Search This Blog

Wednesday, August 14, 2013

SAKATA LA AZAM TV VS YANGA: SERIKALI YAAMUA YANGA NA KAMATI YA LIGI KUPITIA UPYA MKATABA - AZAM MEDIA NA YANGA KUFANYA MKUTANO WA KUJADILI MASLAHI YA WANA JANGWANI

Hatimaye mkutano ulioitishwa na serikali kupitia wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo kusuluhisha mgogoro wa mkataba wa mauzo ya haki za matangazo ya Television uliowashirikisha kamati ya ligi kuu ya soka Tanzania bara, klabu ya Yanga na Azam Media umemalizika hivi punde huku maamuzi kadhaa yakifikiwa.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari cha mtandao huu, klabu ya Yanga ni kama imeibuka kidedea kwenye madai yake ya kupinga utaratibu mzima wa mkataba huo baina ya kamati ya ligi na Azam Media. 

Hii inakuja baada maamuzi ya mkutano huo kuamuru kwamba vipengele vya mkataba huo kupitiwa upya na klabu ya Yanga na Kamati ya Ligi na vile ambavyo vitaonekana kuwa na matatizo virekebishwe. 

Pia imeamuliwa kwamba Yanga SC itakaa kikao na Azam Media kuzungumzia mambo mbalimbali ambayo Yanga imeonekana kuwa na shaka nayo kuhusu Azam pamoja na maslahi ya Yanga kupitia dili hilo la ununuaji wa haki za matangazo ya TV ya mechi za ligi uliofanywa na Azam Media. 

19 comments:

  1. Huu ni upuuzi je na timu nyingine zikigoma kuutambuahuo mpya kwa kuwa utakuwa sio kama ule wao walioukubali kabla itakuwaje, serikali itawaita tena na kuamuru wakae chini. Ifike wakati serikali iache kuingilia mabo ya mpira na Yanga nao wawe serious wakati wa michakato. Mwesigwa alisema kuwa walishiriki. Hii ni kuendelea kuwatia kiburi na ndio maana hata kwenye suala la usajili wameendelea kutumia ubabe kwakuwa na viongozi wa TFF na serikali wanazi wao. Hii inakatisha tama ya hata kuangalia mipira ya bongo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni kweli kabisa Yanga wamejazwa kiburi na viongozi wa serikali kwa sababu ya unazi kwa mtindo huu soka letu litabaki hapahapa.

      Delete
  2. Daniel Sospeter NoahAugust 14, 2013 at 7:53 PM

    Hivi ingekuwaje kama yanga ndo wengekuwa wamepata hilo dili na timu kama samba au azamu ndo wangekuwa wanalalamika, je serikali ingeingilia kati?, je ingekuwaje kama Azam media ingekuwa ya MANJI. Ninachokiona hapa ni kwamba kuna mgongano wa kimaslahi kati ya Manji as personal na Azam media. Hamna lolote hapo.

    ReplyDelete
  3. AZAM KOMAENI MSIENDESHWE YANGA, NAWASHAURI MUWAAMBIE MKATABA ULIOKUBALIWA NA KAMATI YA LIGI NDIYO UTAKAOTEKELEZWA NAAMINI WATAPOKEA ILA HUKO KUPIGAPIGA KELELE NI NJAA

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa sababu uwezo wako wa kufikiri ndo umeishia hapo. walioamua hivyo ni wazi wana upeo na wameona tatizo lilipo.

      Delete
  4. yanga wapumbavu hawana lolote kama n maskini watakuwa maskin hivohivo hawa vibaka ndo wanaoturudisha nyuma kisoka

    ReplyDelete
    Replies
    1. Afadhali upumbavu wa yanga wa kujua na kutetea haki yao kuliko umbumbumbu wako na hao kina Rage kwa kutokujua haki zao na kutokujua nafasi yao. Poleni sana ipo siku mtaelewa tu.

      Delete
    2. hoja ndg c matuc....Azam TV hawajakatazwa na Yanga kuonesha mpira..hoja ni kwamba kila timu ipewe inachostahili....milioni 100 kwa vilabu vingine ni sawa (maana wanashangilia) ila kwa Yanga ni kidogo. Fact ni kwamba Yanga inawashabiki wengi kuliko vilabu vingine na hata mapato ya milangoni huwa makubwa Yanga ikiwa inacheza ukilinganisha na Timu nyingine...unaweza ukaona hata target ya Azam TV kufanya biashara inategemea sana uwepo wa Yanga kwny hilo deal ( hawataki kusema waziwazi)...so pay them what they deserve. c dhambi..kwani unafikiri TBL walikuwa wajinga kufadhili Simba na Yanga ingawa Yanga hawakuwa wameomba ufadhili...ndg yangu fikiri angalau kdg kabla ya kutukana...

