Search This Blog

Tuesday, January 7, 2014

TFF KUZIHAMISHA OFISI ZAKE KARUME ILI KUPISHA UJENZI WA KITEGA UCHUMI.Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF lina mpango wa kuhamisha ofisi zake zilizopo maeneo ya uwanja wa karume na kuzipeleka maeneo ya katikati ya mji.
Akizungumza hapo jana kwenye kipindi cha SPORTS BAR cha Clouds TV katibu mkuu wa shirikisho hilo bwana Celestine Mwesigwa alisema TFF wapo mbioni kuingia makubaliano na mwekezaji ambaye atasaidia ujenzi wa kitega uchumi kwenye eneo zilipo ofisi hizo kwasasa.
‘’Moja kati ya mipango ya shirikisho ni kuongeza vyanzo vya mapato ambavyo vitasaidia kurahisiha utekelezaji wa shughuli mbali mbali za shirikisho,kama unavyojua FIFA na CAF wapo tayari kutoa msaada mahala ambapo mwanachama wake hutaka kufanya jambo la maendeleo.’’ Alinukuliwa hapo jana Mwsesigwa.

No comments:

Post a Comment