Search This Blog

Wednesday, December 14, 2011

CHELSEA WAPO TAYARI KUMUUZA TORRES JANUARY KWA £20MILLION




Chelsea wataisikiliza ofa kwa ajili ya mchezaji waliyemnunua kwa ada ya £50million Fernando Torres katika dirisha la usajili la mwezi ujao.


The £150,000 a week striker amefunga magoli matatu katika premier league tangu ajiunge na The Blues kutoka Liverpool mwezi January mwaka huu.


Chelsea walifikiria kumtoa kwa mkopo ili kuweza kurejesha kiwango na kujiamini kwake, lakini sasa wanajiandaa kumuuza.


Japo itakuwa ni vigumu sana kumuuza bila kupata hasara katika fedha waliyotumia kumnunua lakini klabu hiyo inaona ni bora kumuuza kwa fedha £20million ili kuweza kuepukana na hasara wanayopata kwa kumlipa mshahara mkubwa kila wiki.


Wakati Andre Villas-Boas alipokuwa kocha wa Chelsea kipindi kilichopita cha kiangazi alikuwa alishawishikaTorres anaweza kuirudisha form yake ambayo ilimfanya kuwa mmoja wa washambuliaji wanaogopewa kuliko duniani.


Villas Boas alitumaini kumsajili Juan Mata kutoka Valencia kungeweza kuboresha kiwango cha Torres, lakini mpango huo nao umefeli kumrudisha Torres yule wa misimu miwili iliyopita.


The World Cup winner amekuwa akicheza chini ya kiwango tangu ajiunge na Chelsea na sasa yupo nyuma ya Didier Drogba na Daniel Sturridge katika uchaguzi wa kikosi wa AVB.


No comments:

Post a Comment