Na Baraka Mbolembole
Shomari Kapombe, bahati
nzuri ni kwamba namfahamu toka akiwa kijana mdogo, chini ya mikono ya
marehemu Mwalimu, Yahaya Berlin, akiwa katika kikosi cha vijana chini ya
miaka 12 Jamghuri Ball Boys, baadae akazidi kukua kiumri, ila
alionekana kukua haraka sana kimchezo. Akajiunga na timu ya Moro Kids
chini ya walimu, Allan Sigo na Mao. Mzee mmoja hivi nasikia ndiye
alikuwa mlezi wake, na wengi tulikuwa tukimuona kama baba yake na
Shomari. Mzee huyo ni maarufu sana mjini Morogoro, ni mkereketwa mkubwa
wa mchezo wa soka.
Yeye huratibu michuano mingi katika uwanja wa
Shujaa, uliopo kando kidogo ya mji. Maeneo ya Mafisa. Mafisa ndiyo eneo
ambalo hutoa wahuni wengi zaidi katikati ya mji wa Morogoro, ila Mzee
huyo ambaye siwezi kumtaja jina lake yeye anakubalika kwa kila rika.
Wakati fulani alikuwa mwenyekiti wa matawi ya klabu ya Yanga , mkoani
Morogoro. Kiufupi ni kwamba mahali alipokulia Shomari si salama kwa
wakati huu akkiwa na jina kubwa katika soka. Mafisa ndipo walipozaliwa
na kukulia nyota wengi wa Morogoro wa kizazi cha kuanzia miaka ya 2000.
Kina, Lulunga Mapunda, Godson Mmasa, Patrick Betwel na wengineo. Hawa ni
baadhi tu, na walikuwa na vipaji vya hali ya juu ila walikuja kupotea
haraka.
Unawakumbuka, Faustino Lukoo, Titto Andrew, Shengo
Tondola, Jumanne Ramadhani, Christopher Alex, Ulimboka Mwakingwe, hawa
ni baadhi tu. Ukitoka Mecky Mexime wachezaji hao waliondoka katika
viwango vyao vya kawaida wakiwa bado na nguvu. Walikuwa na vipaji,
pengine mara kumi zaidi ya Kapombe. Betwel alikuwa akicheza kwa
kujihamini nafasi yoyote, wakati fulani akiwa Mtibwa alikuwa akicheza
nafasi ya ulinzi wa kati, akawa anajipasia pasi kwa kugongesha mpira
katika nguzo ya goli. Nani aliweza hivyo, mara moja aliigharimu Mtibwa
akajikuta akijifunga wakati wa mchezo dhidi ya Simba. Fau, alikuwa namba
sita bora baada ya Suleiman, siasa za U- simba na U- yanga zilimuweka
mbali, nafasi hiyo akapewa WAzir Mahadhi aleyekuwa Yanga. Fau,
alitunmika sana kama mlinzi namba nne au tano, katika vilabu vya Moro
United na Mtibwa Sugar kutokana na utulivu wake na uwezo wa kuongoza
wenzake, alikuwa na kipaji cha juu katika kumiliki mpira, kupiga pasi,
na alikuwa muhamasishaji sana. Alifanana na Matola, ila alizidiwa katika
uwezo wa kuipandisha timu kwa kasi
Vipi kuhusu vipaji vya Totto, Shengo, Lulanga?
Morogoro ni mkoa wenye vipaji sana, ila kwa nini havidumu?. Wachezaji wa
mkoa huo hasa wale wanaokuwa wamefanikiwa huwa ni watu wa starehe sana,
starehe ya Morogoro ni rahisi sana. Unapokuwa na kitu utaufaidi mji
ule, ila ukiwa huna utajuta kwa kuwa matumizi ni rahisi sana kuliko njia
za kuingiza kipato. Hapa tunakuwa tunawazungumzia hadi wachezaji ambao
awali hawakuwa na ndoto za kufanikiwa kwa haraka, ila wakahja kupata
mafanikio ndani ya muda mfupi kuliko matarajio. Kuna wachezaji walikuwa
wakiishi Dar e Salaam siku tatu, na siku nne wanakuwa Morogoro.
