Search This Blog

Monday, February 17, 2014

NI MUHIMU YANGA KUYAFAHAMU HAYA KABLA YA KUMCHEZESHA OKWI.



Stori iliyoongoza kwa vichwa vya habari za michezo mwishoni mwa juma lililopita ilikuwa inamuhusu mshambuliaji Emmanuel Okwi.
Kilichopelea gumzo la mchezaji huyo ilikuwa ni baada ya FIFA kuiandikia barua TFF na kuitaarifu ya kwamba mchakato wa uhamisho wa Okwi toka SC Villa kwenda Yanga ulikuwa hauna tatizo. Lakini pamoja na kutoa taarifa hiyo FIFA bado ilisema yenyewe haina mamlaka ya kumruhusu mchezaji kuichezea klabu yake hiyo mpya zaidi ya kuiagiza TFF kufuatilia wenyewe taratibu za uhamisho wa mchezaji huyo kama zipo sahihi.



Sasa hapo kwenye kufuatilia taratibu za uhamisho wa mchezaji huyo ndipo kulileta utata,kutokana na angalizo hilo la FIFA iliulazimu mtandao huu kufuatilia kwa kina kuweza kujiridhisha na mahusiano yaliyopo hivi sasa kati ya Okwi na klabu ya Etoile Du Sahel iliyomnunua toka klabu ya Simba.

Baada ya kufanya mahojiano ya Raisi wa Etoile ndugu Ridha Charfeddine aliuhakikishia mtandao huu ya kwamba bado wana mkataba na mchezaji huyo ambao unakwisha mwezi june mwaka 2016.



Ni vizuri Yanga wakajiridhisha na haya kabla ya kumchezesha mchezaji husika.


                       Barua ya Etoile du Sahel waliyomwandikia Okwi wakimsihi arejee klabuni...


USAJILI



 FIFA inasisitiza mchezaji kusajiliwa na timu moja tu ya soka kwa wakati mmoja, pia FIFA inasema wachezaji wanaruhusiwa kusajiliwa na klabu zisizozidi tatu kwa msimu mmoja. Kwa kipindi hicho mchezaji ataruhusiwa kuchezea timu zisizozidi mbili tu katika mechi rasmi. Kuna mwiko mmoja tu ambao unaruhusiwa kuvunjwa katika sheria hii, na huu ni pale ambapo mchezaji atakua amehama kati ya vilabu viwili ambavyo vinashiriki katika ligi zenye misimu inayofuatana.

Kwa mfano kama mchezaji kahama toka kwenye timu inayoshiriki ligi inayoisha katika mwezi wa tisa kwenda katika timu inayoshiriki ligi inayoanza mwezi wa kwanza, huyu ataruhusiwa kuchezea timu nyingine ya pili katika ligi mpya aliyohamia ili mradi awe ametimiza masharti ya mkataba wake na timu zake zote alizotoka na amezingatia sheria za usajili za chama cha soka cha nchi yake ikiwa ni pamoja na FIFA.



Maswali ya kujiuliza

1.     Timu ipi kati ya Etoile na Yanga inammiliki mchezaji huyu wakati timu zote zimemsajili mpaka sasa wakati FIFA wanasisitiza mchezaji kusajiliwa na klabu moja tu kwa wakati mmoja,

2.       kama FIFA wanasema mchezaji ataruhusiwa kuchezea timu nyingine ya pili katika ligi mpya aliyohamia ili mradi awe ametimiza masharti ya mkataba wake na timu zake zote alizotoka. Je Okwi ametimiza masharti na Etoile moja ya timu alizotoka ?



      Kuvunja mkataba



Mkataba baina ya mchezaji wa kulipwa na klabu utaisha pale tu ambapo muda wa mkataba utafikia mwisho wake au mkataba kuvunjwa kwa makuballiano ya pande zote mbili lakini pia mkataba unaweza kuvunjwa na pande yoyote ile bila ya kuwa na vipingamizi ama adhabu pale tu ambapo kutakua na sababu ya muhimu inayotambulika kisheria.



Madhara ya kuvunja mkataba bila sababu maalum.



1. Mara zote upande unaovunja mkataba ndio unatakiwa kulipa gharama za uvunjaji mkataba.Gharama zinazohusika kulipwa ni zile zinazohusu mafunzo na kiwango huwa kinahesabiwa kutokana sheria za nchi,klabu na chama cha nchi husika.Gharama nyingine husika ni pamoja na madeni ya ada za uhamisho,mshahara wa mchezaji na marupurupu mengineyo.



