Search This Blog

Sunday, April 6, 2014

EXCLUSIVE: MENEJA WA JUMA KASEJA ATAKA USHAHIDI WA KUMUHUSISHA NA TUHUMA ZA KUUZA MECHI....


Siku chache baada ya gazeti ya gazeti moja la michezo kuripoti kwamba golikipa Juma Kaseja na beki Kelvin Yondani wametajwa kuchukua fedha kutoka kwa klabu ya Azam FC ili waifungishe timu yao kwenye mchezo waliopata kichapo dhidi ya Mgambo JKT - meneja wa kipa Juma Kaseja amezungumza na mtandao huu na kutoa ahadi ya kulipeleka gazeti hilo mahakamani.

Akizungumza na mtandao huu meneja wa Kaseja Abdulfatah Saleh alisema kwamba kwamba gazeti hilo limemchafulia jina na sifa mteja wake, na hivyo ameshauriana na Kaseja na sasa wamefikia maamuzi ya kwenda mahakamani kulishtaki gazeti kwa kuripoti story ya uongo dhidi ya kipa huyo ambaye alikaaa kwenye lango la Yanga kwenye mchezo dhidi ya Mgambo na wanajangwani wakafungwa mabao 2-1 hivyo kuuweka ubingwa wao rehani.

"Taarifa zilizochapishwa na gazeti la Championi si za kweli, zinaharibu sifa nzuri ya Kaseja aliyojijengea kwa miaka mingi. Pia limemuweka katika mazingira magumu ya kuitumikia timu yake. Tunakusudia kulipeleka suala hili mbele ya sheria mapema wiki ijayo. Champion itabidi watoe ushahidi wa taarifa yao dhidi ya mteja wangu," alisema meneja huyo wa Juma Kaseja.

4 comments:

 1. Rushwa ya soka ni pamoja na uzembe hivyo baada ya asante hiyo atapewa posho yake kwa kurahisisha kazi ya mbio za ubingwa jiulize mbona mechi ya mtani jembe ilikuwa poa yy meneja nawe shafii unaridhika na jibu eti ni khali ya kawaida ya mchezo? Uzembe na dharau ktk soka ni sumu golikipa ni sawa na askari mtegua mabomu akifanya uzembe anaangamiza kijiji tofauti na mshambuliaji hata akose magoli mia timu inakuwa salama

  ReplyDelete
 2. Kaseja hajawahi kuwa na mapenzi na Yanga, sijui walimchukua kwa ajili ya kuiuza yanga kwa team pinzani?
  Kuhusu lile kosa la Tanga lazima awajibishwe..ule sio uzembe amekula mlungula huyo...
  Nimeangalia video vizuri..
  Hata umlete nan akupe tafsiri ya ile video lazima atakwambia kuwa huyu mchezaji alikuwa na lake jambo..

  ReplyDelete
 3. Nyie nyote hapo juu ni wapumbavu tena wapumbavu hasa..mpira wa mapenzi uko mitaani kaseja mi profesional footballer hata kama hana mapenzi na yanga lakini yanga mdo waajiri wake...mnadhihilisha upumbavu wenu tena hvi kama yanga wangekua wanacheza mchezo mzuri wasingekua wanagombea vipoint viwili na azam..waangalieni b.munic wameshindaje ligi.kaseja kama kacheza game nyingi yanga azizidi tano so em sure sie aloifikisha yanga ilipo..sasa kama kaseja na yondan walifungisha mbana akina okwi mbele kule ealikua wanarukaruka..kabla canavoro ajafunga goli kwenye ile mech ya al ahly huu ujings mlilua mmenzushia yeye sa hzi naona mnawaamishia wengine.fyi.mpira wa kipumbavu wa mapenzi kama mnaoutaki hsuna mafasi tena.

  ReplyDelete
 4. HIVI HUWEZI KUCHANGIAQ MADA BILA KUTUKANA?MBONA WENZAKO WAMECHANGIA BILA MATUSI AU KWA SABABU WEWE NI SHABIKI WA MBUMBUMBU SC BASI LAZIMA UTUKANE ?

  ReplyDelete