF dinnerJavier Hernandez at the UNICEF dinner



DAVID DE GEA AKIWA NA CHICHARITO: NANI KAPENDEZA?

UNAJUA NANI CHELSEA WANAMTAKA KUZIBA PENGO LA TORRES: MUANGALIE HUYU HAPA.



MWANA MUZIKI WA KIMAREKANI JUSTIN BIEBER JANA ALITEMBELEA MAKAO MAKUU YA CHELSEA NA KUPATA NAFASI YA KUPIGA PICHA NA KUCHEZA SOKA NA WACHEZAJI FRANK LAMPARD NA TORRES. BIEBER ALIONYESHA KIWANGO KIZURI KILICHOWAVUTIA WACHEZAJI HAO.

CHELSEA WAPO TAYARI KUMUUZA TORRES JANUARY KWA £20MILLION




Chelsea wataisikiliza ofa kwa ajili ya mchezaji waliyemnunua kwa ada ya £50million Fernando Torres katika dirisha la usajili la mwezi ujao.


The £150,000 a week striker amefunga magoli matatu katika premier league tangu ajiunge na The Blues kutoka Liverpool mwezi January mwaka huu.


Chelsea walifikiria kumtoa kwa mkopo ili kuweza kurejesha kiwango na kujiamini kwake, lakini sasa wanajiandaa kumuuza.


Japo itakuwa ni vigumu sana kumuuza bila kupata hasara katika fedha waliyotumia kumnunua lakini klabu hiyo inaona ni bora kumuuza kwa fedha £20million ili kuweza kuepukana na hasara wanayopata kwa kumlipa mshahara mkubwa kila wiki.


Wakati Andre Villas-Boas alipokuwa kocha wa Chelsea kipindi kilichopita cha kiangazi alikuwa alishawishikaTorres anaweza kuirudisha form yake ambayo ilimfanya kuwa mmoja wa washambuliaji wanaogopewa kuliko duniani.


Villas Boas alitumaini kumsajili Juan Mata kutoka Valencia kungeweza kuboresha kiwango cha Torres, lakini mpango huo nao umefeli kumrudisha Torres yule wa misimu miwili iliyopita.


The World Cup winner amekuwa akicheza chini ya kiwango tangu ajiunge na Chelsea na sasa yupo nyuma ya Didier Drogba na Daniel Sturridge katika uchaguzi wa kikosi wa AVB.


DARREN FLETCHER AZIDI KULIPA MACHUNGU BENCHI LA MAN UNITED


Darren Fletcher atachukua likizo ya muda mrefu nje ya uwanja baada ya kiungo huyo wa Manchester United kukumbwa na matatizo ya kiafya.

Nahodha huyo wa Scotland amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa “Ulcerative colitis” hivyo ameshauriwa kupumzika na kukaa nje ya uwanja kwa takribani kipindi kisichopungua miezi zaidi ya 6 ili aweze kutibiwa na kupona kabisa.

Kutokana na likizo hiyo ya fletcher anategemewa kukaa nje ya uwanja mpaka mwishoni mwa msimu huu, hali itakayopelekea United kuzidi kupungukiwa na wachezaji wake wa kutegemewa baada ya hivi juzi Nemanja Vidic nae kuumia goti litalomuweka nje hadi msimu ujao.

Tuesday, December 13, 2011

MICHUANO YOTE YA CHALLENGE YAINGIZA MIL.267


Mechi 26 za michuano ya 35 ya CECAFA Tusker Challenge Cup iliyofanyika Dar es Salaam kuanzia Novemba 25 hadi Desemba 10 mwaka huu zimeingiza sh. 267,066,000. Michuano hiyo iliyoandaliwa na Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) ilishirikisha timu za mataifa 12.

Hatua ya makundi ya michuano hiyo iliingiza sh. 145,613,000, robo fainali (sh. 58,470,000), nusu fainali (sh. 55,787,000) wakati fainali iliingiza sh. 17,196,000. Kila siku zilichezwa mechi mbili isipokuwa Novemba 26 mwaka huu ambapo ilikuwa siku rasmi ya ufunguzi na Novemba 28 mwaka huu zilichezwa mechi tatu.

Mechi iliyoingiza fedha nyingi kuliko zote ilikuwa ya ufunguzi hatua ya makundi kati ya Tanzania na Rwanda ambapo zilipatikana sh. 64,178,000 wakati fedha kidogo (sh. 446,000) zilipatikana kwenye mechi kati ya Uganda na Somalia iliyochezwa Novemba 28 mwaka huu Uwanja wa Azam.

