Search This Blog

Thursday, October 24, 2013

KIIZA AVUA KIATU CHA DHAHABU YANGA, ATAKA UBINGWA



Mshambuliaji wa Yanga, Hamisi Kiiza amesema hana mpango wa kuwania tuzo ya ufungaji bora yaani kiatu cha dhahabu katika Ligi Kuu ya Bara badala yake anajipanga kuhakikisha timu yake inatetea ubingwa wa ligi hiyo.
Kiiza ambaye hadi sasa amefunga mabao saba, ikiwa ni moja nyuma ya Amisi Tambwe wa Simba ambaye hadi sasa ameshafunga mabao manane.
Baada ya kufunga bao moja moja katika mechi dhidi ya Azam, JKT Ruvu na Kagera Sugar, Kiiza alifunga mabao mawili mawili katika mechi dhidi ya Simba na Rhino Rangers.
Akizunguma na mtandao huu jijini Dar es Salaam, Kiiza amesema licha ya kuwa na mabao saab hadi sasa, hana mpango wa kutolea macho nafasi ya ufungaji bora kwani anachofanya sasa ni kufunga mabao kwa ajili ya timu yake ili iweze kutwaa ubingwa.

“Kuwa mfungaji bora bila ya kutwaa ubingwa hakuna maana yoyote, badala yake mimi najipanga kuhakikisha nafunga mabao muhimu yatakayoiwezesha timu yangu kutwaa ubingwa. Ufungaji bora bila ubingwa unakuwa si lolote,” anasema Kiiza.
Kiiza raia wa Uganda amesema anafurahia akicheza na mchezaji yeyote katika nafasi ya ushambuliaji ndani ya Yanga kwani wote hufanya nao mazoezi na ndiyo maana ameweza kufunga akiwa na wachezaji tofauti tofauti.

Yanga ambayo sasa ina pointi 19 katika mechi 10 ilizocheza, Jumanne ijayo inatarajiwa kucheza na Mgambo JKT katika muendelezo wa ligi hiyo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Yanga inashika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi hiyo yenye timu 14.

No comments:

Post a Comment