Search This Blog

Wednesday, September 25, 2013

WACHEZAJI NDIO CHANZO CHA DI CANIO KUFUKUZWA SUNDERLAND


Inaaminika wachezaji wa Sunderland walilalamika kwa mkurugenzi mkuu wa klabu hiyo Margaret Byrne kuhusu kocha Paolo Di Canio kabla ya kupigwa kalamu.

Di Canio aliitisha mkutano wa timu nzima siku ya Jumapili ambao inasemekana ulikumbwa na majibizano makali kufuatia timu hiyo kushindwa mabao 3-0 na West Bromwich Albion.

Baadae wachezaji waandamizi walimwambia Byrne kwamba hali imekua isioweza kuvumilika kwa sababu ya tuhuma kali na matusi ya Mtaliana huyo dhidi ya kikosi cha timu hiyo.

Kikosi hicho ambacho hujulikana kama 'The Black Cats' wameambulia pointi moja tu kutoka mechi tano za ligi ya Premier League katika msimu huu.

Aliyekua kocha wa Chelsea na West Brom Roberto Di Matteo ndiye anayetabiriwa na wengi kuteuliwa kuwa kocha mpya na wengine wanaotajwa ni Gus Poyet, Tony Pulis na Alex McLeish.

Kocha msaidizi Kevin Ball ameteuliwa kuwa kaimu kocha kwa hivi sasa.

Di Canio ameshinda mechi 3 tu kati ya 13 baada ya kufukuzwa kwa Martin O'Neill mnamo mwezi wa Machi.

No comments:

Post a Comment