Search This Blog

Friday, May 31, 2013

KALI YA LEO: SHABIKI WA MAN CITY ATEMBELEA MAKUMBUSHO YA OLD TRAFFORD AKIWA AMEVAA JEZI YA CITY



Smith akiwa mwanae ndani ya Old Trafford
Siku ya leo wakati nikiwa kwenye ziara yangu ndani ya Theatre of Dreams - Old Trafford nilikutana na kali ya mwaka baada ya kumshuhudia shabiki wa klabu ya Manchester City akiwa miongoni mwa mamia ya wapenzi wa soka waliokuja kutalii ndani ya Old Trafford.

Kitendo hicho ambacho ni kigumu kuweza kutokea kwa timu zenye upinzani mkali kama wa City na United kilionekana kutowashangaza watu wengi waliokuja kwenye ziara ndani ya Old Trafford, lakini kwangu mie niliyezoea vurugu na uhasama usiokuwa na dira wa Simba na Yanga nilishangazwa sana. Hivyo nikajaribu kumuuliza Bwana Peter Smith imekuwaje amekuja kutembelea sehemu ya makumbusho wa klabu ambayo ndio mpinzani wake? Smith alinijibu kwamba hilo ni jambo la kawaida tu kwao ingawa yeye hakuwa anataka kwenda kutembelea vivutio vya Old Trafford ila alilazimishwa na mwanae mpenzi ambaye ni shabiki wa mkubwa wa Manchester United na mchezaji Wayne Rooney.

Kwa wakati wote tuliokuwa kwenye ziara hiyo mamia ya mashabiki wa United hawakuwa na habari kidogo na shabiki huyo aliyevaliwa jezi ya Manchester City ndani ya makumbusho ya OT - waliendelea na shughuli zao bila kumbugudhi mpaka ziara ilipomalizika.

Je itawezekana shabiki wa Simba aende makao makuu ya Yanga pale mtaa wa jangwani akiwa kavaa jezi nyekundu na kutoka salama bila bugudha?? Tuige mfano mzuri wa wenzetu waliotutangulia na kuwa wastaarabu.

2 comments:

  1. Kwa hili shafii hauko sahihi lkn ni utamaduni wako kuwaaminisha watu kuwa soka la ulaya linapendwa zaidi kuliko soka la bongo kama mm ninavyoamini waandishi na watangazaji wa mpira wa ulaya ni bora saana kiuweledi kuliko ss hivyo nakukumbusha tu. Vilabu vyetu havina maktaba zao lkn kipindi cha nyuma wakati yanga wanatumia uwanja wao uliopo pale klabuni kwao kila mtu akiwa na vazi la klabu yoyote alifika pale bila bughudha yoyote. Kingine sio kila kitu kifanane na ulaya ushabiki wa simba na yanga una fleva yake wasioijua wanajaribu kuiondoa ili waaharibu soka la bongo lkn hawataweza tuilinde fleva hii ya yanga na simba nchi zingine wanaitamani lkn waliipoteza na haitorudi. Nyinyi clouds mmefanya kila njia kuiharibu lkn mmeshindwa changamoto wekeni mashindano yenu yalee ya kijinga eti mashabiki wa soka la nje na wale wa simba/yanga muone m ziki wake.mwisho nafurahia saana ninapomuona shabiki wa soka kavaa jezi.kofia.bsngili nk za timu za bongo japo inaniuma kwa klabu hizo kutotumia fursa hiyo kibiashara.

    ReplyDelete
  2. Nimeisoma kwa makini hii report ya mwandishi lakini sijaona hoja/mantiki hasa ni nini! Kuvaa alama ya timu uipendayo na kupita kwenye viwanja/ maeneo ya timu pinzani hata bongo hilo lawezekana. Nafikiri Dauda analinganisha na matukio ya siku ya mechi za watani.Hv kama Yanga wakifungua maduka ya bidhaa zenye nembo yake unafikiri wateja watakuwa ni yanga tu? Hali kadhalika kwa simba!

    Badae

    ReplyDelete