Search This Blog

Wednesday, April 3, 2013

JOSE MOURINHO KUIFIKIA REKODI YA ALEX FERGUSON KUWA KOCHA ALIYEFIKA NUSU FAINALI MARA NYINGI KWENYE CHAMPIONS LEAGUE

Jose Mourinho ataweza kuifikia rekodi ya Sir Alex Ferguson kwa kutimiza rekodi ya kuziongoza timu zao kucheza nusu fainali saba kwenye Champions League ikiwa tu Real Madrid itaweza kuitoa  Galatasaray kwenye mchuano wa robo fainali.

Mourinho ameiongoza Madrid kwenye nusu fainali ya Champions league katika misimu yake miwili aliyokuwepo Bernabeu, na timu yake kwa sasa inapewa nafasi ya kuendelea mbele dhidi ya Waturuki. Wanawakaribisha Galatasary leo hii nyumbani kwao kabla ya kwenda kucheza mechi ya marudiano wiki ijayo jijini Istanbul. Los Blancos bado wanalitafuta taji la 10 la ulaya huku Mourinho akiwania kuweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza kushinda champions league na timu tatu tofauti.


Mourinho aliiwezesha Porto kubeba ubingwa wa ulaya mwaka mmoja baada ya kujiunga nayo kwenye msimu wa 2003/04, na hiyo ikawa nusu fainali yake ya kwanza na ya mwisho akiwa na Porto. Msimu uliofuatia akajiunga na Chelsea na akaiongoza The Blues kwa kuifikisha kwenye nusu fainali mara 2 mwaka 2005 na 2007, katika mara hizi mbili ilikuwa ni Liverpool waliomtibulia nafasi ya kwenda fainali.

Mourinho alipoondoka Chelsea akaenda kujiunga na Inter Milan ambapo msimu wake wa kwanza uliishia kwa kubeba ubingwa wa Serie A, na barani ulaya alikuwa Sir Alex Ferguson aliyemtoa kwenye raundi ya 16. Japokuwa msimu uliofuatia Mou aliiongoza Inter kubeba ubingwa wa ulaya, Scudetto na Coppa Italia.

Huo ulikuwa ubingwa wa pili wa ulaya kwa Mourinho na nusu fainali ya nne. Sasa akiwa na Madrid tayari ameshacheza nyingine mbili endapo ataitoa Galatasary ataifikia rekodi ya Sir Alex Ferguson.

Rekodi ya Sir lex Ferguson imekuja kwenye miaka yake 26 aliyokaa na Manchester United. Babu huyo mwenye miaka 71 ameiongoza United kushinda mkombe mawili ya Ulaya, pia akiiongoza kucheza fainali nne. Katika nusu finali amepoteza mara tatu ( 1996-97, 2001-02 and 2006-07) na timu zote zilizomfunga ziliena kuwa mabingwa wa michuano hiyo mwishoni - Borussia Dortmund, Real Madrid and AC Milan.

Mourinho, amepoteza nusu fainali mbili dhidi ya Barcelona (in 2010-11) na Bayern Munich (msimu uliopita).
.

No comments:

Post a Comment