Search This Blog

Tuesday, February 11, 2014

ANGALIA NAMNA ASKARI MAGEREZA ALIVYOKAMATWA NA TIKETI BANDIA...




Mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Tukuyu Stars na Prisons vya Mbeya John Joseph amekamatwa na jeshi la polisi mkoani Mbeya akiuza tiketi bandia kwenye mchezo wa Mbeya City na Mtibwa Sugar.

John Joseph ambaye kwasasa ni askari wa jeshi la Magereza mkoani humo,alikamatwa na tiketi tano bandia akiziuza nje ya uwanja wa Sokoine.

Akiongea hapo jana usiku kwenye  kipindi cha SPORTS BAR cha Clouds TV kinachoruka kila ya Jumatatu, kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya ndugu Ahmed Msangi alithibitisha kukamatwa kwa askali huyo na kusema uchunguzi ukikamilika atapelekwa mahakamani.


 Hapa John Joseph akiwa ameshikiliwa na polisi.
 Tiketi halali.....imeiva....
Hii ilikuwa tiketi feki......imepauka




No comments:

Post a Comment