Search This Blog

Wednesday, June 29, 2011

EXCLUSIVE: ANDY COLE NDANI YA BONGO


MSHAMBULIAJI WA ZAMANI WA MANCHESTER UNITED ANDY COLE AKIWASILI BONGO ASUBUHI HII.

ANDY COLE AKIFANYIWA MAHOJIANO NA JEFF LEA MMOJA WA SHAFFIH-BLOGSPOT


ANDY COLE WA TATU KUTOKA KULIA MARA BAADA YA KUWASILI NCHINI.

USAJILI WA BONGO UNAFUATA MAHITAJI AU SIASA MBELE.


Mara nyingi huwa napenda kuuzungumzia soka letu kwa kufananisha na sehemu zingine mathalani Ulaya , Afrika Kusini , Kenya na kwingineko, inaweza kuwa sio kitu sahihi lakini maendeleo endelevu hupimwa kwa kufananisha vitu viwili ili kuona kama viwango vya maendeleo husika vimefikiwa.

Kabla ya michuano ya Kagame Castle Cup soka lilikuwa limetawaliwa na taarifa za usajili . Timu mbalimbali zilikuwa kwenye harakati za kufanya usajili ili ‘kuimarisha vikosi vyao. Hapa kwenye usajili ndiyo hasa panaponitatiza . Kwa hali ya kawaida usajili hufanywa kwa kuzingatia mapungufu ambayo timu husika inayo . Mfano Manchester United kabla ya msimu kwisha walijua fika golikipa Edwin Van Der Saar angestaafu hivyo mapema walishafanya mipango ya kutafuta mbadala ,vivyo hivyo kwa Gary Neville ambaye hata kabla ya kustaafu kwake waliletwa vijana mapacha kina Da Silva ambao wamefanya vizuri na wameziba vizuri pengo la mkongwe Neville.
Mfano huu unakupa picha gani? Picha kubwa unayopata hapa ni kuwa klabu hii ina sera madhubuti ya usajili ambayo imesimamiwa na ndiyo kiini cha mafanikio ya muda mrefu ya timu hii na nyingine nyingi barani Ulaya .
Sasa kwa hapa nyumbani kwetu klabu huwa zinafanya usajili hovyo hovyo sana kiasi cha kumpa mtu maswali mengi ya kujiuliza . Watazame Simba msimu uliopita walimkosa mtu muhimu sana kwenye safu yao ya ulinzi , Mganda Joseph Owino , na kukosekana kwake kuliwaathiri sana na pengine ni moja ya sababu zilizopelekea kushindwa kuutetea ubingwa ilhali walikuwa na nafasi nzuri ya kufanya hivyo.


Haimaanishi kuwa Simba hakukuwa na mabeki , la hasha, ila mabeki wa aina ya Owino ndio waliokosekana . Walikuwepo Kevin Yondani , Meshack Abel na Juma Nyosso na hata Jerry Santo ambaye pamoja na kuwa kiungo ana uwezo wa kucheza nafasi ya beki wa kati . Mabeki wote waliotajwa hapo ni mabeki ambao wanacheza mtindo mmoja . Wote ni wakabaji wazuri na wana uwezo wa kumkalia mshambuliaji kooni . Ila wana upungufu mkubwa linapokuja suala la kuusoma mchezo na kujipanga wao kwa wao na ndio maana Simba haikupata matokeo mazuri katika mechi nyingi ambazo mabeki hawa walicheza pamoja.

Kwa kuona hili ungeweza kudhani kuwa Simba wangehitaji mtu kama Owino . Inawezekana ndio sababu iliyopelekea tetesi zakurejeshwa Victor Costa ambaye wote tunautambua uwezo wake . Lakini kurejeshwa kwa Costa kunamaanisha kuwa klabu hii itakuwa na mabeki sita wa kati kwani wapo kina Obadia Mungusa na Derick Waluhya walioongezwa . Sitamzungumzia Mungusa, tatizo langu liko kwa Derrick Waluhya . Huyu jamaa ni mgeni , raia wa Uganda ambaye uwepo wake unamaanisha kuwa Simba watalazimika kupunguza idadi ya wageni ambao walikuwa na mipango ya kuwasajili.

Sisemi kuwa Derick ni mchezaji mbaya , hapana , wala hiyo sio maana yangu ila nichojaribu kuonyesha hapa ni ukweli kuwa huu ni usajili usio na maana kwa Simba kwa kuwa sioni tofauti ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Uganda na mabeki ambao tayari wako Simba . Kama ulitazama mchezo wa jumamosi dhidi ya Vital O ungeona ninaloongea .
Derick ni beki mwenye nguvu na anayeijua kazi yake ya kupambana kwani ni mpambanaji haswa ila mara zaidi ya moja yeye na Nyoso walikuwa wanaukimbiza mpira mmoja na mara zaidi ya moja alikuwa anajikuta analazimika kurudi nyuma kukimbiza washambuliaji wakati kama alikuwa anacheza na Nyoso alitakiwa kuwa nyuma yake ili asahihishe makosa yake kama Libero.
Waluhya alikuwa akishangiliwa sana na mashabiki kwani kazi yake ilionekana lakini naamini kwa asilimia zote kuwa kama ingalitokea Waluhya angecheza na mganda mwenzie Owino kwenye kikosi kimoja basi ukuta wa Simba usingepitika .

Uwepo Waluhya unamaanisha kuwa Simba haiwezi kusajili mshambuliaji tishio ambaye anaweza kuipa Simba mabao muhimu na kuponya ugonjwa sugu wa kina Mgosi wa kukosa magoli ugonjwa ambao umeigharimu mno Simba.
Hapo hapo Simba kuna kipa mpya toka Kenya anayeitwa Wilson Ochieng.kipa huyu amepewa kiasi cha doka elfu ishirini ($ 20,000) na mkataba wa miaka 3.