Jumla ya washabiki walioshuhudia michuano hiyo walikuwa 103,312. Washabiki walioshuhudia hatua ya makundi walikuwa 65,617, robo fainali (17,844), nusu fainali (16,014) wakati fainali walikuwa 4,837.

Mechi iliyokuwa na washabiki wengi zaidi ni kati ya Tanzania na Rwanda ambapo waliingia 23,946 wakati iliyoingiza wachache ni 446 walioshuhudia mechi kati ya Somalia na Uganda.

Tunawashukuru wadhamini wakuu Tusker na washabiki waliojitokeza kushuhudia michuano hiyo. Vilevile Kampuni ya mafuta ya Gapco, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na PSPF, na pia wadau wengine waliofanikisha mashindano hayo kwa njia mbalimbali akiwemo Zacharia Hanspope.

HATIMAYE MAN CITY NAO WAONJA UCHUNGU WA KUFUNGWA -

RAGE: WAVIVU NA WATOVU NIDHAMU KUTOVUMILIWA SIMBA


WACHEZAJI wavivu na watovu wa nidhamu hawatakuwa na nafasi katika kikosi cha Kocha Mkuu wa timu hiyo, Milovan Cirvociv, raia wa Serbia, ambaye amewasilisha rasmi ratiba yake ya kazi kwa uongozi juzi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage, alisema katika programu ya kocha huyo aliyowasilisha kwa Kamati ya Ufundi ameweka wazi kuwa hatawavumilia wachezaji wavivu na watovu wa nidhamu.

Alisema kuwa kocha huyo amebainisha kuwa atakuwa na mazoezi magumu ili kuwandaa vijana wake kwa ngwe ya pili ya Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho barani Afrika.

“Tumeipokea ratiba ya CAF na pia tunafurahi kwamba kocha wetu, Milovan, ameshatupatia proramu yake huku akisema hatawavumilia wachezaji wavivu na watovu wa nidhamu bali atawatimua kwa kuwa anataka kuiimarisha Simba, na sisi tutamkubalia kwa hilo,” alisema Rage.

Alisema Simba inapigania kuwavua Yanga ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara na pia inataka kufanya vizuri kwenye michuano ya Shirikisho, hivyo itamuunga mkono kocha huyo.

Kwenye michezo ya Shirikisho Simba imepangwa kuanza kampeni yake kwa kucheza na Kiyovu ya Rwanda, mchezo utakaopigwa mjini Kigali, Rwanda kati ya Februari 17 na 19 mwakani na mchezo wa marudiano utapigwa jijini Dar es Salaam kati ya Machi 2 na 4, 2012.

OKWI AIKATAA TUZO YA CECAFA


Mshambuliaji Emmanuel Okwi wa timu ya taifa ya Uganda ‘The Cranes’ amekataa heshima ya kutambulishwa kuwa miongoni mwa wafungaji bora wa michuano ya Kombe la Chalenji iliyomalizika Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwa maelezo kwamba hastahili hadhi hiyo.

Akizungumza jana, Okwi aliyeng’ara katika michuano hiyo na kufunga mabao yaliyoipa nchi yake taji la 12 la Chalenji, alisema kwamba yeye alifunga mabao manne tu na hivyo waliostahili kuitwa ‘wafungaji bora’ wa michuano hiyo ni Warwanda Olivier Karekezi na Meddie Kagere waliofunga mabao matano kila mmoja.

Awali, ilielezwa baada ya kumalizika kwa mechi ya fainali ambayo Uganda walishinda kwa penati 3-2 dhidi ya Rwanda kuwa Okwi, Karekezi na Kagere ndio wafungaji bora baada ya kila mmoja kupachika mabao matano.

Okwi alisema kuwa takwimu hizo si sahihi kwani yeye alifunga mabao manne tu; matatu aliyafunga katika mechi moja ya hatua ya makundi dhidi ya Somalia na jingine ‘alimdungua’ kipa anayecheza naye Simba, Juma Kaseja wa wenyeji Kilimanjaro Stars wakati walipokutana katika mechi yao kali ya nusu fainali.

"Kama wamenijumuisha katika orodha ya wafungaji bora watakuwa wamekosea... mimi nilifunga magoli manne tu. Ila wenzangu (Karekezi na Kagere) wana magoli matano kila mmoja na ndio waliostahili tuzo ya ufungaji bora," alisema Okwi.

HATIMAYE WALUSIMBI KUJIUNGA NA SIMBA MSIMU UJAO


BAADA ya harakati za muda mrefu, Simba imenasa kifaa cha timu ya taifa ya Uganda, The Cranes, ambacho kilitwaa Kombe la Chalenji wikiendi iliyopita.
Simba kwa miaka miwili ilikuwa ikimfukuzia beki wa kushoto, Godfrey Walusimbi na sasa kazi hiyo imefikia tamati.

