Search This Blog

Tuesday, February 11, 2014

NILING'OKA MENO KWASABABU YA NDONDO- KIPANYA MALAPA

 Kutoka kushoto ni orodha ya waliokuwa wacheza NDONDO maarufu: Shaffih Dauda,Gula Joshua,Kipanya Malapa,Jemedari Said na James Chirwa


 Mshambuliaji wa zamanai wa vilabu vya Blackpool na Black Six za Ving'ung'uti,Ashanti ya Ilala,Singida UTD na Yanga Kipanya Malapa amesema mashindano ya mitaani maarufu kama 'NDONDO' yalimpekea hadi kung'oka meno.
 Mmoja wa wanasoka maarufu wa kucheza NDONDO alikuwa ni Marehemu Omari Changa 'Mapung'o'.


'Ndondo zilikuwa hazilipi na moja ya athari zake ni kuniachia mapengo',Enzi zetu tulikuwa tunacheza bila mikataba ndio maana tulikuwa tunacheza sana ndondo,siku sababu ya wachezaji kucheza ndondo kwasababu wanalipwa mishahara hadi kufikia 500,000'.
Kipanya pia hakuacha kuwataja wacheza ndondo maarufu aliokuwa anakutana nao viwanjani,miongoni mwa wachezaji aliwataja ni Mshambuliaji Omary Changa aliyefariki hivi karibuni,wengine aliowataja kwenye orodha yake ni Juma Kisungura,Edward Kayoza na Omary Bunju.

No comments:

Post a Comment