Search This Blog

Wednesday, April 3, 2013

SIMBA YAJIVUA RASMI UBINGWA WA LIGI KUU - YENYEWE YASEMA INATAKA NAFASI YA PILI

UONGOZI wa Simba umeamua kujivua rasmi ubingwa wao na sasa wameamua kuelekeza nguvu zao katika nafasi ya pili ya ligi kuu Tanzania bara ambayo inaelekea ukingoni.
Simba ambayo ni bingwa mtetezi wa ligi jana umetamka rasmi kushindwa kutetea taji hilo na kuziachia Yanga na Azam ambazo zinafukuzana kuwania ubingwa huo.
Ofisa habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga amethibitisha hilo na kudai kuwa kwa sasa uongozi wa klabu hiyo wanajitaidi kuakikisha Simba inamaliza ligi ikiwa nafasi ya pili na kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi mashindano ya Kombe la Shirikisho (CAF) mwakani.
Alisema kuwa hali hiyo imetokana na mwenendo wa timu yao kwa hivi karibuni na kupelekea kushika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi.
''Ni kweli kwa sasa hatuwezi tena kutetea ubingwa wetu. Kilichobaki ni kupigana kumaliza katika nafasi ya pili kucheza Kombe la Shirikisho mwakani."
Kamwaga alisema kwa sasa uongozi wa timu hiyo una changamoto nyingi ikiwemo usajili ya mambo mengine mengi.

No comments:

Post a Comment