Search This Blog

Wednesday, April 3, 2013

BAADA YA KUSHINDWA KUNG'ARA NYUMBANI - HUMUD ATISHA SAUZI AFUZU MAJARIBIO JOMO COSMOS

Kiungo wa Azam FC, Abdulhalim Humoud amefuzu majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika klabu ya Jomo Cosmos ya Afrika Kusini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Meneja wa Azam Patrick Kahemele alisema kuwa, Humoud amefuzu majaribio hayo baada ya kufanya mazoezi na klabu hiyo mara moja na kucheza mechi moja.
"Ni kweli Humud amefuzu majaribio na timu ya Jomo Cosmos, yalikuwa ya wiki mbili."
"Kijana wetu amefuzu majaribio hayo baada ya kufanya mazoezi  mara moja na kucheza mechi moja."
Kahemele alisema kuwa baada ya kufuzu kwake wanasubiri maafikiano baina ya Azam FC na Jomo Cosmo  kuhusu ada ya uamisho ambayo alidai ana uhakika Wataafanikiwa.
"Kama unavyojua kulikuwa na mapumziko ya sikuu ya pasaka,lakini baada ya kwisha tunatarajia Azam na Jomo Cosmo zitazungumza na kuafikiana kuhusu uhamisho wa Humoud," alisema Kahemele.
Iwapo Humoud atafanikiwa kujiunga na timu hiyo atakuwa Mtanzania wa pili kuichezea, baada ya Yusuf Macho 'Musso'

No comments:

Post a Comment