Search This Blog

Monday, November 4, 2013

NAHODHA SIMBA SC AISUBIRIA ASHANTI



NAHODHA wa Simba, Nassor Masoud ‘Chollo’ amesema kikosi chake kipo kamili kuweza kuivaa Ashanti United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Bara keshokutwa Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Simba inaingia katika mchezo huo huku ikiwa inashika nafasi ya nne ikiwa na pointi 21 baada ya mechi 12, wakati Ashanti yenyewe ina pointi 10 ikiwa katika nafasi ya 11 baada ya kucheza mechi 12 pia.
Ashanti ni miongoni mwa timu tatu zilizopanda msimu huu wa Ligi Kuu huku nyingine zikiwa ni Mbeya City na Rhino Rangers ya Tabora, imeonyesha kuzinduka katika ligi hiyo baada ya kuanza kwa kusuasua hapo awali.
Akizungumza na mtandao huu, Chollo amesema anaamini wachezaji wenzake wapo tayari kwa mchezo huo ambao ni muhimu kwao kuweza kujiongezea pointi muhimu ambazo zitaiwezesha timu hiyo kupaa kutoka nafasi ya nne wanayoshika sasa.

“Unajua ligi ni ngumu kweli kweli, kila timu tunayokutana nayo ni ngumu lakini nadhani baada ya kuyumba kwa muda kidogo sasa umefika wakati wa kufanya vizuri kwa kuhakikisha tunafanya vizuri mbele ya Ashanti katika mchezo wa wiki hii na kujiweka katika nafasi nzuri ya kwenye msimamo wa ligi.
“Lengo letu ni kuona Simba inakuwa katika nafasi nzuri kabla ya kwenda kupumzika ligi itakaposimama, lakini hilo litawezekana kama wachezaji tukipambana na kushinda mechi dhidi ya Ashanti,” anasema Chollo.

Chollo alienda mbali kwa kuwataka wachezaji wenzake kuwa wapole muda wote wa mchezo dhidi ya Ashanti na kuachana na tabia za kuanzisha vurugu hata kama watahisi kuna kitu kimeenda ndivyo sivyo.
“Vurugu haziwezi kutusaidia hata kidogo, hata kama tumeonewa bado mashabiki wa Simba wanatakiwa kutushangilia kuanzia mwanzo hadi mwisho ili tu timu ipate hamasa na kushinda,” anasema Chollo.

2 comments:

  1. MKIBAHATIKA BBASI NI PONT MOJA, HILA MTANI JEMBE TEGEMEA MAJANGA. ONYO KWA WALE WANAOKUJA WAKIAMKIA KWENYE SHINDANO LA MTANI JEMBE ALAFU MKIFUNGWA MNAONA KAMA VITLE VITI VYA UWANYANI NI STULI MMEKUJA NAZO TOKA MAJUMBANI KWENU MNANG'OA ILI MRUDI NAVYO MTATAUTAKA UBAYA, NI KHERI MMBAKI BAR MUONGEZE KIPATO CHA TIMU YENU
    NI MM NNDUGUU YENU ISMAIL ADEN RAGE aka MR. PAMA

    ReplyDelete
  2. 2NA nafasi kubwa ya kuwa kileleni mwa ligi (SIMBA)

    ReplyDelete