Walusimbi mwenyewe amethibitisha kuwa atajiunga na Simba kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Ujio wa Walusimbi, ambaye anahesabiwa miongoni mwa mabeki bora wa kushoto katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ni wazi utawapa presha mabeki wa sasa wa timu hiyo, Amir Maftah na Juma Jabu, ambao wamekuwa

wakipokezana nafasi hiyo katika kikosi hicho cha Msimbazi.
Maftah ni majeruhi kwa muda mrefu, sasa Jabu anatamba kwenye nafasi hiyo.
Walusimbi sasa ameamua kujiunga na Simba baada ya kufanya majaribio katika nchi za Sudan na Ethiopia.

Baada ya kukwama kupata timu huko, alirudi Uganda na kujiunga na Bunamwaya, ambako mkataba wake unamalizika baada ya miezi mitatu.

Simba walicheza karata yao wakati wa Kombe la Chalenji na kumshawishi Walusimbi kujiunga nao.

Walusimbi ambaye alicheza mechi zote za Chalenji akiwa amevaa jezi namba 15, alisema; Naipenda Simba na ndiyo klabu yangu ninayokuja kuichezea msimu ujao.

Nimeshafanya mazungumzo na viongozi wao ninachosubiri ni kumalizia mkataba wangu na Bunamwaya na baada ya hapo, nitakuwa huru kukamilisha mambo yangu,alisema Walusimbi, ambaye jana Jumatatu aliondoka na The Cranes kurudi kwao Uganda.

PAMOJA NA KUWA NA MATOKEO MABAYA-BIDHAA MAN UNITED ZAENDELEA KUFANYA VIZURI SOKONI


Pamoja na kwamba club ya soka ya Manchester United imeshuka kutoka nafasi ya kwanza na kuwa ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza mpaka sasa kwa kipindi cha miezi miwili na kutolewa katika ligi ya mabingwa wa ulaya, lakini bado bei za bidhaa za club hiyo ziko pale pale na nyingine zimeongezeka.

Bidhaa kubwa ya man u ambayo inauzwa kwenye maduka mengi Dar es salaam ni jezi, na bei zake zinafanana kwa asilimia kubwa, sasa hivi jezi ya Man U inauzwa elfu 35 kutoka elfu 30 miezi miwili iliyopita, ambapo jezi ya Man U ndio inayoongoza kwa kuuza.

Ni utafiti mdogo uliofanywa na Millard Ayo kujaribu kuangalia kama kushuka kwa Man U kumeathiri mauzo ya bidhaa zake madukani, japo ligi kuu ya England haijamalizika, bado round ya kwanza ambayo kila timu inacheza michezo 19 haijamalizika.

Man U katika miezi miwili iliyopita wamekuwa na matokeo mabovu mpaka kupelekea kutolewa kwenye kombe la FA,Ligi ya mabingwa pamoja na kupata wachezaji majeruhi.

Nimegundua sio jezi za Man U peke yake zilizopanda bei DAR ES SALAAM, hata gum ambazo huwa anazitafuna sana kocha Alex Ferguson nazo zimepanda bei, zinaitwa TREDENT ambazo kutoka shilingi elfu 3 miezi miwili iliyopita, wanaozitumia wameongezeka, ambako kwenye duka wanakoziuza, wanasema kwa siku wanaweza kumaliza box moja, ambapo mwanzo zilianza kwa kuuzwa kwa shilingi 2500.

Monday, December 12, 2011

ANELKA HUYOOOOOOOOO CHINA - DROGBA KUFUATA


Hatimaye leo Nicolas Anelka ametambulishwa rasmi kwa waandishi wa habari kama mchezaji mpya wa Shanghai Shenhua akiwa mchezaji wa kwanza mkubwa wa The Blues kuondolewa kikosini chini ya utawala wa kocha Andre Villas-Boas.

Na sasa Shenhua wana matumaini makubwa kumshawishi Didier Drogba kujiunga na Anelka kwa kuihama Chelsea kwa ajili ya klabu yao.

Taarifa kutoka katika mtandao rasmi wa Chelsea ilisema: “Chelsea Footbal club na Shanghai Shenhua wamekubaliana juu ya uhamisho wa kudumu wa Nicolas Anelka katika dirisha la usajili la mwezi January.”


Sunday, December 11, 2011

BREAKING NEWZ: MAN CITY YAKUBALI KUMUUZA TEVEZ KWA PSG


Manchester city wamekubali ada ya £21million kumuuza Carlos Tevez kwenda Paris Saint-German, jambo ambalo litazusha vita mpya na Tevez anayetaka kujiunga na AC Milan.

