Search This Blog

Friday, May 31, 2013

TOUR YANGU NDANI YA OLD TRAFFORD: HATIMAYE MANCHESTER UNITED KUBADILI NYASI MBOVU ZA OLD TRAFFORD BAADA YA MIAKA 10

Shaffih Dauda, Ismail Sota, tour guide wa Old Trafford, na Jonstone Mulunda
Siku ya leo nikiwa bado hapa nchini Uingereza nilifanikiwa kufanya ziara kwenye uwanja wa pili kwa ukubwa hapa UK - uwanja wa Manchester United - Old Trafford.

Katika ziara yangu ya leo kwenye makao makuu ya klabu ya Manchester United nimefanikiwa kujifunza vitu vingi sana, na kwa utaratibu nitaanza kuwajuza wapenzi wasomaji wa mtandao huu.

UWANJA WA OLD TRAFFORD - SEHEMU YA KUCHEZEA
Nikiziaga nyasi za Old Trafford ambazo zinatarajiwa kuondolewa

Katika kipindi cha hivi karibuni sehemu ya kuchezea ya uwanja Manchester United imekuwa ikalalamikiwa kwamba haina ubora mzuri. Kufuatiwa malalamiko hayo uongozi wa Manchester United umeamua kubadilisha nyasi za sehemu ya kuichezea za uwanja zilizodumu kwa takribani miaka 10 sasa. 

Uwanja huo ambao United walianza kuutumia mnamo mwaka 1910 ndio uwanja wa tisa wa ukubwa barani ulaya wenye uwezo wa kuingiza watu 75,765, katika miaka ya hivi karibuni umekuwa ukichezewa mechi za mchezo wa Rugby tangu mwaka 1998, mechi ambazo zimepelekea uharibifu mkubwa wa sehemu ya kuchezea ya Old Trafford.
Timu ya watoto wa Manchester United

Uwanja huo kwa sasa unachezewa na timu ya watoto ya Manchester United baada ya msimu wa ligi kumalizika, na sasa unatarajiwa kuanza kufanyiwa marekebisho baada ya mechi ya magwiji wa klabu ya Manchester United dhidi ya wale wa Real Madrid itakayofanyika siku ya jumapili wiki hii.

Gharama za marekebisho ya nyasi mpya zinazotarajiwa kuwekwa kwenye uwanja huo wa Old Trafford zina gharama ya £250,000, na ukarabati wa huo utaanza rasmi siku ya jumatano.


3 comments:

  1. safiii Dauda tunajifunza mengi tusiyajua kutoka kwako..........

    ReplyDelete
  2. keep us updated that close bro!!pa1 sana shaffih..

    ReplyDelete
  3. Kwanini tu OLD TRAFFORD, NA SI VIWANJA VINGINE KAMA STANFORD BRIDGE AU EMARATE AS WELL AS ANFIELD? NINGEFURAHI SANA LEO KUKUONA UKIWA VIWANJA VINGINE NA SI OT. MTANZANIA ALOONESHA BANGO LA SAF ALISHATUWAKILISHA TAYARI HAPO OT, NAWEWE UNGEENDA SEHEMU NYINGINE SHAFFIII!!!!!!

    ReplyDelete