Ila Kapombe ni kama alipata bahati ya kuvuka mtego
huo ambao uliwanasa wachezaji kama Alex, Betwel kwa kupata nafasi ya
haraka ndani ya Simba, na kisha kupata nafasi timu ya Cannes ya
Ufaransa. Haijajilishi ni timu ya daraja gani, ila kwa umri wa Kapombe
anayo nafasi ya kufanikiwa zaidi kuliko akiendelea kucheza soka nchini.
Tangu alipokuja kuiwakilisha timu ya Taifa mwezi, novemba mwaka uliopita
mchezaji huyo bado yupo tu nchini. Aliumia katika mchezo dhidi ya
Zimbabwe, ila alionekana kukua kimchezo. WAkati anakwenda huko
ililipitiwa kuwa alikwenda kwa mkataba wa mkopo wa miaka miwili.
Sitahoji sana katika hilo ila ninaulizia tu inakuwaje mchezaji huyo bado
yupo nchini? mbaya zaidi yupo kwao Morogoro. Ni hatari ushauri wa bure
tu ni kwamba Kapombe anatakiwa kutazamwa wakati huu vinginevyo, njia
yake itakuwa ileile ya kina Titto. Kapombe ananye mazoezi na Simba na
awe kambini na wachezaji wa timu hiyo na si kumuacha Morogoro wakati huu
mipango yake ikitazamwa vizuri.
Hivi wakala wake aliyempeleka huko ni nani?pengine iwe fundisho kwa viongozi wa simba na vilabu vingine,Simba imekuwa inajisifia wao wanauza wachezaji nje kwa kutumia mawakala feki matokeo yake wachezaji wanateseka kwa kishi maisha ya tabu bila kulipwa mishahara,matokeo yake hurudi bila ya mafanikio yeyote bali ni kupotezeana muda na hata wachezaji kushuka kiwango na kukosa timu ya kuchezea kwa muda mrefu.Hii imemtokea Haruna Moshi,Emmanuel Okwi japo aliokolewa na Sports Club villa kabla ya Yanga kumchukua.Pengine unaweza kujiuliza Simba ilinufaika na nini kwa kumpeleka Kapombe Ufaransa na kisha kumtelekeza,huyo wakala aliyempeleka ni wakala wa ukweli au ni mtu wa mishemishe kama mimi?Pengine kutokuw ana elimu kwa wachezaji wa kwetu kunaweza kuchangia,maana kama dalili za kutelekaza hujulikana tu,Lunyamila aliwahi kwenda kucheza ujeruman bahati nzuri alikaa na sekion Kitojo wa Dw,baada ya kuona ngoma ni nzito Sekioni akamwambia arudi nyumbani kucheza,kuliko huyu wakala wa kapombe alivyofanya.
ReplyDeletelabda kapombe nae kaludi kama alivyoludi ngasa
ReplyDeleteTatizo sio mawakala, ukipata nafac ya kucheza ulaya kinachotakiwa ni kujituma! Kupata nafac ulaya sio kazi nyepec kama wachezaji wetu wanavyodhani. Tatizo kwa ni wachezaji wa kitanzania, hawajitambui! "Lack of commitment" ndio tatizo kubwa. Watu wanataka wafanikiwe haraka, wachukue ujinga wa simba na yanga waende nao ulaya! Waulizeni akina Georg Opong Weah, watakwambia magumu waliyopitia hadi kufikia mafanikio! Ugumu wa maisha ni kipimo cha akili na c kukata tamaa, tuache visingizio! Waliondoka hapa nchini Nonda Shabani na Bakari Malima, Nonda kasonga mbele na Bakari akarudi nyumbani! Jiulize mawakala walikuwa tofauti!!? Ukipata jibu hauotowatuhumu mawakala tena bali wachezaji wenyewe! Badala ya kuwaiga akina Mess na CR7, tunawaiga akina Balotel na Gaza. Hayo ndio matokeo
ReplyDelete