Ni kipa mzuri na rekodi yake inajieleza bila ubishi wala kificho kwani amewahi kucheza soka nje ya nchi yake na alikuwemo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Kenya ambacho kilishiriki michuano ya kombe la mataifa ya afrika kwa mwaka 2004 nchini Tunisia. Lakini anakuja Simba ambako tayari yupo Juma Kaseja , kipa ambaye ni roho na uti wa mgongo wa timu , amechezea klabu hii kwa muda mrefu ana uwezo ambao haupishani sana na kipa huyu Mkenya.

Hivi Karibuni Kaseja ametia saini mkataba mpya wa miaka 2 kuitumikia Simba.Kaseja kwangu anabaki kuwa kipa bora na haingii akilini kumleta kipa mwingine tena kwa bei kubwa kama ilivyokuwa kwa Wilson Ochieng , jamani kipa wa akiba hawezi kuwa ‘high profile’ ,huwezi kukuta kipa namba moja kwenye timu ni Peter Cech halafu msaidizi wake ni David De Gea au Victor Valdez , hili linaweza kutokea tu kwenye timu ya taifa na si klabu ambapo unaweza kukuta kipa anacheza misimu mitatu bila kubadilishwa.Ni sera ipi iliyotumika kumsajili Wilson Ochieng?
Ndolo vs Niyonzima

Tuachane na Simba na tuhamie kwa mahasimu wao wakubwa Young Africans . Kuna majina matatu ambayo ni Kiza Hamis , Niyonzima Haruna na Ndolo . Kesi inayowahusu wachezaji hawa ni kwamba Yanga itakuwa na idadi ya wachezaji sita wa kigeni ilhali wachezaji wanaohitajika ni watano . Kati ya wachezaji hawa watatu kuna wawili ambao ni chaguo la kocha Sam Timbe na mmoja ambaye si chaguo la kocha ila ametokea kuteka hisia za viongozi,wanachama na mashabiki wa Yanga kiasi kwamba kama asingesajiliwa amani klabuni ingepotea . Hilo linakuonyesha kuwa hakuna sera ya usajili.Achana na kesi ya waganda hao wawili na Niyonzima , kuna jina ambalo halimo kwenye usajili wa Yanga msimu huu Ernest Boakye . Boakye kwa mtazamo wangu alikuwa mmoja ya wachezaji muhimu sana kwa Yanga na hata kwenye michezo dhidi ya Simba iliyochezwa msimu uliopita, Boakye alikuwa muhimu sana kwa Yanga kwenye nafasi ya kiungo, sijui kama kuna mchanganuo wa msimu uliopita na viongozi wa vilabu vyetu hivi juu ya michango ya wachezaji Fulani na umuhimu wao kwenye timu zao na ndio hasa ukafanyika usajili .
Usajili wa Humud Azam…

Ukiwatizama Azam msimu huu ni mojawapo ya timu ambazo zimefanya usajili makini sana , wanaye mshambuliaji hatari Kipre Tchetche ambaye naamini hataifaidi Azam kwa umahiri wake tu bali hata kiuchumi kwa sababu ana uwezo unaoweza kushawishi vilabu vikubwa nje ya nchi kumnunua japo Azam wana mafedha ya kutosha . Ila katika usajili huo kuna walakini kidogo . Mwaka jana Azam waliipiga bao Simba kwenye usajili wa Patrick Mafisango , mchezaji ambaye ni muhimu sana kwenye timu yoyote kutokana na uwezo wake wa kucheza mpira na kumudu nafasi nyingi uwanjani . Lakini msimu huu Azam wamembadili Mafisango na mchezaji toka Simba Abdulhalim Humoud . Humoud ni mchezaji mwenye kipaji halisi ambacho hakipingiki .Ila msimu uliopita haukuwa mzuri kwake akiwa Simba na kiukweli uwezo wake umeshuka kwa asilimia Fulani . Wenzetu ulaya huzingatia baadhi ya vitu kabla ya kumsajili mchezaji , vitu hivyo ni historia ya mchezaji , uwezo wake wa kucheza pasipo kuumia kwa muda mrefu na cha muhimu kabisa ni mchango wa mchezaji husika kwa timu anayotoka . Hii inamaanisha alicheza asilimia ngapi ya mechi za timu yake , kama alicheza mechi pungufu ya asilimia sabini na tano lazima uhoji mara mbili kabla ya kumsajili . Humoud alicheza mechi chache sana akiwa na Simba msimu uliopita na hilo linanipa maswali mengi kuhusu aliyefanya uamuzi wa kumsajili Azam. Ukiachana na mchango wa mchezaji kwa upande wa mechi kuna uwezo halisi wa mchezaji , Mafisango ana uwezo wa kumudu nafasi zaidi ya mbili uwanjani , humoud yeye anacheza nafasi moja tu ambayo ni kiungo wa kati , ina maana kuwa Simba wamepata faida ya kuwa na mchezaji ambaye ni sawa na wachezaji watatu ndani ya mchezaji mmoja .Kwa kutazama usajili ulivyofanyika ni dhahiri siasa zinatawala kuliko ufundi , je soka letu litapiga hatua kwa mtindo huu?

Tuesday, June 28, 2011

HUYU NDIYE MWANAMKE WA KWANZA DUNIANI KUFUNDISHA TIMU YA SOKA YA WANAUME.



