Search This Blog

Monday, January 13, 2014

MNATAKA KUMMALIZA NA SHOMARI KAPOMBE?


Na Baraka Mbolembole

Shomari Kapombe, bahati nzuri ni kwamba namfahamu toka akiwa kijana mdogo, chini ya mikono ya marehemu Mwalimu, Yahaya Berlin, akiwa katika kikosi cha vijana chini ya miaka 12 Jamghuri Ball Boys, baadae akazidi kukua kiumri, ila alionekana kukua haraka sana kimchezo. Akajiunga na timu ya Moro Kids chini ya walimu, Allan Sigo na Mao. Mzee mmoja hivi nasikia ndiye alikuwa mlezi wake, na wengi tulikuwa tukimuona kama baba yake na Shomari. Mzee huyo ni maarufu sana mjini Morogoro, ni mkereketwa mkubwa wa mchezo wa soka.

Yeye huratibu michuano mingi katika uwanja wa Shujaa, uliopo kando kidogo ya mji. Maeneo ya Mafisa. Mafisa ndiyo eneo ambalo hutoa wahuni wengi zaidi katikati ya mji wa Morogoro, ila Mzee huyo ambaye siwezi kumtaja jina lake yeye anakubalika kwa kila rika. Wakati fulani alikuwa mwenyekiti wa matawi ya klabu ya Yanga , mkoani Morogoro. Kiufupi ni kwamba mahali alipokulia Shomari si salama kwa wakati huu akkiwa na jina kubwa katika soka. Mafisa ndipo walipozaliwa na kukulia nyota wengi wa Morogoro wa kizazi cha kuanzia miaka ya 2000. Kina, Lulunga Mapunda, Godson Mmasa, Patrick Betwel na wengineo. Hawa ni baadhi tu, na walikuwa na vipaji vya hali ya juu ila walikuja kupotea haraka.

Unawakumbuka, Faustino Lukoo, Titto Andrew, Shengo Tondola, Jumanne Ramadhani, Christopher Alex, Ulimboka Mwakingwe, hawa ni baadhi tu. Ukitoka Mecky Mexime wachezaji hao waliondoka katika viwango vyao vya kawaida wakiwa bado na nguvu. Walikuwa na vipaji, pengine mara kumi zaidi ya Kapombe. Betwel alikuwa akicheza kwa kujihamini nafasi yoyote, wakati fulani akiwa Mtibwa alikuwa akicheza nafasi ya ulinzi wa kati, akawa anajipasia pasi kwa kugongesha mpira katika nguzo ya goli. Nani aliweza hivyo, mara moja aliigharimu Mtibwa akajikuta akijifunga wakati wa mchezo dhidi ya Simba. Fau, alikuwa namba sita bora baada ya Suleiman, siasa za U- simba na U- yanga zilimuweka mbali, nafasi hiyo akapewa WAzir Mahadhi aleyekuwa Yanga. Fau, alitunmika sana kama mlinzi namba nne au tano, katika vilabu vya Moro United na Mtibwa Sugar kutokana na utulivu wake na uwezo wa kuongoza wenzake, alikuwa na kipaji cha juu katika kumiliki mpira, kupiga pasi, na alikuwa muhamasishaji sana. Alifanana na Matola, ila alizidiwa katika uwezo wa kuipandisha timu kwa kasi 

Vipi kuhusu vipaji vya Totto, Shengo, Lulanga? Morogoro ni mkoa wenye vipaji sana, ila kwa nini havidumu?. Wachezaji wa mkoa huo hasa wale wanaokuwa wamefanikiwa huwa ni watu wa starehe sana, starehe ya Morogoro ni rahisi sana. Unapokuwa na kitu utaufaidi mji ule, ila ukiwa huna utajuta kwa kuwa matumizi ni rahisi sana kuliko njia za kuingiza kipato. Hapa tunakuwa tunawazungumzia hadi wachezaji ambao awali hawakuwa na ndoto za kufanikiwa kwa haraka, ila wakahja kupata mafanikio ndani ya muda mfupi kuliko matarajio. Kuna wachezaji walikuwa wakiishi Dar e Salaam siku tatu, na siku nne wanakuwa Morogoro.

