Search This Blog

Tuesday, April 8, 2014

GUARDIOLA: BAYERN HATUJAFANYA MAZOEZI YA KUPIGA PENATI, SIDHANI KAMA TUTAFIKA HATUA HIYO!!


Spot on: Pep Guardiola, pictured at Tuesday's press conference, said his side have not prepared for penalties
Kazi ndogo tu: Pep Guardiola, amesema timu yake haijajiandaa kupiga penati kesho
Feeling the strain, Pep? The Munich boss oversaw his side's first defeat in 53 Bundesliga games on Saturday
Alipata maumivu?:  Kocha wa Bayern Munich alipokea maumivu ya kufungwa kwa mara ya kwanza bao 1-0 katika michezo 53 ya Bundesliga jumamosi dhidi ya Augsburg
................................................................
KOCHA wa Bayern Munich, Pep Guardiola amesisitiza kuwa klabu yake haijafanya mazoezi ya kupiga mikwaju ya penati kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya Manchester United.

Bayern wataingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya bao 1-1 na Man Unted dimba la Old Trafford, na kama matokeo kama hayo yatatokea kesho Allianz Arena, basi mikwaju ya penati itatumika kuamua mshindi.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kabla ya mchezo wa kesho, Gaurdiola amesema timu yake haijafanya maandalizi juu ya mazingira ya penati.

"Ni masuala ya mbinu tu na kujiamini. Yote yapo kichwani mwa wachezaji wangu". Alisema Gaurdiola.

Guardiola alisema Man Unted watacheza mpira wa kujihami na kushambulia kwa kushitukiza, lakini hadhani kama watafikia hatua ya penati.


   "Nadhani United watacheza zaidi nyuma. Watataka kucheza zaidi eneo lao na kujilinda". 
  "Timu za England zinaweza sana kujilinda na kushambulia kwa kushitukiza".
  "David Moyes atakuwa na wachezaji 8 mpaka 9 nyuma. Watakuwa wanasubiri tufanye makosa na watushambulie kwa kushitukiza".
  "Ndio maana nasema lazima tuwe na nidhamu kubwa. Tunacheza nyumbani na ni faida kwetu. Tunalazimika kushambulia vizuri" . Alisema Guardiola.

  Guardiola hana wasiwasi na Rooney ambaye anasumbuliwa na majeruhi kama ataweza kuamua matokeo ya Man United usiku wa kesho.

  1 comment:

  1. sa dauda mbona unatudanganya. hiyo picha ina nembo ya uefa champion, hafu iweje augulie maumivu ya kufungwa bundasliga.

   ReplyDelete