Search This Blog

Wednesday, April 3, 2013

KOCHA WA MTIBWA SUGAR ATIMULIWA KAZI NA AFC LEOPARDS

AFC Leopards ya Kenya imemfukuza Kocha wake Tom Olaba aliyekuwa akiifundisha Mtibwa Sugar msimu uliopita.
Olaba ametimuliwa kwenye kibarua hicho baada ya miezi mitatu kupita tangu ilipompa dhamana ya kuifundisha timu hiyo.
Kutupiwa virago kwa kocha huyo kumekuja baada ya saa chache kabla ya Leopard (Paka Wakubwa) kucheza na Homeboyz FC kwenye Uwanja wa Mumias Complex jana.
Katika mahojiano na vyombo vya habari nchini Kenya, Makamu Mwenyekiti wa Leopards, Walter Onyino, amesema wamelazimika kuchukua uamuzi huo uli kulinda usalama wa Olaba dhidi ya mashabiki wa klabu waliotishia uhai wake kama angekuwa uwanjani hapo.
“Tumemwita arudi Nairobi kwa sababu mashabiki wametishia kumletea vurugu. Kocha wa makipa, John Busolo na Meneja wa timu, Nicholas Muyoti ndiyo waliopewa jukumu la kuinoa timu hiyo kwa sasa.

No comments:

Post a Comment