Mmiliki wa City Sheikh Mansour anaeleweka kuwa na uhusiano mzuri na karibu na Qatar owners of the French club.

And Roberto Mancini , kocha wa City hayupo katika mood nzuri ya kumridhisha Carlitos na matakwa yake ambaye currently yupo Argentina bila kuwa ruhusa ya klabu yake.

AC Milan wanataka kumchukua Carlitos kwa mkopo inJanuary, huku wakiwa wanataka kumnunua kwa £21million kipindi cha kiangazi kijacho, lakini City, ambao waliwalipa Manchester United £32million kwa ajili ya mshambuliaji huyo in July 2009, hawataki biashara hiyo, wakisisitiza timu inayomtaka Tevez ni lazima wamnunue moja kwa moja.

Juventus jana walionyesha nia ya kumtaka Tevez kitu kilichowafanya PSG kuweka ofa nzuri mezani.

Tevez sasa anategemewa ku-react kwa hasira juu ya suala la City kukubali kumuuza kwenda Ufaransa huku arugue kuwa hawezi kulazimishwa kujiunga klabu yoyote, hali ambayo itaendelea kuvumisha vita kati yake na klabu yake.

ANELKA KUJIUNGA SHANGHAI KWA KWA MKATABA WA MIAKA 3


Nicolas Anelka amekubali kujiunga na Chinese club Shaghai Shenhua.

The French star kwa muda mrefu sasa alikuwa akitegemewa kuondoka Stamford Bridge na alikuwa akihusishwa kuelekea Asia wiki iliyopita.

Na sasa Shenhua wametangaza rasmi kwamba Anelka atajiunga nao na kusaini mkataba wa miaka 3.

Anelka anategemewa kuwa anaingiza kiasi cha £175,000 kwa wiki.

BARCELONA YAENDELEA KUINYANYASA REAL MADRID

INTER MILAN YAIFUMUA 2-0 FIORENTINA

MAJOGOO WA JIJI WAINYOOSHA QPR

VAN 'MAGOLI' PERSIE AZIDI KUNG'ARA ARSENAL WAKIIFUNGA EVERTON

MANCHESTER UNITED YAIMALIZIA HASIRA WOLVES YAITANDIKA 4-1

UGANDA MABINGWA WA CECAFA CHALLENGE CUP

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dk. Ali Mohamed Shein akikabidhi kombe la TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP 2011 kwa wachezaji wa timu ya Uganda (The Cranes) mara baada ya timu hiyo kushinda kombe hilo kwa kuifunga timu ya Rwanda (Amavubi) katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni hii jijini Dar es salaam.

Ilikuwa ni fainali ya kuvutia kwa timu zote mbili kutokana na kiwango kilichoonyeshwa katika dakika 90, timu hizo zilitoka suluhu ya magoli 2-2 ambapo dakika 30 ziliongezwa lakini hazikuzaa matunda kwa timu zote mbili, mpaka ilipofika wakati wa mikwaju ya penati, timu ya Uganda ilipata penati 4-3 dhidi ya Rwanda, hivyo Uganda kutawazwa mabingwa wapya wa kombe hilo.

Wachezaji wa timu ya Uganda wakishangilia mara baada ya kukabidhiwa kombe lao.

Saturday, December 10, 2011

RATIBA YA CAF CHAMPIONS LEAGUE

DOUBLE CLICK TO ENLARGE

CAF WATOA RATIBA: YANGA KUANZA NA ZAMALEK, SIMBA NA KIYOVU


Shirikisho la soka barani Afrika - CAF limetoa ratiba michuano ya kombe la ligi ya mabingwa wa afrika pamoja na kombe la shirikisho.

Wawikilishi wa Tanzania katika kombe la klabu bingwa ya afrika Yanga wamepangwa kuanza na Zamalek ya Misri na mshindi kati yao atacheza dhidi ya Missile ya Gabon au African Sport ya Ivory Coast, huku Mafunzo ya Zanzibar wakianza dhidi ya Muculmano ya Msumbiji na endapo watashinda watakutana na Dynamo ya Zimbabwe.

Klabu ya Simba ya Tz ambayo ni wawikilishi wetu katika kombe la shirikisho wenyewe wamepangwa kuanza na Kiyovu na Rwanda na mshindi wa mechi kukutana na Estif ya Algeria, huku Jamhuri la Zanzibar wakianza na Hwange ya Zimbwabwe na mshindi wa mechi hii atacheza na Amal ya Sudan.

