Search This Blog

Tuesday, April 8, 2014

ROONEY KAMILI GADO KUWAVAA BAYERN, AWAPASHIA LEO ALLIANZ ARENA!!


All smiles: Wayne Rooney appeared in a relaxed mood as he joined his Manchester United team-mates on Tuesday
Tabasamu: Wayne Rooney ameonekana mwenye furaha akiwa mazoezini na wachezaji wenzake
Working hard: Rooney trains ahead of the crunch tie in Munich
Tayari kwa kazi: Rooney akijifua kujiandaa kuwakabili Bayern kesho
Wayne Rooney amewapa matumaini makubwa Manchester United kuelekea katika mchezo wa pili wa robo fainali kesho usiku,  ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Bayern Munich baada ya kufanya mazoezi leo hii katika dimba la  Allianz Arena.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Rooney alishindwa kuitumikia Man United ikishinda mabao 4-0 dhidi ya Newcastle kwasababu ya majeruhi ya mguu.
Katika mazoezi ya leo, Ryan Giggs alishiriki baada ya kuwakosa Newcastle, lakini Marouane Fellaini, aliyetolewa nje katika dimba la  St James' Park kufuatia kuumia, pamoja na  Rafael hawakushiriki.
Rooney ameonekana kutougulia maumivu katika mazoezi ya leo kwasababu alionesha juhudi kubwa.
Awali Kocha wa Man United, David Moyes alisema Rooney alikuwa hatarini kuukosa mchezo wa kesho baada ya kuumia katika mechi ya sare ya 1-1 Old Trafford wiki iliyopita, lakini kwasasa inaonekana kutoathirika tena.
Hata hivyo, nyota huyo mwenye miaka 28 atacheza mechi hiyo kubwa zaidi kwa United msimu huu akitumia dawa za kuua maumivu.
Na kocha wa Bayern  Pep Guardiola kwa upande wake hakuwa na wasiwasi kuwa Rooney ataikosa mechi ya kesho.
Alisema: 'Rooney anakwenda kucheza kwa asilimia 100. Atacheza, kama mtu anabisha naahidi kumpa zawadi kubwa endapo hatacheza"
Guardiola alimuelezea Rooney  kuwa ni mmoja kati ya wachezaji wakubwa aliowaona katika maisha yake ya soka.
Man United baada ya kuonesha kiwango kizuri katika mchezo wa kwanza, wanaonekana kuwa na imani ya kufanya kazi vizuri na kusonga mbele dhidi ya mabingwa hao watetezi.

No comments:

Post a Comment