Mwanama aitwaye Donna Powell ametengeneza historia huko nchini Uingereza ya kuwa mwanamama wa kwanza kuwa kocha wa timu ya soka.na hii yote ni baada ya kushinda shindano la kumtafuta kocha mwananama wa kwanza wa timu moja ya nchini Uingereza iitwayo Fisher Athletic.
Mama Powell alipewa jukumu hilo la kuwasaidia Fisher athletic kuepuka kushuka daraja baada ya kushinda mnada ambao zawadi yake ilikuwa ni kupata nafasi ya kufundisha soka kwa siku moja katika timu ya Fisher.
Inaaminika kuwa Mama Powell ndiye alikua mwanamama wa kwanza kuwa kocha wa klabu ya soka ya wanaume.
Lakini hii yote ilianzaje? na ikawaje hadi mwanamke huyu akajikuta akikabidhiwa jukumu hilo zito la timu hiyo ambayo ukiachilia mbali matatizo yake ya kifedha pia ilikua hatarini kushuka daraja.
Mama Powell mwenyewe alinukuliwa akisema kuwa mabosi wa timu hiyo walifanya mkutano na kufikia uamuzi wa kufanya shindano la kumtafuta kocha wa kike kwa siku moja ikiwa ni njia ya kuchangisha pesa kwa ajili ya kuinusuru klabu hiyo.Mama Powell anakubali kuwa isingekuwa hilo shindano kamwe asingeweza kupata nafasi hiyo sababu kubwa ikiwa yeye ni mwanamke.
Mwanamke huyo alielezea kwamba alishawahi kuomba kazi katika nafasi hiyo mara baada ya kocha wa zamani kuondoka lakini mabosi walifikiri kuwa anatania.Lakini kipindi hiki Mama Powell alijipiga mfukoni akakusanya kiasi cha pauni 500 ili aweze kushiriki katika shindano lililomuweka hapo.
Mama Powell ambaye kabla ya hapo alikuwa kocha wa timu ya vijana chini ya miaka 11 iitwayo Red Lion Boys club amekabidhiwa mikoba ya kuifunga timu ya Eastleigh katika mechi yake ya kwanza akiwa katika benchi la ufundi la Fisher athletic.
Tayari Mama Powell anakwambia alishafanya utafiti kuhusu timu pinzani na mpango wake wa kwanza ni kubadili mfumo wa uchezaji wa timu yake toka mfumo wa 3-5-2 wa na kuwa 4-4-2 sababu aliamini vijana wake wangecheza mfumo huo wangepata nafasi ya kumiliki mpira zaidi.
Mwenyekiti wa klabu ya Fisher Martin Eddie alisema kwamba baada ya mwezi tu ndani ya msimu iliwalazimu kuwaachia wachezaji wote waondoke sababu walishindwa kuwalipa mishahara yao.Kocha wa zamani ilibidi aondoke na kuhamia timu nyingine wakabaki mabosi wawili akiwemo mwenyekiti na watu wachache waliojitolea kuisaidia timu hiyo.
Mama Powell hakuamini kabisa kuwa Fisher wangeshuka daraja ingawa kwa walikuwa katika nafasi ya pili toka mkiani wakiwa wamefungwa mechi 11 mfululizo!Mama Powell anajiamini sana juu ya uwezo wake na mara zote huwa yuko thabiti na msimamo wake kuwa Fisher haitoshuka daraja kamwe.Anachukulia kazi yake kwa umakini mkubwa sana.
Ingawa kifedha klabu hiyo haikua katika hali nzuri Mama Powell aliamini kuna njia nyingi sana za kuwahamasisha wachezaji katika vyumba vya kubadili nguo ama mazoezini.Kila mchezaji alijua baada kufungwa mechi 11 mfululizo kilichohitajika ni ushindi tu na wala si kingine.
Mama Powell ambaye ana daraja la kwanza na pili la ukocha linalotambulika na chama cha soka nchini Uingereza si mgeni katika ulimwengu wa soka uliotawaliwa na wanaume.na alijua fika mikiki mikiki yote ambayo angekumbana nayo wakati akiwa katika benchi la timu ya Fisher. hii ilikua nafasi ya kungara kwa nyota yake.
Anaelezea kwamba alishawahi kukumbana na makocha wa timu pinzani ambao waligoma kusalimiana naye mara baada ya timu yake kuwapo kichapo.Anasema wengi huwa wanakuwa wakijisikia wamedhalilishwa sababu ya kufungwa na mwanamke.
Anamalizia kwa kusema kuwa anadhani ni muda umefika kwa wanawake kufundisha soka.kama wanaume wanaweza kwa nini wanawake wasiweze?

HII NDIYO SIRI YA KIPARA CHA PIERLUIGI COLLINA

HII ILIKUA FAINALI YA MAN U VS BAYERN MUNICH MWAKA 1999

Collina alikuwa ni mwamuzi wa kiitaliano anayechukuliwa na wadau wa soka duniani kama muamuzi bora aliyewahi kutokea.Nguli huyu alikuwa ni mwamuzi mwenye haiba na mwenye kuogopwa na wachezaji anapokuwa uwanjani.Lakini pia alikua ni mwamuzi ambaye timu nyingi zilifurahia kupangiwa achezeshe michezo yao kwani uamuzi wake mara nyingi haukuwa na makosa.

Collina alizaliwa tarehe 13 Februari 1960 mjini Bologna na kupata elimu yake ya chuo kikuu katika mji huo huo akipata shahada ya uchumi mnamo mwaka 1984.Kabla ya kupata shahada yake alihudhuria mafunzo madogo ya uamuzi mwaka 1977 na hapo ndipo alipoanza kugundua uwezo wake katika fani hiyo.

Baada ya miaka mitatu Collina alijikuta akichezesha mechi kubwa zaidi katika jimbo lake huku wakati huo huo akimalizia mafunzo ya lazima ya jeshi,mwaka 1988 alichaguliwa kuwa mwamuzi katika ligi daraja la tatu nchini Italia yani serie C1 na serie C2.baada ya misimu mitatu alipanda daraja na kuwa mwamuzi wa ligi daraja la pili yani serie B na baadaye kidogo akapandishwa kuchezesha serie A.


COLLINA AKIWA NA TUZO YA UEFA.

Katika wakati huu aliugua ugonjwa Fulani uitwao alopecia uliosababisha apoteze nywele zake zote na hivyo watu wake wa karibu kumpa jina la utani la “kojak”.

Mnamo mwaka 1995 baada ya kuwa mwamuzi katika mechi 43 za ligi kuu ya Italia aliwekwa katika orodha ya waamuzi wa FIFA.Alichaguliwa kuwa muamuzi katika mechi tano za mashindano ya Olimpiki ya mwaka 1996 ikiwemo mechi ya fainali kati ya Nigeria na Argentina.

