Search This Blog

Sunday, January 19, 2014

SAMUEL ETO'O 3 MANCHESTER UTD 1.

Samuel Eto'o amekuwa mchezaji wa nne kuifunga Machester Utd mabao 3 ( Hat Trick ) kwenye ligi kuu ya England.

Eto'o ameungana na kina Romelu Lukaku,David Bentley na Dirk Kuyt kuifunga Man Utd Hat Trick baada ya kufunga mabao yote matatu kwenye mchezo ambao Chelsea imeifunga Man Utd mabao 3-1 kwenye uwanja wa Stamford Bridge.
Pia bao la pili la Eto'o kwenye mchezo huo lilikuwa bao lake la 300 kwenye historia yake ya kucheza soka.

   Miongoni mwa walioumizwa sana na mabao ya Eto'o alikuwa ni Sir Alex Ferguson.

Hat Trick ya Eto'o ilikuwa ni ya 25 kwa wachezaji kutoka Barani Afrika kwenye ligi kuu ya England akiungana na wakali kama Mghana Tony Yeboah,Wanigeria Nwankwo Kanu,Yakubu Aiyegbeni,Peter Odemwingie,Wa-Ivory Coast Didier Drogba na Salomon Kalou wengine ni Emmanuel Adebayor,Peter Ndlovu bila kumsahau raia mwingine wa Cameroon mshambuliaji wa zamani wa West Bromwich Albion Somen Tchoyi.

No comments:

Post a Comment