Search This Blog

Wednesday, September 25, 2013

MOYES: KIPIGO KAMA CHA MAN CITY KINAWEZA KUIRUDIA - TIMU IPO KATIKA MAPITO"

Kocha wa Manchester United David Moyes amewaonya mashabiki wa mabingwa wa ligi kuu ya England kwamba anahitaji kuimarisha kikosi chake na kwamba kipigo cha Jumapili ambapo walichapwa 4-1 na Manchester City huenda isiwe ndio mwisho wa matokeo kama hayo.
"Kutatokea siku kama ile ya Jumapili na huenda tukakabiliwa na matokeo zaidi kama hayo kwa sababu tuko katika kipindi cha mpito," aliwaaambia waandishi habari kabla ya pambano la Jumaatano la kombe la Capital One dhidi ya Liverpool.

"Tulihitaji wachezaji wawili watatu hivi ambao wangeweza kuingia moja kwa moja katika timu. Lakini hayo yatatokea, kweli huenda itabidi nikabiliane na vipigo vichache zaidi. Bado tunakabiliwa na kazi pevu ya kuwasajili wachezaji sio tu watakaojumuishwa na kikosi chetu lakini wenye uwezo wa kuingia moja kwa moja katika timu," aliongeza kusema Moyes katika msimu wake wa kwanza katyika a Old Trafford baada ya kushikikilia nafasi iliyoachwa na Alex Ferguson.
Manchester United iliwakosa wachezaji kadhaa mastaa wakati wa kipindi kilichopita cha usajili na hata kulikua na tetesi za juhudi za dakika ya mwisho za kuipiku Real Madrid ili kumsajili Gareth Bale ambae kuuzwa kwake kutoka Tottenham Hotspur kulivunja rekodi kama mchezaji ghali kupita wote duniani.
Juhudi za kuwasajili Cesc Fabregas kutoka Barcelona, Ander Herrera kutoka Athletic Bilbao na Fabio Coentrao kutoka Real Madrid ziliambulia patupu.
Leighton Baines aliamua kubaki Everton wakati Thiago Alcantara aliamua kuihama Barcelona na kujiunga na Bayern Munich.
Moyes badala yake alikimbilia kumsajili mchezaji wa kiungo wa Ubelgiji Marouane Fellaini, kutoka klabu yake ya zamani Everton, kwa dola millioni ($43.96 ) dakika chache tu kabla ya kufungwa dirisha la usajili.

1 comment:

  1. Nashukuru kwan unajua kuwa huwezi epuka aibu toka kwa Arsenal Nov 10. Mimi ninachojua Moyes uwezo wake nikufika nafasi ya sita au saba kama alivyozoea Everton hivyo Man U wasitegemee kuwa kwenye top four. Nasijui ingekuwaje kama Rooney nae angeondoka

    ReplyDelete