Alikuwa mwamuzi katika mechi ya Fainali ya kombe la mabingwa barani ulaya mwaka 1999 kati ya Bayern Munich na Manchester United.Collina anachukulia mechi hii kama mechi anayoikumbuka zaidi katika historia yake sababu ya sauti za washabiki mara baada ya mechi kwisha zilikuwa kama muungurumo wa simba.

Mwaka 2002 ulikuwa ni mwaka wa kukumbukwa katika maisha yake ya uamuzi kwani alichaguliwa kuwa muamuzi wa mchezo wa fainali ya kombe la dunia kati ya Brazil na Ujerumani .Kabla ya mchezo nahodha wa timu ya Ujerumani alisikika akiwaambia wandishi wa habari wa Ireland.com kuwa “Collina ni muamuzi wa kimataifa lakini huwa analeta bahati?”.alisema hivi sababu katika mechi mbili ambazo kahn alikuwepo huku Collina akiwa muamuzi yani mechi ya fainali kombe la mabingwa ulaya 1999 na mechi kati ya Ujerumani na Uingereza mwaka 2001 ambapo ujerumani ilifungwa 5-1.hata hivyo bahati ya Kahn haikubadilika katika fainali hiyo.




Mwaka 2003 Collina alichapisha kitabu cha historia yake kilichoitwa kwa Kiingereza “The rules of the game”.

Mchezo wake wa mwisho kimataifa ulikuwa ni wa fainali ya kombe la UEFA mwaka 2004 kati ya Valencia na Olympique Marseille kwani alifikisha umri wa miaka 45 na hivyo alitakiwa kustaafu kwa sheria za waamuzi wa FIFA.
Hata hivyo Chama cha soka nchini italia kiliongeza umri wa kustaafu kwa waamuzi hadi miaka 46 ili kumuongeze a Collina mwaka mmoja zaidi.Hata hivyo kulitokea msuguano kati ya Collina na chama cha soka nchini Italia baada ya Collina kusaini mkataba wa kibishara na kampuni ya Opel mkataba huu ulionekana kama ugesababisha upendeleo kwa timu ya AC Milan amabao walikuwa wakidhaminiwa na kampuni hiyo hiyo ya Opel na hivyo Collina alilazimika kujiuzulu na hivyo kuacha rasmi uamuzi wa soka.




Baada ya maisha yake ya Uamuzi Collina amekuwa akijishuhulisha na masuala ya kibiashara kwani sura yake imetumika katika matangazo kadhaa kama matangazo ya adidas na Mastercard katika kombe la Dunia 2006 pamoja na michezo ya video ya Pro Evolution Soccer 3 na Pro Evolution Soccer 4.
Ingawa Collina anatambulika sana katika ulimwengu wa soka .timu ya michezo aipendayo ni timu ya mpira wa kikapu ya Fortitudo Bologna ambayo amekuwa mshabiki wake wa muda mrefu.
Collina anaishi katika mji wa Viarregio na mke wa kiitaliano aitwae Gianna na watoto wawili na mbwa wao aitwae Wallace.
Kwa sasa Collina na Kampuni yake ya kutoa ushauri wa kibiashara.

COUNTDOWN:MPAMBANO WA KUFA MTU KATI YA HAYE NA KLITSCHKO


KWA MUDA WA MIAKA MIWILI SASA ULIMWENGU UMEKUWA UKILISUBIRI PAMBANO LA MASUMBWI KATI YA DAVID HAYE BINGWA WA UZITO WA JUU TOKA ENGLAND NA YOTE KATI YA WANANDUGU WAWILI TOKA FAMILIA YA KLITSCHKO VLADMIR NA VITALY.

PAMBANO HILI LIMEWAHI KUPANGWA HAPO AWALI LAKINI KWA SABABU KADHAA LIMESHIA HEWANI ILA SASA HAKIKA LITAFANYIKA NA HAKUNA WA KUMKIMBIA MWENZIE KWANI TAREHE 2 MWEZI JULAI KWENYE UWANJA WA MPIRA WA HAMBURG ARENA PAMBANO KUBWA NA LA AINA YAKE AMBALO HALIJAONEKANA KWA MUDA WA MIAKA KARIBU KUMI LITAFANYIKA.


DAVID DERON HAYE AMEKUWA AKIPANDA CHATI ZA MCHEZO WA MASUMBWI KWA KASI YA JUU NA AKIWA NA UMRI WA MIAKA 30 AMEDHIHIRISHA UWEZO WAKE WA KUPAMBANA KATIKA HALI NGUMU DHIDI YA MABONDIA WALIOMZIDI KIMO , NA KATIKA MAJARIBU MBALIMBALI UWEZO WAKE WA KUTUMIA KASI NA AKILI NYINGI NDIO UMEMPA USHINDI LAKINI DHIDI YA VLADMIR KLITSCHKO.
BONDIA ANAYETUMIA NGUVU SAMBAMBA NA AKILI NYINGI DAVID HAYE HAKIKA ANAKUTANA NA MTIHANI MGUMU KULIKO YOTE ALIYOWAHI KUKUTANA NAYO . HADI SASA HAYE ANA REKODI YA KUCHEZA MICHEZO 26 AMBAPO AMESHINDA MARA 25 , 23 KATI YA MARA HIZO IKIWA KWA NJIA YA KNOCK OUT HUKU AKIPOTEZA MCHEZO MMOJA TU NA AMEWAHI KUTWAA MEDALI YA SHABA KWENYE MASHINDANO YA DUNIA YA NDONDI ZA RIDHAA HUKO BELFAST MWAKA 2001.

VLADMIR KLITSCHKO AKA DR STEEL HAMMER KWA UPANDE WAKE NI MTU AMBAYE ULIMWENGU WA MASUMBWI UNAMTAMBUA VYEMA . KAKA YAKE AMECHUKUA NAFASI YAKE KATIKA HISTORIA YA MASUMBWI NA SASA NI ZAMU YAKE . SIKU ZOTE KLITSCHKO MDOGO AMEKUWA AKIWAONEA MABONDIA ALIOKUTANA NAO KWA MAKONDE YAKE YENYE NGUVU ANAYOTUPA KWA USTADI NA MAHESABU MAKALI .


