Search This Blog

Tuesday, April 1, 2014

JKT RUVU WAWATISHIA YANGA YA MGAMBO JKT, MINZIRO ATAMBA KUWASHANGAZA WENGI TAIFA!!

Na Baraka Mpenja , Dar es sakaam

Maafande wa JKT Ruvu wamesema kwasasa malengo yao makubwa ni kusalia ligi kuu soka Tanzania bara baada ya kufanikiwa kuwafumua Rhino Rangers mabao 3-1 wikiendi ya wiki iliyopita uwanja wa Azam Complex, uliopo Chamazi, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

Kocha mkuu wa klabu hiyo, Fredy Felix Minziro ameuambia mtandao huu kuwa sasa nguvu zao wanaelekeza katika mechi tatu zilizosalia kuhakikisha wanavuna pointi sita na kubakika ligi kuu.

“Mchezo uliopita ulikuwa mgumu kwasababu timu ya Rhino bado ilikuwa inapambana isishuke daraja, nadhani sasa wameshuka rasmi. Kama nilivyosema malengo yetu ni kuhakikisha timu inabakia. Tuna imani katika michezo iliyobaki tutafanya vizuri”. Alisema Minziro.

Minziro aliyekuwa kocha msaidizi wa Yanga mzunguko wa kwanza msimu huu akiwa chini ya kocha mkuu, Mholanzi, Erne Brandts aliyetimuliwa pamoja naye, aliongeza kuwa wanakabiliwa na changamoto kubwa katika mechi ijayoaprili 6 mwaka huu dhidi ya Yanga sc,  kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

“Mechi hii itakuwa ngumu zaidi kwetu kwasababa Yanga wataingia kwa machungu ya kufungwa na Mgambo JKT na kujiweka katika mazingira magumu ya kutetea ubingwa wao”.

“Lakini mpira unachezwa uwanjani, hatutaingia kinyonge bali tutapambana dakika zote kuhakikisha tunapata matokeo mazuri
 JKT Ruvu wapo nafasi ya 9 katika msimamo baada ya  kushuka dimbani mara 23 na kujikusanyia pointi 28.

Hata hivyo wanaonekana kuwa mazingira mazuri ya kubakia endapo wataweza kuchanga vizuri karaka zao mechi tatu zilizosalia.

Wamebakiza mechi  dhidi ya Yanga uwanja wa Taifa, Coastal Union uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga, na kipute cha mwisho watavaana na vinara Azam fc uwanja wa Azam Complex.

Katika mechi hizo tatu, michezo miwili dhidi ya Yanga na Azam fc itakuwa mtihani mkubwa kwa kocha Minziro, kwasababu timu hizo zinapigana kwa nguvu zote kutwaa ubingwa.

Yanga wenye pointi 46 wapo katika `presha` kubwa kufuatia kuachwa kwa pointi saba na Azam fc waliopo kileleni kwa pointi 53.

Mechi ijayo wataingia kwa malengo ya kushinda, lakini lazima wawe na tahadhari ili kutokumbana na mambo ya Mgambo JKT  kule Tanga, `waja leo waondoka leo`.

No comments:

Post a Comment