      Delete
  5. Kwenye kikao hicho Rais wa TFF Leodger Tenga amezungumza wazi kuwa suala hilo la haki za kuonesha mpira ni la kikanuni na limekwenda kwa kufuata kanuni hivyo Yanga kama wanataka kuongezwa fedha hilo linabaki kati yao na Azam na si kamati ya ligi wala TFF. (source supermario blogspot)

    ReplyDelete
  6. Huu ni upuuzi y? Kila mgogoro wa soka unaanzia yanga. Wapeni nafasi azam media wafanye kazi ya kuonyesha ligi. Kuna kituo kimoja walikua wanaonyesha bila malipo ligi yetu au mmesahau au kwakuwa kipo nje ya nchi

    ReplyDelete
  7. vingozi na wapenzi wa yanga hongera sana kwa kushikamana katika jambo hili.yaani haki zetu zinauzwa na third party hata bila sisi kujiuliza kulikoni.yanga na wapenzi wake wanaweza kupoteza hii kesi lakini tusipoteze haki yetu ya kuchagua kitu ambacho kinatuibia uhuru wetu wa kuuliza na kujua.

    ReplyDelete
  8. nina maswali yangu?
    tender ilitangazwa lin? hiyo azam tv iko wapi? kwa nini wasipewe star tv au supersport wanaoonekana dunia nzima kama lengo ni kuiwezesha lig yetu?
    naskia azam tv ni king'amuzi mamaa huku kwetu kijijn ndo basi tena lakin star tv tunaipata vzur. hongeren yangaaa

    ReplyDelete
  9. azam hakuna kuwaongezea hawa wanjinga yanga fedha kama mkataba umeshasainiwa na klabu zote za Tz hawa vibaka wanaleta mgomo wanataka kuongezewa hela cha msingi hakuna kuongeza hela kama vip chukuen hela zem milion mia haf mechi yao isionyeshwe kwan wana nn hawa hata mpira wenyewe hawajui kaz ya kupiga marefa

    ReplyDelete
  10. mbona hajingiliaa kenye riadha kama kweli anauchungu wa maendeleo ya michezo tatizo mnaaendekeza watu wenyewe YANGA haapo tayari kubadilika kama TFF na zabuni ya CRDB ya kusimamia ticket mechi zitaanza hakuna E-card

    ReplyDelete
  11. WATU WENGINE NASHINDWA KUWAELEWA HIVI KAMATI YA LIGI NA MIUNGU KUWA WAKISEMA WAMESEMA,...?

    HIVI THE WAY YANGA WAMEINVEST NI SAWA NA SIMBA ILIYO SAJILI WACHEZAJI WA LAKI TANO NA MILIONI MOJA AU ASHANTI ILIYOSAJILI KWA MALI KAULI AU WENGINE WALISAJILI BURE...?

    IMEFIKA KIPINDI LAZIMA TUWE NA MWELEKEO AZAM WANALENGO ZURI NA YANGA PIA WANA LENGO ZURI KWA MASLAHI YAO.....!!

    YANGA HAWAJA WALAZIMISHA WENGINE WAKATAE MKATABA WAO C WAMELIZIKA KULINGANA NA INVESTMENT YAO...SO YANGA WANAPIGANIA HAKI YAO KAMA CLUB.....!!

    "IMEANDIKWA KUWA NI LAZIMA MMOJA AFE ILI WENGINE WAPATE KUOKOLEWA" MAANA YAKE KT. SWALA LOLOTE NI LAZIMA MMOJA AJITOE MUHANGA ILI WENGIEN WAJJIFUNZE KAMA TOKEO NI BAYA AMA ZURI WATAJIFUNZA..YANGA KEEP IT UP"

    TFF NI CHOMBO CHA SERIKALI NA KAMATI YA LIGI INAFANYA KAZI NA TFF NA IMEUNDWA KWA MISINGI YA KATIBA YA TFF...HIVI MNAOONGEA HAPO JUU MNAWEZA KUTUELEZA KUPATIKANA KWA DILI......YAAZAM ILIFUATA KANUNNI NA SHERIA ZA MANUNUZI ZA SERIAKLI (PPRA)...?

    ILITANGAZWA LINI NA WAKINA NANI WALIOMBA...?

    BAKHERESA NI MJUMBE KWENYE KAMATI YA LIGI HIVYO KISHERIA HAKUPASWA KUPEWA TENDA YA MATANGAZO KWANI HIYO NI ROBBYING NA IMEPUNGUZA USHINDANI WA KIBIASHARA NA WAHITAJI WENGNE...SO NAWASHAURI MSIONGEE KAMA WALEVI NA WATU MANOSUKUMWA NA MIHEMKO YA USHABIKI WA USIMBA/AZAM NA UYANGA....!!

    ReplyDelete
  12. Kabla hujatuma comment uwe unafikiria, kifupi ni hvi, yanga ni bigg brand inayolipa kuliko hata hayo makampuni ya AZAM, ndio maana wakataka kuonyesha ligi ili waendelee kufanya biashara zao vzr, na Katika timu zote kwenye ligi YANGA ndio brand kubwa. Sasa mnao chukia haya mtajiju. HIIIII NDIO YANGAAAAA.ALEX NGAI WA KINONDONI MKWAJUNI.

    ReplyDelete
  13. HIYO NDIO YANGA BWANA UTAIPENDA 2

    ReplyDelete