Search This Blog

Monday, August 5, 2013

CHELSEA VS REAL MADRID: JOSE MOURINHO ASEMA "MADRID KUNA SIASA TUPU NA SIO MICHEZO." AMPONDA CRISTIANO RONALDO PIA

Siku ya jumatano Real Madrid watakutana na Chelsea katika fainali ya michuano ya Guinness Champions Cup huko nchini Marekani, hii ni mechi ambayo itamkutanisha kocha wa Chelsea Jose Mourinho dhidi ya timu yake ya zamani, miezi miwili baada ya Jose na Madrid kuvunja mkataba wao. 

Mourinho tayari ameshazungumza na ESPN wiki iliyopita, katika mazungumzo hayo Jose alisema: "Madrid ni siasa, Madrid haihusu michezo tu kuna siasa katika kila kitu."

Pia Mourinho alimzungumzia aliyekuwa nyota wake wakati akiwa na Madrid - Cristiano Ronaldo kwenye mahojiano hayo ambapo alisema ameshawahi kufundisha mastaa wakubwa akiwemo mchezaji wa zamani wa Brazil, FC Barcelona na Real Madrid Ronaldo: "Nimewahi kufundisha wachezaji wakubwa duniani Rivaldo, Figo, Guardiola na hata 'Ronaldo wa Ukweli' sio huyu Cristiano."  

Lakini Cristiano Ronaldo alipoulizwa kuhusu kauli hii ya kocha wake wa zamani, Ronaldo alisema: "Kuna vitu kwenye maisha ambavyo havihitaji kuzungumziwa. Hili ni mojawapo na sitozungumza lolote kuhusu jambo hili kwa sababu nilizotoa. Siku zote nimekuwa nikiheshimu makocha wangu na najaribu kujifunza kutoka kwao.
Kama tusemavyo nyumbani Ureno: "Hatutemi mate kwenye sahani tunayokulia chakula." Hivyo ndivyo ninavyojisikia. Najaribu na ningependa kukumbuka upande mzuri wa Mourinho."

2 comments:

  1. Mheshimu mjinga uepukane na balaa,real matured CR7 hata Mourinho asemeje kijana anaweza na kudhihirisha hilo hiyo J5 kijana lazima atascore,sasa cjui huyo anayejiita special one atasemaje(hila zake zote watu washazingudua so hana jipya R.I.P MOURINHO na hila zako za kipumbavu)

    ReplyDelete
  2. Hiyo ni mind game tu, huna haja ya kuropoka kiasi hicho. Unapofuatilia kauli za Mourinho usiende moja kwa moja, anaposema kafundisha wachezaji wakubwa zaidi ya Cr7 c kwamba kamtusi ila anajaribu kumtia hofu kijana!

    ReplyDelete