MPAMBANO wa masumbwi uliokuwa uwakutanishe kati ya Bondia Kalama Nyilawila na Sado Philemon uliokuwa uchezwe Oktoba 20 jumapili katika uwanja wa CCM Mwijuma Mwananyamala umeailishwa kutokana na kupisha mpambano wa watani wa jadi simba na yanga utakaofanyika katika uwanja wa taifa
akiongea mratibu wa mpambano huo
Ibrahimu Kamwe 'amesema mpambano huo umeailishwa kwa muda kupisha mchezo
wa simba na yanga kwa kuwa mashabiki wa mpira ndio hawo hawo mashabiki
wa mchezo wa masumbwi hivyo kwa sasa mpambano uho utafanyika Novemba 3
katika ukumbi uho huo mpambano huo uliokuwa uwakutanishe mabondia
mbalimbali wakongwe na chipkizi sasa utachezwa siku hiyo alitaja
mapambano ambayo yatakuwepo kuwa '
Mwaite Juma na Shadrack ignas , nae bingwa wa zamani wa bantam Ajibu salum atapimana ubavu na Martin
Richard,huku mbena Rajab akizipiga na
Godwin Mawe, Ibrahim class 'King Class Mawe ' atazichapa na Rashid
Ali, Hassan kiwale (Moro best) na Harman Richrd, Kasim chuma na Shaban Manjoly,
mdogo wake francis miyeyusho Yona
miyeyusho atacheza na julias Thomas,
Abdalla ruwanje na Bakari zoro, na kutakuwepo na pambano la kitaa kwa mbabe wa
mwananyamala sokoni joseph stanslaus(amita
au jose mawe) na mbabe wa manzese sokoni
shaban seif(body kitongoji) pambano lililojaa vituko na mbwembwe kwa
mabondia hawa, nae yasin omari atazichapa na Innocent Gabriel pamoja na
mapambano mengine kadhaa ya vijana
wadogo wenye vipaji vya mchezo wa ngumi.
Mapambano haya yote yameandaliwa na Ibrahim kamwe wa bigright promotion kwa kusindikiza pambano la ISSA OMAR(peche
boy) atakaezipiga na ATHONY MATHIAS katika pambano la round nane
na SADO PHILEMON atakaezipiga na KARAMA NYILAWILA katika uzito
wa middle kutafuta mshindi wa
atakaezipiga na Thomas mashali katika pambano la ubingwa.kwa ufupi
mabondia
wote wapo katika hali nzuri na wametakiwa kuendelea na mazoezi kwa ajili
ya mpambano utakaofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao katika ukumbi wa ccm
mwinjuma
mwananyamala A
No comments:
Post a Comment