2. Jukumu la ulipaji lazima libebwe na mchezaji ama akishirikiana na timu anayohamia.



3. Ushindwaji wa kulipa gharama hizi utasababishwa kutolewa kwa adhabu ya kufungiwa kucheza miezi minne ama miezi sita kutokana na uzito wa kosa. Adhabu hizi zitaanza kutumikiwa mara baada ya mchezaji husika kupewa taarifa rasmi. Adhabu hizi pia zitasimamishwa kuanzia mwisho wa msimu hadi mwanzo wa msimu mwingine ndipo zitakapoanza tena. Ingawa adhabu hizi huruhusiwa kuendelea kama mchezaji husika ni mmojawapo wa wachezaji katika timu ya taifa inayoshiriki fainali za mashindano yanayotambulika na FIFA.



4. Kwa ziada ya kulipa fidia  baada ya kuvunja mkataba,adhabu za ziada zitatolewa kwa klabu ambayo itapatikana na hatia ya kutumia mbinu zisizo halali za kuchochea uvunjaji wa mkataba kabla ya kipindi kinachoruhusiwa. Klabu hiyo itafungiwa kusajili mchezaji yoyote kwa kipindi kisichopungua madirisha mawili ya usajili.



VIPENGELE MAALUM KUHUSU MIKATABA YA WACHEZAJI NA VILABU



Klabu nyingine yoyote yenye nia ya kuvunja mkataba wa mchezaji na klabu yake ya wakati huo italazimika kuifahamisha klabu ya mchezaji huyo kwa maandishi kabla ya kuanza mazungumzo na mchezaji. Mchezaji wa kulipwa ataruhusiwa tu kuanza mazungumzo na klabu nyingine ikiwa mkataba wake umeisha ama unatarajiwa kuisha ndani ya miezi sita.


  Hii ni sehemu ya barua ya FIFA waliyoiandikia TFF... Interview ya Rais wa Etoile

26 comments:

  1. mbona unatumia nguvu nyingi sana shafiii na maestro ushabiki wa nini bhana

    ReplyDelete
  2. Kuvunja Mkataba wowote ule : "Iwapo pande mojawapo au pande zote hazitatimiza masharti/consideration za mkataba" umesahau au umeacha makusudi kwa sababu unazozijuwa wewe.

    FIFA ilitoa maamuzi ya kwamba OKWI acheze ili asipoteze kipaji chake kwa kuwa ilionekana hakuna maelewano kati yake na Etoile. Ili OKwi acheze Villa, lazima status yake ya Mkataba wake na Etoile ipbadilike na TMS ikubali (Match). Ninavyoona mie kuwa FIFA ili nulfy contract na kumfanya OKWI ni free agent na hapo sasa akasajiliwa na Villa kwa miezi sita na status hiyo ndiyo yanga wameitumia kumsajili na kupata ITC.

    Kama FIFA watataka kubadili tena itabidi Warudishe Status ya OKWI ni mali ya Etoile sijui watafanyaje kwenye hiyo system. Ndio maana naona Mawazo yako Shafii kwa kutaka kuthibitisha uko sahihi yamelalia upande mmoja. FIFA wamesema Kesi zilizopo haziusiani na USAJILI bali ni za Madai. Kwa hiyo zikiamuliwa ni masuala ya compensation tu ndio yatafuata.

    Alafu tumewasikia Jana mkifanya kipindi pasipo ueledi kwa kuuliza maoni Panelist kwa kutumia closed question (Yaani Ndi au Hapana) bila kuruhusu hoja za wajumbe zitoke hewani na sisi wasikilizaji tuchambue tuone Clouds mlikosea vipi au mpo sahihi. Nilishangaa sana Mnatafuta mlango wa kutokea lakini mnajifunga wenyewe na mnatapa tapa, Come cleans kama mmoja wenu ameegemea upande na kutoa Comclusive statements aombe radhi yaishe tu lakini si jinsi mfanyavyo.

    IDD GODEGODE alikua na hoja akitaka kuzitoa mnamkata, mnaongea na mtu wa Etoile na maswali hayo hayo mnayotaka kuthibitisha kuwa Okwi bado anamkataba na Etoile, mngewaachia na akina IDD nao waulize au mnge probe more.

