Search This Blog

Friday, February 21, 2014

KUELEKEA KOMBE LA DUNIA: ENGLAND KATIKATI YA URUGUAY NA ITALIA, KUNDI D


Na BARAKA MBOLEMBOLE

WIKI ILIYOPITA tulitazama kundi la pili la michuano ijayo ya kombe la dunia ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake nchini Brazil Juni mwaka huu.   Mabingwa watetezi Hispania, Uholanzi, Australia na Chile ndiyo wanaounda kundi hilo. Leo tunalitazama kundi la nne ( kundi la tatu utalitazama kesho katika mtandao huu) Kundi la D, Lina nchi za  England, Uruguay, Italia na Costa Rica/

NI mataifa machache sana yenye historia ya soka kama Uruguay ' The Sky Blue One'. IKiwa ni nchi yenye wakazi wasizidi millioni nne Uruguay inajivunia kuwa moja ya mataifa yenye mataji mengi ya kimataifa duniani.  Imetwaa ubingwa wa kombe la dunia mara mbili, 1930, na 1950, pia wanaongoza kwa kutwaa ubingwa wa Amerika ya Kusini mara nyingi zaidi, mara 15, huku ubingwa wao wa mwisho wakitwaa mwaka 2011 nchini Argentina.

Mabingwa hao wa kwanza wa dunia,  tayari wamecheza michezo 47 ya fainali za kombe  la dunia, wakiwa wamepata ushindi mara 18, kutoa sare mara 12 na kupoteza michezo 17, wamefunga mabao 76 na kuruhu nyavu zao mara 65. Walimaliza katika nafasi ya nne katika fainali zilizopita, WOZA 2010, na sasa wamefuzu kwa fainali zao za 12 kati ya 20.

Kiwango cha sasa cha nchi ya Costa Rica  kinaweza kufanya kundi hilo kuhesabika kama ni moja ya makundi magumu zaidi, kwani wawakilishi wa Ulaya, England na Italia walifanya vibaya katika fainali zilizopita. England iliishia hatua ya 16 bora na Italia ilishindwa hata kuvuka hatua ya makundi.

Mabingwa hao mara nne, ' Azzurri' ni moja ya mataifa mawili ambayo yanashikilia rekodi ya kutwaa ubingwa huo mara mbili mfululizo sambamba na Brazil, Italia ilitwaa katika miaka ya 1934 na 1938, wakarudia tena katika miaka ya 1982 na 2006.Wamefuzu kwa mara ya 13 mfululizo  kati ya mara 17 walizowahi kufuzu. Hii ni timu ya kombe la dunia. WAmefuzu mbele ya mataifa ya Denmark, Czech Republic, Bulgaria, Armenia na Malta,  wakishinda michezo sita na sare nne kati ya michezo 10 waliyocheza.

Kikosi hicho kiliifunga England katika robo fainali ya michuano ya Euro 2012 na hatimaye kufika fainali wakati huo. Imeshacheza jumla ya michezo b3,  wakishinda michezo 45, sare katika michezo 21, na wamepoteza mara 17, wamefunga mabao 130 na wameruhusu mabao 78. Italia na Uruguay zinaweza kuvuka kundi hili na kuziacha nje England na Costa Rica.

England ' The Three lions' wamefuzu tena kwa fainali za kombe la dunia. NI moja ya timu maarufu sana katika michuano hiyo japo huwa haifanyi vizuri. Mafanikio yao ya mwisho ni katika fainali za mwaka 1990 walipofanikiwa kufika hadi hatua ya nusu fainali, walishindwa kufuzu kwa fainali za mwaka 1994 na wakaondolewa katika hatua ya robo fainali katika fainali za miaka ya 2002, 2006, na wakaishia hatua ya mtoano mwaka 2010.

Wamewahi kucheza michezo 59 katika fainali 13 walizopita miaka ya nyuma, wameshinda mara 26 tu, sare wametoa mara 19 na wamefungwa michezo 14. Ni moja ya timu zenye uhaba wa mabao katika michuano hiyo, wakiwa wamefunga mabao  77 na kuruhusu mabao 52 ni wastani wa chini katika ufungaji na uzuiaji katika kombe la dunia. Costa Rica wanatajwa kama vibonde katika kundi hili wamefuzu kwa fainali zao za nne. Wamewahi kuishia hatua ya 16 bora katika fainali za mwaka 1990 na wamewahi kuishia hatua ya makundi katika miaka ya 2002 na 2006. WAmecheza michezo 10 ya fainali za kombe la dunia, wameshinda michezo mitatu, wametoa sare mchezo mmoja na wamepoteza michezo sita. Hii ni ratiba ya mechi za kundi hili.
June 14 Fortaleza, 2000:

Uruguay v Costa Rica

June 15 Manaus, 0200:

England v Italy

June 19 Sao Paulo, 2000:

Uruguay v England

June 20 Recife, 1700:
Italy v Costa Rica

June 24 Natal, 1700:
Italy v Uruguay

June 24 B. Horiz, 1700:

No comments:

Post a Comment