Search This Blog

Monday, August 5, 2013

KATIBU MKUU MSAIDIZI WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA KIKAPU TANZANIA(TBF) AKABIDHI BENDERA YA TAIFA KWA TIMU ZITAKAZOSHIRIKI MASHINDANO YA KIMATAIFA YA KIKAPU (ZONE V CLUB CHAMPIONSHIP):


Katibu Mkuu msaidizi wa shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania,Michael Maluwe akabidhi Bendera ya Taifa kwa timu zitakazo Shiriki Mashindano ya kikapu ya Kimataifa yaliyo andaliwa na shirikisho la Kikapu Afrika Maarufu kama ZONE V CLUB CHAMPIONSHIP.Ikiwa ni ishara ya kuwakilisha Taifa katika mashindano hayo ya Kimataifa,Katibu wa Vijana City Bulls na Kocha wa VIJANA walipokea Bendera hiyo kwa niaba ya timu zote mbili.Vijana city Bulls watawakilisha Taifa kwa Upande wa Wanaume na DON BOSCO LIONESS watawakilisha taifa kwa Upande wa Wanaume.
Mashindano hayo Yanatarajia Kuanza Leo Tarehe 05 mpaka tarehe 11 mwezi huu (August) Huko Bujumbura, nchini Burundi.Timu nyingine zitakazo shiriki michuano hiyo mikubwa Afrika mashariki na KATI kwa upande wa wanaume ni pamoja na URNANI NA NEW STAR za nchi Burundi,USIU(KENYA),ESPOIR(RWANDA),WARRIORS AND FALCONS(UGANDA),NA VIJANA ikiwakilisha Tanzania.
Kwa upande wa wanawake timu zitakazo shiriki ni pamoja na BERCO STARS AND LES GAZELLES(BURUNDI),EAGLE WINGS AND USIU(KENYA),APR(RWANDA),KCCA(UGANDA),DON BOSCO LIONESS itakayo wakilisha TANZANIA.
Bongobasketball inawatakia kila la Kheri TIMU ZOTE MBILI ziwezi kufanya vizuri na kurudi na Ushindi kwa Faida ya ULIMWENGU WA KIKAPU Tanzania.

No comments:

Post a Comment