    Hiyo Analysis yako Shafi Ungeiacha iwe neutral na Pia unavyotaka wewe OKWI arudi Tunisia ambako yeye hataki kufanya kazi na Muajiajili asiyempa ujila wake. Kwa namna hiyo OKWI ataua kipaji chake mpaka June 2016, Rules zinasema, kama kuna dispute basi decision huwa inaegemea kwa Weaker part, Lazima mpira uchezwe na OKWI acheze, hapo ndio naona FIFA haiwezi kumzuia OKWI asicheze

    Hongera kwa kuijali Yanga kwani unataka wasipokwe point Linalotokea kwa Viongezi wa Vilabu vyetu ndilo hilo linataka kumtokea Kapombe tena.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hakuna kitu kama hico kaka, mkataba unavunjwa na wahusika wote sio kama mnavyo ambiwa na viongozi wa yanga, na kama umesikia na kuisoma barua hakuna kipengele cha Okwi kuvunja mkataba zai ya TFF kusema kuna uhamisho kudumu kutoka Simba kwenda Etoile na uhamisho wa muda wa miezi sita kwenda Villa hayo ya kuvunjwa mkataba mmeyatoa wapi? tujuavyo mkataba ulitakiwa uvunjwe na Etoile wakishilikiana na okwi mbona Etoile wanasema Okwi ni mchezaji wao? Majanga hayoooooooooooooo

      Delete
    2. Nenda kaangalie statutory inayohusu mikataba. Sio polojo. Zingatia ili mkae meza moja lazima muelewane lakini kama mmeshindwana then mmoja kati yenu anaweza ku sue the contract kwa kua address non performance of consideration of the party to the contract. Pale panapotokea kila mmoja anadai lake then sheria inachukua mkondo wake.

      Delete
  3. Shaffih sawa nakupongeza kwa kusikiliza maoni ya wadau ya balance story, lakini kitu kimoja toka kwangu, 'Mbona hiyo barua ya FIFA kwa TFF umeikata? kwa nini hukuionyesha yote? Hujui neno moja ambalo pengine hukulionyesha lingeleta maana ya ziada.

    ReplyDelete
  4. Shaffih kuna maneno unayatumia sijui ni kwa makusudi ama vp? ambayo yanatoa tafsiri potofu. kwa mfano unasema FIFA imeagiza TFF nakunukuu: "Kilichopelea gumzo la mchezaji huyo ilikuwa ni baada ya FIFA kuiandikia barua TFF na kuitaarifu ya kwamba mchakato wa uhamisho wa Okwi toka SC Villa kwenda Yanga ulikuwa hauna tatizo. Lakini pamoja na kutoa taarifa hiyo FIFA bado ilisema yenyewe haina mamlaka ya kumruhusu mchezaji kuichezea klabu yake hiyo mpya zaidi ya kuiagiza TFF kufuatilia wenyewe taratibu za uhamisho wa mchezaji huyo kama zipo sahihi" Ilichowaagiza TFF siyo kufuatilia taarifa za uhamisho wa mchezaji huyo kama zipo sahihi! bali TFF iangalie taratibu zake za NDANI kama zimefuatwa. FIFA siyo chombo ujanja ujanja Shaffih!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hapo hata mimi nimepaona, Jamaa anatafasiri jinsi yeye fikra zake zinapomuelekeza. TARATIBU ZA NDANI YA SHIRIKISHO KAMA ZIMEFUATA.

      Delete
  5. God! huyu Shaffih nimegundua tatizo lake ni Communication skills(kimombo) mbona hiyo kipande aliyoweka hapo inaeleweka kwa uwazi kabisa! shabash!!!!!!!!!! Shaffih pole mdogo wangu next time weka hivi vitu hapa halafu tukueleweshe kwanza kabla hujaweka upupu wako!!!
    Hata interview zako zingekupa mwongozo. logging out!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  6. Lakini Shafii dauda kajuna si alishapewa ONYO na Kamati ya Rufaa ya Maadili ya TFF kwa kuweka kwenye blog yake nakala ya barua ya FIFA kwa TFF huku yeye akiwa hajanakiliwa barua hiyo?Hata kama alipata msamaha feki na wa kinyume cha katiba ya TFF toka kwa swahiba wake Malinzi lakini alipaswa kuheshimu ONYO hilo kwani msamaha huo feki wa Malinzi ulimfutia adhabu tu na siyo hatia ya kosa hilo aliyopatikana nayo.Hivi sasa yuko kwenye kamati za TFF na anarudia kosa lilelile ambalo alitiwa hatiani na hakuwahi kulikatia rufaa na kujiondoa hatiani..Labda anfanya hivyo kwa sababu tu yuko karibu na Malinzi na TFF imekaa kimya tu

    ReplyDelete
  7. Hao Simba sc waache kufuatilia usajili wa Okwi Yanga kwa kuwa hauwahusu na kule FIFA hakuna kesi inayohusu Etoile kumshataki Okwi bali ipo kesi ya Simba kuidai Etoile fedha za mauzo ya OkwiHivyo Simba wanatakiwa kudai fedha zao na wakishazipata wakumbuke kuwalipa Villa asilimia 20 ya mauzo hayo kwa kuwa ndio waliomlea na kumfundisha mpira Okwi akiwa chini ya miaka 18

    ReplyDelete
  8. Ukweli tutaupata tu bado kidogo, Uhuni wa usajiri Tanzania umezidi soma hapo chini niambie taratibu zikoje na kwanini TFF wanajifanya hawajui ile hali wanahusika?