Ila Kapombe ni kama alipata bahati ya kuvuka mtego huo ambao uliwanasa wachezaji kama Alex, Betwel kwa kupata nafasi ya haraka ndani ya Simba, na kisha kupata nafasi timu ya Cannes ya Ufaransa. Haijajilishi ni timu ya daraja gani, ila kwa umri wa Kapombe anayo nafasi ya kufanikiwa zaidi kuliko akiendelea kucheza soka nchini. Tangu alipokuja kuiwakilisha timu ya Taifa mwezi, novemba mwaka uliopita mchezaji huyo bado yupo tu nchini. Aliumia katika mchezo dhidi ya Zimbabwe, ila alionekana kukua kimchezo. WAkati anakwenda huko ililipitiwa kuwa alikwenda kwa mkataba wa mkopo wa miaka miwili. Sitahoji sana katika hilo ila ninaulizia tu inakuwaje mchezaji huyo bado yupo nchini? mbaya zaidi yupo kwao Morogoro. Ni hatari ushauri wa bure tu ni kwamba Kapombe anatakiwa kutazamwa wakati huu vinginevyo, njia yake itakuwa ileile ya kina Titto. Kapombe ananye mazoezi na Simba na awe kambini na wachezaji wa timu hiyo na si kumuacha Morogoro wakati huu mipango yake ikitazamwa vizuri.

3 comments:

  1. Hivi wakala wake aliyempeleka huko ni nani?pengine iwe fundisho kwa viongozi wa simba na vilabu vingine,Simba imekuwa inajisifia wao wanauza wachezaji nje kwa kutumia mawakala feki matokeo yake wachezaji wanateseka kwa kishi maisha ya tabu bila kulipwa mishahara,matokeo yake hurudi bila ya mafanikio yeyote bali ni kupotezeana muda na hata wachezaji kushuka kiwango na kukosa timu ya kuchezea kwa muda mrefu.Hii imemtokea Haruna Moshi,Emmanuel Okwi japo aliokolewa na Sports Club villa kabla ya Yanga kumchukua.Pengine unaweza kujiuliza Simba ilinufaika na nini kwa kumpeleka Kapombe Ufaransa na kisha kumtelekeza,huyo wakala aliyempeleka ni wakala wa ukweli au ni mtu wa mishemishe kama mimi?Pengine kutokuw ana elimu kwa wachezaji wa kwetu kunaweza kuchangia,maana kama dalili za kutelekaza hujulikana tu,Lunyamila aliwahi kwenda kucheza ujeruman bahati nzuri alikaa na sekion Kitojo wa Dw,baada ya kuona ngoma ni nzito Sekioni akamwambia arudi nyumbani kucheza,kuliko huyu wakala wa kapombe alivyofanya.

    ReplyDelete
  2. labda kapombe nae kaludi kama alivyoludi ngasa

    ReplyDelete
  3. Tatizo sio mawakala, ukipata nafac ya kucheza ulaya kinachotakiwa ni kujituma! Kupata nafac ulaya sio kazi nyepec kama wachezaji wetu wanavyodhani. Tatizo kwa ni wachezaji wa kitanzania, hawajitambui! "Lack of commitment" ndio tatizo kubwa. Watu wanataka wafanikiwe haraka, wachukue ujinga wa simba na yanga waende nao ulaya! Waulizeni akina Georg Opong Weah, watakwambia magumu waliyopitia hadi kufikia mafanikio! Ugumu wa maisha ni kipimo cha akili na c kukata tamaa, tuache visingizio! Waliondoka hapa nchini Nonda Shabani na Bakari Malima, Nonda kasonga mbele na Bakari akarudi nyumbani! Jiulize mawakala walikuwa tofauti!!? Ukipata jibu hauotowatuhumu mawakala tena bali wachezaji wenyewe! Badala ya kuwaiga akina Mess na CR7, tunawaiga akina Balotel na Gaza. Hayo ndio matokeo

    ReplyDelete