Search This Blog

Sunday, March 30, 2014

MTWARA KUCHELE,NDANDA KWA ROHO SAFI !


Mwishoni mwa juma hili mkoani Mtwara mashabiki pamoja na wadau wa mchezo wa soka mkoani humo waliwapa mapokezi makubwa wachezaji pamoja na viongozi wa timu ya Ndanda FC iliyopanda ligi kuu ya Vodacom kwa msimu ujao.
Ilikuwa ni mishale ya saa tisa kamili alasiri siku ya ijumaa wakati ndege ya shirika la ndege la Tanzania iliposhuka mkoani hapo ikiwa imewabeba wachezaji pamoja na viongozi wa timu hiyo,walikutana na viongozi mbali mbali wa serikali mkoani humo,wakuu wa wilaya na viongozi wa vyama vya soka vya wilaya kwa  pamoja na viongozi wa chama cha soka cha mkoa wa Mtwara wakiwasubilia kwa hamu kubwa.

Wakati msafara wa wachezaji na viongozi wa Ndanda walipokuwa kwenye uwanja wa ndege wa mwalimu Nyerere.
Wakipanda Ndege kuelekea mkoani Mtwara....
Wakipanda Ndege kuelekea mkoani Mtwara....
Wananchi wa mkoa wa Mtwara wakiwa wamejipanga barabarani kuipokea timu ya Ndanda FC.

Nyomi kwenye uwanja wa Nang'wanda


Kocha wa Ndanda FC Dennis Kitambi akivishwa taji la maua na mgeni wa heshima..
Mwenyekiti wa chama cha soka Mkoani Mtwara,Athumani Kambi mwenye jezi nyeupe ya NDANDA FC akisimamia shughuli za kuipokea na kuipongeza timu ya NDANDA.

Mwenyekiti wa NDANDA FC Ndugu Ahmed Omar akivishwa taji la maua na mwakilishi wa mkuu wa Mkoa ambaye alikuwa ndiye mgeni wa heshima.

No comments:

Post a Comment