    Sheria zinasema ili kufanikisha usajiri lazima vilabu viwili na vyama wanachama wote kwa pamoja waweke maelezo sahihi, Tff wanashindwa nini kusema ukweli kuhusu hilo? kazi ya vyama wanachama ni kueleza kuhusu taarifa za ligi zao na mambo mengine yaliyoko hapo chini, je Yanga waliwezaje kujaza kila kitu bila TFF kuwepo?


    To which type of transfers does it apply?
    The system is designed to regulate the international transfers of male professional footballers and does not cover so-called “domestic” transfers, i.e. those between clubs of the same association . It may be extended at a later date, however. Nor does the TMS apply to transfers of players who retain their amateur status when moving between clubs, although the transfer of a player from amateur to professional status must be registered in accordance with the system.

    Who is responsible for entering the information on the system?
    In order for a transfer to be validated the two clubs involved must enter the relevant information on the deal. Member associations must keep all information relating to the league season in question up to date, as well as information on player registrations, clubs and agents.

    What information has to be provided?
    The following information must be given: The names of the clubs, the member associations, player details (date of birth, nationality, first last and middle names) , type of transfer (permanent, loan, exchange), possible commission payments, the total transfer fee, details of any training compensation or solidarity contributions, payment deadlines (of which there may be one or more), the payment schedule (including dates, amounts paid and recipients), details of payments already made (including information on the paying bank, the payee bank, the amount paid, the date of payment and the recipient).

    What other guarantees need to be provided?
    As well as the information above, clubs and associations are required to upload a series of documents in the system. These are as follows: documents providing proof of the nationality, correct spelling of name and age of the player; a copy of the player’s new contract of employment, a copy of the transfer agreement and proof of payments.

    How will the system increase transparency?
    The fact that fraud is very difficult to carry out online guarantees transparency. Clubs and their member associations are responsible for the information they enter on the system and for the actions that need to be undertaken. Prior to forwarding information, clubs are required to tick a box confirming that no third parties are involved in the transaction. Each club and association has their own system account and this allows the TMS teams to view the information they provide immediately, enabling them to identify each party involved along with any irregularities.

    How will the TMS monitor information?
    The TMS has a dedicated compliance and monitoring team plus a number of additional tools that oversee each transfer.

    What happens if a transfer is not completed in the correct manner?
    The TMS comes into effect on 1 October. Clubs and associations failing to apply the system after that date may be subject to a wide range of penalties imposed by FIFA’s Disciplinary Committee in accordance with the seriousness of the violation. These penalties are as follows: An official warning, a fine, exclusion from a competition, the withholding of a trophy or award, the annulment of match results, match forfeiture, a points deduction, demotion to a lower division and a transfer ban.

    ReplyDelete
  9. Shaffih hao wanaokuona kama unachochea baada ya siku watakuja kukukubali tu hayo maneno yako maana yanga wameshazoea kufanya mambo kienyeji kienyeji kwa kutegemea kubebwa hapa mwendo wa sheria tu kufuata

    ReplyDelete
  10. Halafu hao waarabu mbona kama matapeli tuu. Hela ya Simba wanasumbua kulipa. Ni wajanja sana kwenye kuongea. Lakini kulipa hawalipi. Hata Okwi inawezekana hawjamlipa.

    ReplyDelete
  11. we Dauda ndo mana hatas mashabiki wa yanga wanakuchukia,coz unaleta ushabiki sometimes then unapublish vi2 ambavyusan katika swala la michezo na impacts zakoo huna uhakika navyo bila kujua nafas yako katika jamii hususan kimichezo, ulijijengea heshima sna bt ths tme heshma yako imeshuka afu unaonekana unaongea vi2 kiushabik sna

    ReplyDelete
    Replies
    1. Msameheni ni bei ya mkaaaaa tuuuuu! shafiii wewe ni booooongeeeee la mwandishi upo juuuu unatishaaaaa kaza mwambie maestro akusaidie, tutakuchagua aseeee uwe mjumbe wa kujitegemea

      Delete
  12. Nashindwa kuelewa hivi hizi comments na maangalizo yote haya waachieni Yanga wenyewe wao ndo watapata faida au hasara; hali ya kujifanya mnaitahadharisha Yanga ni ya kinafiki na uzandiki tu.

