Search This Blog

Wednesday, August 14, 2013

KOCHA WA EVERTON ATHIBITISHA MAN UNITED WALITUMA OFA MOJA TU KWA AJILI YA LEIGHTON BAINES LAKINI WALIIKATAA

Kocha wa klabu ya Everton Roberto Martinez amesisitiza is kwamba Leighton Baines hatojiunga na Manchester United kwenye dirisha hili la usajili. 


David Moyes amekuwa akihusishwa na usajili wa beki huyo wa kushoto wa Everton lakini Martinez amesisitiza ofa ya £12million iliyotumwa mwezi June ilikuwa ni ya mwisho kutoka United. 


Mchezaji mwenzie Marouane Fellaini pia amekuwa akihusishwa na kumfuata Moyes Old Trafford lakini kocha wa Toffees amesisitiza hatouzwa wakati huu.

'Kabla hatujaenda Austria klabu moja iliwasiliana nasi rasmi wakiwa na ofa ambayo kwao ilikuwa ya mwisho kwa ajili ya Leighton,' alisema Martinez.


'Walitoa ofa ya kiasi cha fedha ambacho hakikuwa karibu na thamani halisi ya ubora alionao Leighton Baines.
'Huo ndio ulikuwa mwisho wao na tangu wakati huo kumekuwepo tu na tetesi kuhusu suala hili.

'Tangu wakati huo hakujawahi kuwa na ofa rasmi kwa Leighton. Tumeachana na hilo suala na tunajiandaa na msimu mpya.' 

Baines anatimiza miaka 29 mwaka huu na ofa yoyote zaidi ya  £12million itakuwa vigumu kwa klabu hiyo kuikataa.  


United ilikuwa ikitegemewa kutuma ofa ya £35million kwa ajili ya Baines na Fellaini lakini sasa dili hilo linaonekana kuwa na uwezekano mdogo kufanyika. 

No comments:

Post a Comment