Search This Blog

Monday, October 21, 2013

PAMBANO LA SIMBA NA YANGA LAINGIZA MILLIONI 500 - WASHABIKI 57,422 WALIKATA TIKETI


Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ya watani wa jadi Simba na Yanga iliyochezwa jana (Oktoba 20 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya mabao 3-3 imeingiza sh. 500,727,000.

Washabiki 57,422 ndiyo waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo namba 63 kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.

Ni tiketi 131 tu ndizo hazikuuzwa ambazo ni 90 za VIP A, 40 za VIP B na moja ya VIP C. Tiketi zilizochapwa kwa ajili ya mechi hiyo ni 57,558 ambayo ndiyo idadi ya viti vilivyopo kwenye uwanja huo.

Kila klabu imepata mgawo wa sh. 123,025,564.32 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 76,382,084.75.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 62,555,371.69, tiketi sh. 7,309,104, gharama za mechi sh. 37,533,223.01, Kamati ya Ligi sh. 37,533,223.01, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 18,766,611.51 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 14,596,253.39.

1 comment:

  1. Huo mgawanyo wa hela ni wa kijinga sana.
    watu wengine zinawakuta ofisi hizo pesa bila jasho lolote na timu zetu zitaendelea kuwa masikini.
    kwangu mgao huo uangaliwe upya.

    kwa maoni yangu ni sawa..
    1. Ya uwanja ni sawa kabisa ili tuweze kumantain uwanja wetu.
    2.Kodi ni sawa ila serikali nayo ingepunguza kidogo 12%VAT.
    ambayo siyakubali migao ya kamati ya ligi,gharama ya mechi...siwaelewi ni wizi mtupu.
    Chondechonde naomba wakae wajadili na wadau jinsi ya mgawanyo unaofaa

    ReplyDelete