AKILI NYINGI ALIZO NAZO AMBAZO ZINASAIDIWA SANA NA UWEZO WA HALI YA JUU ALIO NAO KWENYE MCHEZO WA CHESS AMBAO SAMBAMBA NA KAKA YAKE VITALY AMEWAHI KUCHUKULIA UBINGWA WA DUNIA UNACHANGIA SANA AKILI NYINGI ANAZOTUMIA AKIWA ULINGONI LAKINI HATA YEYE MWENYEWE ANATAMBUA FIKA KUWA KIWANGO CHA KUJIAMINI CHA DAVID HAYE NA UWEZO HALISI WA KUTUPA MAKONDE YA KASI NA WEPESI AMBAO SIKU ZOTE HUMLETEA FAIDA NI VITU AMBAVYO KLITSCHKO ATALAZIMIKA KUTUMIA UJANJA AMBAO HAJAWAHI KUUTUMIA SIKU ZA NYUMA KAMA ATATAKA KUMSHINDA MUINGEREZA HUYU.

VLADMIR KLITSCHKO ANA REKODI YA KUCHEZA MICHEZO 58 AMBAPO AMESHINDA MARA 55 , AKIWA NA KNOCK OUT 49 HUKU AKIWA AMEPOTEZA MARA 3 . DR STEEL HAMMER PIA AMEWHAI KUTWAA MEDALI YA DHAHABU KWENYE MICHUANO YA OLIMPIKI ILIYOFANYIKA HUKO ATLANTA MAREKANI MWAKA 1996 PAMOJA NA MEDALI YA SHABA KWENYE MASHINDANO YA HUKO VELJE ILIYOFANYIKA MWAKA HUO HUO WA 1996,
JULAI MBILI NI TAREHE AMBAYO ITAINGIA KWENYE HISTORIA YA MCHEZO WA MASUMBWI KWANI MMOJA KATI YA WATU HAWA WAWILI , TOKA UKRAINE AU TOKA ENGLAND ATAONDOKA ULINGONI AKIWA AMEVALIA MIKANDA MINNE KIUNONI MWAKE.

JE ITAKUWA VLADMIR KLITSCHKO AMBAYE ATAONGEZA MKANDA MMOJA WA WBA UNAOSHIKILIWA NA HAYE JUU YA MIKANDA YAKE YA YA IBO , IBF NA WBO AU KINYUME CHA HAPO YAANI HAYE KUONGEZA MIKANDA INAYOSHIKILIWA NA VLADMIR JUU ULE WA KWAKE , JIBU LITAPATIKANA JULAI MBILI HUKO HAMBURG UJERUMANI.

ON THIS DAY : MAN UTD ALIPIGWA 'WASH' / 'SUPER' kwenye fainali ya UEFA Champions League.

Ni mwezi mmoja umepita sasa tangu Man utd walipofanywa kitu mbaya na Fc Barcelona kwenye mchezo wa Fainali ya UEFA Champions League mnamo may 28 kwenye dimba la Wembley.
katika fainali hiyo Man Utd hawakupata kona hata moja na mashabiki wa soka walikifananisha kitendo hicho kama kufungwa 'woshi' kwenye mchezo wa POOLTABLE au kupigwa 'Super'

kwenye mchezo wa DRAFT.



Monday, June 27, 2011

KIGOGO CHA SOKA NCHINI ARGENTINA RIVER PLATE MARA BAADA YA KUSHUKA DARAJA HALI ILIKUA TETE KWA MASHABIKI WAKE.






COUNTDOWN:MPAMBANO WA KUFA MTU KATI YA HAYE NA KLITSCHKO


Kuanzia leo blog yako itakua inakuletea habari kuelekea mpambano wa ndondi za uzito wa juu duniani.







RAUL ALBIOL AMLIPIZIA NSAJIGWA

BEKI WA REAL MADRID RAUL ALBIOL JANA ALIFUNGA NDOA NA MCHUMBA ALICIA ROIG JIJINI VALENCIA-HISPANIA.

KALI YA LEO! SINEMA YA TRESOR BABI MPUTU









Huu ulikua mchezo kati ya APR na TP MAZEMBE,


TP walikua waalikwa wa KAGAME CUP kwenye mashindano ya mwaka jana yaliyofanyika nchini Rwanda.
Baada ya mwamuzi kupuliza filimbi ya kuashilia mchezaji mmoja wa TP alikua meotea,wachezaji wa TP hawakukubaliana na maamuzi hayo na kuanza kumzonga mwamuzi,Tresor mputu ndiye alikuwa nahodha na pia akawa msitari wa mbele kuonyesha vitendo vya utovu wa nidhamu mwishowe akalimwa kadi nyekundu na hapo ndipo 'mtiti' ulipoanzia ambapo wachezaji wa TP wakiongozwa na nahodha wao huyo walisababisha mchezo huo kuvunjika baada ya kumpiga mwamuzi.




kitendo hiki kilimpelekea Mputu kufungiwa na FIFA kutocheza soka kwa muda wa mwaka mmoja, hivi sasa anaelekea mwishoni kumalizia kifungo chake.

DA GEA AWASILI ENGLAND KUFANYA VIPIMO VYA KUJIUNGA NA UNITED

DAVID DA GEA AKIINGIA NDANI YA HOSPITAL YA BRIDGEWATER HUKU MAOFISA WA MAN U WAKIJARIBU KUMFICHA


David de Gea amewasili nchini Uingereza na sasa anafanyiwa vipimo vya afya ili aweze kukamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Manchester United kutoka Atletico Madrid kwa dili paundi millioni 18.
Da Gea mwenye umri wa miaka 20 ameonekana katika hospital Bridgewater jijini Manchester tayari kufanyiwa vipimo hivyo mchana wa leo ili aweze kukamilisha uhamisho wake wa kuja kuwa mrithi wa golikipa Edwin Van Der Sar aliyestaafu.