JUVENTUS YAMTAKA TEVEZ KWA £20MILLION

Juventus wamekuwa klabu ya kwanza kuonyesha ishara ya kwamba wapo tayari kulipa £20 million kwa ajili Carlos Tevez mwezi ujao.

Sources in Italy zinasema Raisi wa Juventus Andre Agnelli amezungumza na kocha wa Manchester city Roberto Mancini jana Ijumaa kuhusu Tevez.

Inasemekana kwamba City wapo tayari kumuachia Carlitos atleast kwa ada isiyopungua £20million , na Agnelli aliweka wazi kuwa anataka kumnunua Tevez kwa dili la permanently.

AC Milan walikuwa ndio timu ya kwanza kuzungumza na City kuhusu kumchukua Tevez lakini mkopo kitu ambacho City hawataki hata kusikia.

HIVI NDIVYO NEMANJA VIDIC ALIVYOUMIA

UNITED KUWAKOSA WACHEZAJI 9 LEO DHIDI YA WOLVES


Manchester United imethibitisha kua beki wake Nemanja Vidic hawezi kuonekana tena uwanjani katika msimu mzima baada ya kuondolewa uwanjani kwa kutumia machela baada ya kuumia goti kwenye mechi na Basel ndani ya Ligi ya mabingwa.

kocha Ferguson amesikitika kwasababu alihisi jamaa angetibiwa na kuwa poa ndani ya kipindi kifupi, kumbe sivyo, ambapo nafasi yake inaweza kuchukuliwa na Jones au Smalling.

BBC wamesema Ferguson anakabiliwa na kigezo cha kupoteza hadi wachezaji tisa jumamosi hii wakati watakapocheza na Wolves, ambapo Miongoni mwa wachezaji wasioweza kumsaidia Ferguson ni Michael Owen, Anderson, Tom Cleverley, Fabio, Rafael na Javier Hernandez pamoja na mshambuliaji wa upande wa kushoto Ashley Young alionekana kuzidi kutonesha jeraha la kidole chake katika mechi dhidi ya Basel ambapo ilibidi aondolewe mapema kwenye kipindi cha pili.

MillardAyo.com

Friday, December 9, 2011

THIERRY HENRY AMWAGA MACHOZI BAADA YA ARSENAL KUMTUNUKU NA SANAMU LAKE NJE YA UWANJA WA EMIRATES


KUELEKEA EL CLASSICO KESHO: TUANGALIE MAGOLI 11 BORA KATI YA MADRID VS BARCA

NAMBA 1: LIONEL MESSI

NO.2: SANTIAGO ARAGON

N0.3: RONALDO DE LIMA

NO.4: ROBERTO CARLOS

NO.5: DAVID VILLA

NO.6: JULIO BAPTISTA

NO.7: RAUL

NO.8: XAVI

NO.9: JOHAN CRUYFF

NO.10: ZINADINE ZIDANE

NO.11: RONALDINHO

PMI hosts Football Business Seminar in Tanzania

Mwanzilishi wa Kampuni ya PMI MR MICHAEL HITCHCOCK ATAKUEPO Kwenye semina hiyo.






For Immediate Release
PMI Media
214-335-3865
media@playbookmanagement.com

PMI hosts Football Business Seminar in Tanzania

Dar es Salaam, Tanzania (December 8, 2012) – On Saturday,

December 10th, 2012 9am at the Paradise Express Hotel; Playbook Management International, a Dallas Texas based sports management company will host a Football Business Seminar in East Africa for football leaders from the Tanzania Premier League, CECAFA, Tanzania Football Federation. The Business Seminar will cover topics that range from a historical study of the growth of Major League Soccer, growing the global brand of a professional football league, sustainable business management of a professional football club, strategies to monetize professional football assets, sponsorship strategies, community outreach for professional football clubs including the sharing of best practices from the US and International football clubs and associations.

PMI Founding Partner shared his thoughts on the seminar, “PMI is extremely proud to be here in Tanzania to share our experience and expertise in the business of professional football. It’s an incredible country with a great football future. There’s strong leadership and passionate fans which means that there is tremendous potential. I’m very optimistic in where Tanzanian Football will be in 10 years, on and off the pitch.”

PMI would like to thank seminar partners: Tanzania Premier League, African Lyon FC, Clouds FM and the Paradise Express Hotel.

About Playbook Management International (“PMI”):
PMI is a Dallas, Texas based Sports Management Company that works with professional sports teams, venues and events all over the world to assist our partners in running a more efficient and profitable business operation. PMI brings over 50 years of professional sports management experience to our hand selected clients. For more information on PMI, please visit www.playbookmanagement.com