Search This Blog

Tuesday, February 11, 2014

WASHINDI KILI MARATHON KUNYAKUA ZAIDI YA SH MILIONI 40

Zawadi za fedha taslimu kwa washindi wa Kilimanjaro Marathon 2014 zimeongezwa hadi zaidi ya shilingi milioni 40 na kuifanya mbio hii kuwa kati ya m io kubwa zaidi barani Afrika.

Waandaaji wa mbio hizo wametangaza kuwa washindi wa wa Kilimanjaro Marathon 2014 watajipatia zaidi ya shilingi milioni 40 fedha taslimu kama zawadi.

John Addison, Mkurugenzi Mkuu wa Wild Frontiers, waandaaji wa mbio hizo alisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana kuwa mbali na washindi kujinyakulia zaidi ya shilingi milioni 40 pia watapata fursa ya kujishindia zawadi nyingine kabambe za kuvutia kutoka wadhamini wakuu Kilimanjaro Premium Lager kwa kushirikiana na wadhamini shirikishi
Alisema washindi wa mbio ndefu za marathon ya kilomita 42 watajishindia jumla ya shilingi milioni 20, na zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni 10 kwa washindi wa nusu marathon huku washindi wa mbio za walemavu maarufu kama GAPCO 10km Marathon wakijishindia kiasi cha shilingi milioni 6. Washiriki wote watakaomaliza mbio za kujifurahisha za Vodacom 5km Fun Run wataweza kujishindia zawadi mbalimbali.

Addison alisema kuwa mbio za mwaka huu zimesheheeni motisha mbalimbali za kuvutia ili kuongeza idadi ya washiriki. Washindi wa kwanza kwenye mbio ndefu za kilomita 42 (Kilimanjaro Premium Lager Marathon) wanawake kwa wanaume watajinyakulia kiasi cha shilingi milioni 4 kila mmoja, shilingi milioni mbili kwa washindi wa pili na shilingi milioni 1 kwa washindi wa tatu. Washindi wa kwanza kwenye mbio ndefu za  nusu marathon (km 21) wanawake kwa wanaume watajinyakulia kiasi cha shilingi milioni 2 kila mmoja, shilingi milioni 1 kwa washindi wa pili na shilingi 500,000 kwa washindi wa tatu.

Addison aliongeza kuwa medali na t-shirt zitatolewa kwa wanariadha 500 wa kwanza kumaliza mbio za kilomita 42, wanariadha 2,200 wa kwanza kumaliza mbio za nusu marathon na wanariadha 80 wa kwanza kumaliza mbio za walemavu.  Washiriki 3,000 wa kwanza kumaliza mbio za kujifurahisha za Vodacom 5km Fun Run watapewa t-shirts baada ya kumaliza mbio na watapata fursa ya kujishindia zawadi mbalimbali za kuvutia kupitia droo.

Ili kuwapa hamasa wanariadha wa Tanzania kufanya vizuri katika mbio hizi, Kilimanjaro Premium Lager imetenga kiasi cha shilingi milioni 2 bama bonsai kwa wanariadha Watanzania watakaovunja rekodi katika mbio hizi.

Mbio hizi zinaratibiwa na kwa kushirikiana na Riadha Tanzania, Chama cha Riadha Mkoa wa Kilimanjaro na Kilimanjaro Marathon Club huku zikidhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, Vodacom Tanzania, GAPCO, Simba Cement, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, TanzaniteOne, CMC Automobiles Ltd, Kibo Palace Hotel, RwandAir, FNB Tanzania, UNFPA na Kilimanjaro Water.

No comments:

Post a Comment