    ReplyDelete
  13. Dauda.....hiyo notice ya hao warabu nayo mbona magumashi tu...notice haina hata tarehe,haijulikani imeandikwa lini na ni notice ya mudagani!!
    Kama ni formal notice kama unavyodai it supose to state a time frame given to the player......otherwise that does not qualify to be a notice!!!!

    ReplyDelete
  14. Shaffih please naamini we ni mwandishi mzuri wa michezo. You need to kill the issue by analyzing all parts involved. You just talk to Etoile leaders and conclude the matter while its actually incomplete. Naamini Yanga walimnnunua Okwi kutoka Sport Villa Ug. Then ongea na viongozi wa Sport Villa wao wana sema nini kuhusu hii issue? Na walimuuzaje Okwi kwenda Yanga wakati alikuwa still bado anamkataba na hao watunisia ?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Abdul umesema kweli maana mwandishi mwenye ueledi wa kutosha hawezi ku conclude issue bila kushirikisha pande zote zinazohusika.Shaffih angewatafuta SC Villa kujua ni criteria gani walizitumia mpaka kumuuza Okwi kwenda yanga?Na pia Okwi ana agent wake na mwanasheria wake.Pia Maestro ni kiongozi wa simba sasa tutajuaje hayo yote anayoyatafuta hayana mkono wa simba sc?Mimi naona uchambuzi wao umejaa ushabiki zaidi.Kwa kifupi uchambuzi wa maestro una mgomgano wa kimaslahi.

      Delete
  15. "alikuwa still bado anamkataba"

    ReplyDelete
  16. kaka anza kufuatilia kwanza fedha za simba zipatikane, hiyo ndio inakuhusu zaidi acha yanga waendelee na yao. Au ingekuwa bora uanzishe stori mpya ya kapombe. Au ukishindwa wapelekee yanga maombi ya kuwa mshauri wao wa kuua timu. Vipi safari hii hukupata mapema jina la kocha mpya wa yanga ili umwambie asije bongo. Duuu blog hii inaongoza kwa fitna na uzandiki

    ReplyDelete
  17. I CAN SEE SO MANY BUSH LAWYERS IN THIS SAGA......

    ReplyDelete
  18. Wewe jamaa nimekudharau sana, sijui hata kama unapata singizi usiku, naona kila siku unamuota Okwi! Pole sana, naona wewe ndiyo msemaji wa Etoile kila simu unapiga simu, eti bado mchezaji wao, ingia web site ya Etoile uone ktk list ya wachezaji kama kuna jina la Okwi,kama bado wao inamaana jina la Okwi liko mala mbili Fifa si ndiyo? Hata hapo clouds hufai kufanya kazi watu wanaichukia radio sababu yako, omba kazi Simba tujue moja, badala ya kufuatilia HeLa za simba Etoile unapoteza vocha kuulizia Okwi, utakuwa mchawi wewe ila Yanga huiwezi.

    ReplyDelete
  19. mr shafi nina kipande cha ushauri kwako nianze na swali' je okwi akichezea yanga na akiwa safe unafikiri watu wanaosikiliza kipnd cha spots extra watakufikiriaje? alf kipnd okwi anapata tabu tunisia ulikuwa unaongea xana redion kuonyesha huruma yako juu yake(hypocricy) what i think to keep your value up to date stay away from okwis's matter otherwise you gonna endanger your work'

    ReplyDelete
  20. SHAFFIH HOVYOOOOOOOOO! UNAHANGAIKA NINI WEWE NA MAMBO YA OKWI NA YANGA? HUNA KAZI NYINGINE ZA KUFANYA? WEWE NI NANI KATIKA SWALA HILI? MBONA UMELING'ANG'ANIA SANA SWALA LA OKWI WEWE? UMEUMIA SAAAANA. UNAZI UTAKUAIBISHA WEWE. ONA SASA UNAVYOFEDHEHEKA, AIBUUUUUU.

    ReplyDelete
  21. Hata macheda ni mchezaji wa man united lakini hayuko kwenye list yao hili swala okwi zima NI TFF NDIO YA KULAUMIWA WAO NDIO WAONGO NA WANAFIKI WAKUBWA LAKINI MWISHO WA SIKU KILA KITU KITAJULIKANA ,RAGE MWIZI NA MROHO WAPESA ULIONA WAPI MWENYEKITI WA TIMU ANAUZA MCHEZAJI HUU PIA NI UBABAISHAJI KWANAMNA HII SOKA LA TANZANIA LITABAKIA KWENYE MAGAZETI YA UDAKU TU

    ReplyDelete