LEO KATIKA USAJILI BARANI ULAYA


FABREGAS YUPO TAYARI KUKOSA £5 MIL. KWA AJILI YA BARCA

Cesc Fabregas yupo radhi kukosa paundi million 5 katika gawio la uhamisho wake ili aweze kupunguza bei ya Arsenala wanayoitaka kutoka Barcelona.
Arsenal wiki iliyopita waliripotiwa kukataa ofa ya paundi million 27 kutoka kwa Barca kwa ajili kumsaini Fabregas.
Katika mkataba wa kiungo huyo wa Spain kuna kipengele kinasema kuwa Arsenal wakimuuza Fabregas kwa timu yoyote itabidi wampe gawio la asilimia 15 la fedha ya uhamisho, hivyo kupitia kipengele hicho Cesc anatarajiwa kuwaambia Arsenal wasimpe kiasi cha £5 milion kutoka katika katika ofa ya £ 33 million, kiasi ambacho Barcelona wanajipanga kueleka kwa Gunners kwa ajili yake ili aweze kurahisha uhamisho kutoka Emirates kuelekea Nou Camp.

MAN UNITED NA ALCANTARA + NASRI

Klabu bingwa la ligi kuu ya England wanaripotiwa kupeleka ofa ya paundi millioni 15 kwa ajili ya kupata saini ya kiungo wa Spain na Barcelona Thiago Alcantara.

Thiago amekuwa akitumika na Barca katika harakati za kutaka kumrudisha Cesc Fabregas Nou Camp kwa

kumtoa kwa mkopo au kumuuza kwa Arsenal kwa mkataba utakaokuwa na kipengele cha kuwawezesha wao(Barca) kumnunua watakapomhitaji tena, sasa amekuwa gumzo katika dirisha la usajili barani ulaya akifuatilwa na timu kama Chelsea na Bolton.

United wanamuona Alcantara kama moja ya viungo wanaoweza kuziba pengo la Paul Scholes hivyo kumfanya Sir Alex Ferguson kufungua pochi kwa ajili ya kinda huyo aliifungia timu yake ya Spain bao la ushindi katika fainali ya EURO under 21, weekend iliyopita.

Wakati huo huo taarifa za ndani kutoka kutoka ndani ya klabu hiyo ya Mashetani Wekundu zinasema kuwa Mnager wa United anatarajiwa kupeleka ofa nzuri ya paundi million 20 kwa Arsenal kwa ajili ya kiungo kifaransa Samir Nasri.

Man United ambao wakuwa wakihusishwa na kuhitaji huduma za Nasri tangu mchezaji huyo alipokataa kusaini mkataba mpya na klabu yake kutokana na masuala ya mshahara anaotaka sasa wanaonekana kuwa serious na kukamilisha uhamisho wa mchezaji huyo kabla ya kuanza kwa mataarisho ya ligi ya msimu ujao.


HAPPY BIRTHDAY RAUL GONZALEZ BLANCO

Siku kama ya leo June 27, mjini Madrid Hispania Raúl González Blanco alizaliwa moja ya washambuliaji hatari kuwahi kutokea kwenye soka alizaliwa.
Raul ambaye kwa sasa ni mchezaji klabu ya kijerumani Schalke 04 ametumia muda mwingi wa maisha yake kuitumikia klabu ya Real Madrid kuanzia mwaka 1994 mpaka 2010, amefanikiwa kuwa mfungaji bora wa muda wote, akishinda kombe la klabu bingwa ya ulaya mara 3, pia akiwa ndio mfungaji bora wa mashidano wa michuano hiyo ya ulaya.
Aliondoka Real Madrid baada ya kuwasili kwa Jose Mourinho akiwa ameifungia timu hiyo mabao 323 katika mechi 741.
Pia Raul anshika nafasi ya pili nyuma ya David Villa kwa kufunga mabao mengi ndani ya historia ya timu za taifa za Spain akiwa amefunga mabao 44.
Raul atakumbukwa pia kwa ushangiliaji wake wa kubusu pete ya ndoa ikiwa ni ishara ya kuithamini ndoa yake na mkewe Mamen Sanz ambaye ameaa nae watoto wanne wa kiume, mapacha Hector na Mateo, Hugo, na Jorge ambaye amempa jina la mtu anayempaenda na kumhusudu sana Jorge Valdano, na mmoja ya kike aitwaye Maria.


HIZI NI REKODI ZA KAMA MCHEZAJI

EXCLUSIVE: SHADRACK NSAJIGWA AVUTA JIKO

USIKU WA TAREHE WA TAREHE 26/6 NAHODHA WA YANGA NA TAIFA STARS SHADRACK NSAJIGWA ALIAS FUSO ALITIMIZA NDOTO YAKE YA MUDA MREFU BAADA YA KUFUNGA NDOA NA MCHUMBA WA SIKU NYINGI JANE.
NDOA HIYO ILIFANYIKA KATIKA UKUMBI WA JKT MGULANI, NA ILIHUDHURIWA NA WATU TOFAUTI, NDUGU,JAMAA, MARAFIKI WAKIWEMO WACHEZAJI WA TIMU YA YANGA,AZAM NA SIMBA.




MAMA NSAJIGWA





BABA YAKE NA SHEDRACK NSAJIGWA AKIWA KATIKA POZI


BAADHI YA WACHEZAJI NA VIONGOZI WA YANGA WAKIPIGA PICHA NA MAHARUSI


KIUNGO WA YANGA NA TAIFA STARS GODFREY BONY YEYE ALIKUWA UPANDE WA KAMATI YA VINYWAJI


JUMA KASEJA NA MOHAMED BANKA 'FIGO; WALIIWAKILISHA SIMBA


MSHAMBULIAJI WA AZAM MRISHO NGASSA AKILISAKATA RHUMBA NA JAMAL RWAMBO KAMANDA WA POLISI


BWANA HARUSI NSAJIGWA AKIMPA ZAWADI MKURUGENZI WA MAWASILIANO WA KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI,TEDDY MAPUNDA AMBAYE PIA ALIKUA MTENGENEZAJI WA KEKI HIYO YA HARUSI.


