Search This Blog

Tuesday, February 11, 2014

NIONAVYO MIMI:SWANSEA CITY IMEPOTEZA "USWANSELONA" WAKE

Na Oscar Oscar Jr
0789-784858
Barcelona ni timu maarufu sana kwa kucheza "Tick-Taka style",mchezaji wake akiwa anamiliki mpira,wenzie wawili wanasogea kuomba pasi na wanapopoteza ,wanaondoka watatu kwa pamoja kama nyuki kwenda kuutafuta kwa mpinzani.

Swansea city walikuwa wameimasta style hii. Arsenal amepata shida sana mbele ya Barcelona na Swansea city timu ambazo inaaminika zina falsafa moja ya mpira ingawa wachezaji wake wana ubora tofauti.Unajua kwa nini? Arsenal anafanana na hao wawili anapokuwa anamiliki mpira tu,anapopoteza arsenal hakabi vizuri kama hao wenzie.

Swansea city ni timu ambayo ilikuwa inamiliki mpira kuliko kawaida na kupata ubingwa wa Capital one Cup kwa kumchapa Chelsea kwenye nusu fainali 2-0 pale "Daraja la Mtera" Stanfford Bridge na kufanikiwa kutoa Sare kule Liberty stadium,huku Hazard akimaliza hasira zake kwa kumtia mateke ball boy wa swansea city.

kwa nini wamepotea msimu huu? Kumkosa mchezaji wao bora wa Klabu wa mwaka jana MICHU ni pigo kwenye kikosi chao.Michu alifunga goli 18 za EPL msimu uliopita na mabao yake mengi sana yaliwapatia point 3 kwenye timu.Ukitaka kujua hili,waulize arsenal pale emirates msimu uliopita watakupa jibu.

Kwa sasa wanamtumia Wilfred Bonny,ni kweli anafunga sana lakini magoli yake mengi hayawapi point yoyote Swansea.Bonny alifunga dhidi united na matokeo yakawa 4-1 kwa united kuibuka na ushindi,alifunga mabao mawili dhidi ya man city na matokeo wao ndo wakalala kwa mabao 3-2,alifunga dhidi ya Spurs na wakalala 3-1 n.k ingawa lazima pia nimpe credit kwa bao lake maridadi lililowaondoa man united kwenye FA CUP pale Shamba la bibi Old Trafford.

Swansea city kwa sasa wanapumulia mipira na ubora wa uchezaji wao umepotea,naamini kurudi kwa Jonathan De Guzman,Nathan Dyer na Michu kunaweza kuwarejeshea tena makali yao.Kukosekana kwa hao watu,naamini ni moja ya wao kuyumba lakini pia kuuzwa kwa Scott Sincair,Graham na mkopo wa Ki Sung umewaathiri.

Swansea wanashiriki michuano ya Europa League na kwa mujibu wa historia inaonyesha kwamba timu za Uingereza huwa hazifanyi vizuri kwenye ligi pindi zinaposhiriki Michuano ya Europa.Wanalazimika kusafiri na kucheza mara mbili kwa wiki,kwa udogo wa kikosi chao,wachezaji wanachoka sana.

Liverpool alishiriki Europa League,akamaliza wa 7 kwenye Ligi,Stoke city aliwahi maliza wa 14,Newcastle mwaka jana alimaliza wa 16,Fulham waliwahi kumaliza wa 12.Ni man city tu ndo wamewahi kushiriki Europa na kufanikiwa kucheza UCL msimu uliofata.

Europa kwenyewe kuna kina Juventus,Napoli n.k sidhani kama mambo yatakuwa mazuri huko ingawa kwenye soka hakuna kinachoshindikana.Kama waliweza kumpiga Vallencia kule Spain,lolote linawezekana.Sina hakina kama watarudia tena Uswanselona wao but namtakia mema kocha wao wa muda Garry Monk ambaye ameanza kwa ushindi kwenye mechi ya dhidi ya Cardiff city na nitammiss sana kocha Michael Laudrap aliyetimuliwa hivi karibuni..

No comments:

Post a Comment