Search This Blog

Sunday, January 19, 2014

MALINZI: ZAMA ZA KUPINDUANA HAZIPO TENARAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Jamal Malinzi, amezitaka klabu hapa nchini, ambazo zitatoa wachezaji wa timu ya Taifa kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya AFCON zikubaliane na hali halisi ya mabadiliko ya ratiba ya michuano hiyo.


Malinzi aliyasema hayo katika Mkutano wa Yanga akiwa kama Mgeni Rasmi alisema, ni vyema klabu zikafahamu ratiba hiyo ambayo kwa namna moja ama nyingine inaweza kuathiri ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara inayotarajia kuanza Januari 25 mwaka huu.

Alisema, kuna uwezekano wa wachezaji kuchukuliwa wakati timu zao zinacheza Ligi, hivyo basi akizitaka klabu zote kujiandaa kwa usumbufu huo wa kuwaruhusu wachezaji endapo watafanikiwa kuitwa katika timu hiyo ya Taifa.


Katika hatua nyingine, Malinzi amewataka wanachama wa klabu mbalimbali hapa nchini kuheshimu katiba za klabu zao na kuwaacha viongozi waliowateua kuwatumikia mpaka muda wao utakapomalizika, kwani migogoro ni ngumu kujenga timu na ndio sababu ya kutokuwa na wachezaji wazuri wa timu ya Taifa kutokana na migogoro hiyo.

“Klabu muache migogoro, kaeni mjenge timu zenu, kuanzia timu za vijana kwani programe ya TFF kwa sasa ni vijana kwanza, nawaomba Yanga na wadau wote wa Soka mlioko hapa tushirikiane katika hilo,”alisema na kuongeza kuwa, wameamua kuanzisha tiketi za kierektroniki ili kuzifanya klabu kunufaika na mapato ya viwanjani huku pia akizitaka klabu kutafuta vyanzo vyao vya mapato.

No comments:

Post a Comment