NSAJIGWA NA MKEWE WAKICHEZA PAMOJA NA NGASSA



MCHEZAJI WA ZAMANI WA YANGA SALVATORY EDWARD AKIWA NA OMEGA SEME NA CANAVARRO


WANANDOA WAKIPATA MSOSI


JUMA KASEJA AKIWAPONGEZA BIBI NA BWANA HARUSI


FREDY MBUNA AKIWA NA MKEWE PAMOJA NA BWANA HARUSI NA MOHAMED BANKA


WASIMAMIZI WA BWANA HARUSI, KIGGI MAKASSY, NGASSA NA OMEGA


WACHEZAJI WA YANGA PIUS KISAMBALE, NURDIN BAKARI NA DAVIS MWAPE WALIKUJA KUMSAPOTI NAHODHA WAO

KAGAME CASTLE CUP: YANGA VS EL MEREIKH MATUKIO



KIPA WA EL MEREIKH AKIWA NDANI YA NYAVU BAADA YA KUFUNGWA BAO LA KWANZA NA KUSAWAZISHA KWA YANGA.
KIKOSI CHA YANGA KILICHOANZA LEO DHIDI YA EL MEREIKH YA SUDAN
KIKOSI CHA WAWIKILISHI WA SUDAN ER MEREIKH KILICHOANZA DHIDI YA YANGA
MASHABIKI WA YANGA, DINO MCHEZA WA FILAMU AKIWA NA SWAHIBA YAKE



MOHAMED HUSSEIN MMACHINGA ALIKUWEPO UWANJANI KUTOA SAPOTI KWA YANGA


VITUKO VILIKUWEPO KAMA KAWAIDA

Sunday, June 26, 2011

KAGAME CASTLE CUP: LIVE MATCH CENTER


Cecafa Kagame Castle Cup 2011
Match No. 4, Sun June 26, 4pm
National Stadium [Dar es Salaam]
Young Africans [Tanzania v El Mereikh [Sudan]

YOUNG AFRICANS:
19. Yaw BERKO (Gk)
17. Godfrey TAITA
14. Oscar JOSHUA
24. Chacha MARWA
23. Nadir HAROUB (captain)
5. Nurdin BAKARI
18. Julius MROPE
16. Rashid GUMBO
28. Davies MWAPE
10. Jerry TEGETE
7. Kigi MAKASI
RESERVES:
30. Said MOHAMMED
13. Fred MBUNA
29. Juma SEIF
6. Godfrey BONNY
26. Kenneth ASAMOAH
COACH: Sam TIMBE [Uganda]
…….
EL MEREIKH:
01. Isam ELHADARI (Gk)
23. Saeed MUSTAFA (captain)
9. Badr ELDIN
7. Ahmed ALBASHA
18. Nasr ELDIN
12. Musab OMER
8. Kelechi OSUNWA
14. Balla GABIR
5. Wawa PASCAL
17. Karim EDDAFFI
19. Remi ADIKO
RESERVES:
21. Mohammed KAMAL
2. Nagm ELDIN
11. Ragei ABDELATI
10. Stephen WORGU
30. Mohammed MUGADM
4. Jonas SAKUMAHA
COACH: Husam AL BADR
MATCH UPDATE:
YANGA 2 1 EL MERREKH, MAGOLI YOTE WAMEJIFUNGA.

KUTOKA MOROGORO APR IMEPA BAO,HARUNA NIYONZIMA YUPO NDANI YA KIKOSI CHA APR AMEVAA JEZI NAMBA 8,

YANGA 2- 1 EL MERREIKH - HALF TIME

KIPINDI CHA PILI NDIO KINAANZA
DAKIKA 55:YANGA WANANSHAMBULIA VIZURI SANA KUPITIA PEMBENI HASA UPANDE WA KULIA ANAOCHEZA JULIUS MROPE,KWA UPANDE WA EL MERREKH WAMEONGEZA MCHEZAJI MWINGINE KWENYE KIUNGO,STEVEN WORGU ALIYEINGIA KIPINDI CHA PILI
DAKIKA 60: EL M,ERREKH WANAKOSA BAO LA WAZI

KUTOKA MOROGORO APR BADO INAONGOZA BAO 1-0 DHIDI YA PORTS YA DJIBOUT KIPINDI CHA PILI NDO KINAANZA.

EL MERREKH WAMESAWAZISHA BAO SASA 2:2

KUTOKA MOROGORO
DAKIKA 58: APR 3-0 PORTS

MUSAB OMAR WA ELBMEREIKH KAONYESHWA KADI YA NJANO.
NADIR HAROUB WA YANGA KAONYESHWA KADI YA NJANO.

KUTOKA MOROGORO
DAKIKA YA 85: APR 4: 0 PORTS

KUTOKA DAR ES SALAAM.

DAKIKA 90: YANGA 2:2 EL MERREIKH

KUTOKA MOROGORO:

FULL TIME: APR 4: 0 PORTS

DAKIKA 3 ZIMEONGEZWA MCHEZO KATI YA YANGA NA EL MERREIKH MATOKEO BADO 2:2

FULL TIME: YANGA 2:2 EL MERREIKH

Saturday, June 25, 2011

KAGAME CASTLE CUP: MATCH REPORT


MATCH REPORT: SIMBA VS VITAL'O - FIRST HALF

Vital'O waliuanza mchezo vizuri, wakitawala vilivyo mchezo ndani ya kipindi chote cha kwanza na wakitengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini kukosa umakini na umahiri Juma Kaseja walizipoteza nafasi hizo.Kwa upande wa Simba wakiwa wamewaanzisha wachezaji wao wapya mabeki Derrick Walulya na Saidi Nassoro Cholo, Ulimboka Mwakingwe, Haruna Moshi na Salum Machaku walionekana kukosa maelewano na hivyo kupelekea kushindwa kucheza vizuri ndani kipindi hiki ingawa wachezaji kama Ulimboka Mwakingwe, Boban na beki Said Nassoro Cholo walionekana kucheza vizuri.
Ndani ya kipindi kwanza Simba walicheza faulo 14, Mgosi akicheza 5, Boban 3, Cholo 1,Maftaa 3, Santo akacheza 2 na kupata kadi moja ya njano.
Vital'O walicheza faulo 8.
Kona- Simba 5, Vital'O - 1

SECOND HALF
Kipindi cha pili Simba waliuanza mchezo kwa kasi Boban,Machaku na Mwakingwe wakilisakama lango la Vital'O, lakini kutokana na kukosa umakini kwa mshambuliaji Mussa Hassan Mgosi aliyecheza chini kiwango Msimbazi walishindwa kupata bao.
Vital'O ndani second half walionekana kuchoka na kutokana Simba kuwashambulia sana walianza kucheza rafu zisizo na msingi hasa kwa Boban.
Waburundi hawa baada ya kipindi cha pili kuanza walifanya mabadiliko kwa kumtoa Stanley Minzi na kuingia Mbakiye Beby Miami, pia walimtoa Ndizeye Alain akaingia Garukwishika Jean.
Simba waliwatoa Salum Machaku, Banka, Mgosi na nafasi zao zilichukuliwa na Shija Mkina, Patrick Mafisango na Rajab Isiaka.
Kipindi cha pili Simba walicheza Faulo 4, huku Vital O wakicheza faulo 10 na kupata kadi 1 ya njano.

MAONI YA MAKOCHA
Mosses Bassena-"Timu yangu ilijitahidi kucheza vizuri na kumiliki mchezo kwa zaidi ya asilimia 70, na tumepoteza nafasi nyingi za kufunga hasa ndani ya kipindi cha pili lakini haikuwa siku yetu hasa kwa Mgosi ambaye leo hakuwa ndani ya kiwango chake.Tunajipanga kucheza vizuri katika michezo inayofuatia ili tuweze kufanikisha adhma yetu kubeba kombe hili."

YAOUNDE KANYANKOLE - VITAL'O COACH
"Nashukuru timu imepata sare dhidi ya timu kubwa kama Simba tena ukizingatia tulikuwa tunacheza mbele ya maelfu ya washabiki wa wapinzani wetu lakini vijana wangu wamejitahidi na tumefanikiwa kupata sare.Naamini tutajipanga na kupata ushindi katika mechi zijazo.Simba ni timu nzuri japo wanaonekana hawajazoeana lakini naamini wakikaa muda mrefu watakuwa na timu bora."

BOXING: FRANCIS CHEKA VS DANIEL WANYONYI

Bondia Francis Cheka amefanikiwa kumshinda Daniel Wanyonyi kwa pointi katika pambano ambalo lilikuwa zuri na la kusisimua.



21: 10- Matokeo ni Cheka ameshinda kwa pointi kutoka kwa majaji wawili
21:06 - Raundi ya 10 imeisha na mkenya alianguka tena, tunasubiri matokeo
21: 02 - Raundi ya mambo sio mazuri kwa mkenya, Cheka anashambulia vilivyo
20:59 - Raundi ya 8, wanashambuliana zamu kwa zamu na Cheka amefanikiwa kumwangusha mkenya , lakini anainyka na kuendela na mchezo
20:55 - Raundi ya 7 mkenya anaendeleza mashambulizi lakini cheka anajitahidi
20:50 - Raundi ya 6 mkenya amezinduka Cheka ameelemewa
20:44 - Raundi ya 5 imeisha Cheka ameendelea kufanya vizuri na mkenya anazidi kuvimba jicho
20:40 - Raundi ya 4 imeisha Cheka anaendelea kupafomu vizuri, mkenya amechanika anatokwa na damu.
20:35 - Raundi ya 3 Cheka anendelea na mashambul
20:32 - Raundi pili mkenya anajaribu kurudisha mashambulizi.
20:20 - Raundi kwanza imeisha Cheka amecheza vizuri sana
20:15 - Pambano linaanza
20:13 - Nyimbo za taifa zinapigwa na unaanza wimbo wa Tz.
20:12 - Mabondia wote wanaingia ulingoni, Cheka anashangiliwa sana.

KAGAME CASTLE CUP: LIVE MATCH CENTER


MATCH UPDATE: SIMBA VS VITAL' O
dakika 45 za kwanza zimemalizika matokeo 0:0 huku simba wakionekana kuelemewa kwenye sehemu ya kiungo na kupelekea mpaka wakati huu wa mapumziko wachezaji wake wanaocheza sehemu ya kiungo kucheza jumla ya faulo 14 huku musa mgosi peke yake akiwa amecheza jumla ya faulo 5, Vital'o wamefanikiwa kuingia kwenye eneo la hatari la simba mara 6 huku golikipa juma kaseja akiokoa magoli mawili,
salum machaku wa simba kapewa kadi ya njano.
dakika 45: subs Vital'o, stanley Minzi-out,mbakiye bebi -in
dakika 60: SImba, salum machaku -out,shija mkina-in
dakika 64: nzigamasabosteve-yellow card
dakika 67: simba-subs ,mohamed banka-out,patrick mafisango-in
dakika 69: golikipa wa Vital'o ameumia baada ya kugongana na Ulimboka mwakingwe lakini ananendelea na mchezo
wakati huo huo simba wanaishambulia sana Vital'o
dakika 72: simba ,musa mgosi-out,rajabu ishiaka -in
dakika 74: bado matokeo ni 0:0,ulimboka mwakingwe amecheza vizuri sana kwa upande wa simba mpaka sasa.
huku mshambuliaji aliyeingia kipindi cha pili wa Vital'o ,mbakiye beby akiwasumbua sana mabeki wa simba.
dakika 81: saidi nassor amepiga shuti lake la 3 katika mchezo wa leo lakini linatoka nje
dakika 82: aruna moshi amepiga shuti limetoka juu ya goli.
dakika 86: vital'o wamekosa bao,
dakika 90: dakika mbili zimeongezwa

fulltime: simba 0:0 Vital'o