Search This Blog

Tuesday, March 5, 2013

KUFANYA VIBAYA KWA SIMBA: MASTAA WATOA LAWAMA KWA KOCHA - UONGOZI WASEMA LIBOLO WALIJIANDAA VYEMA

Na Edo Kumwembe

BAADHI ya mastaa wa kikosi cha kwanza, Simba (majina tunayo) wamesema hawana imani na mbinu za Kocha Mkuu Patrick Liewig na hilo limethibitika zaidi katika mchezo wao wa Angola.
Mwishoni mwa wiki, Simba ilishambuliwa na kipigo cha mabao 4-0 kutoka  Recreativo Libolo ya Angola katika mchezo wa marudiano Ligi ya Mabingwa Afrika.
Matokeo hayo yanaifanya Simba kuaga mashindano raundi ya kwanza kwa jumla ya mabao 5-1, kutokana na kufungwa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza wiki mbili zilizopita, Dar es Salaam.
Wakizungumza juzi usiku kwenye hoteli ya Ritz iliyopo mji wa Calulu lilikofanyika pambano hilo la marudiano, mastaa hao wamesema mfumo wa sasa wa Simba ni kujihami zaidi kuliko kushambulia.
"Mbinu nyingi tunazotumia ni za kujihami. Mazoezini hatufundishwi kucheza soka la kushambulia na badala yake kocha amekuwa akitumia muda mwingi kutufundisha namna ya kukaba maadui katika maeneo yetu."alisema mchezaji mmoja nyota katika nafasi ya kiungo.
"Mimi siyo msemeji, lakini sasa hivi inabidi niseme. Wachezaji vilevile hatuko fiti. Tunafanya mazoezi kwa dakika chache, hatujawahi kucheza mazoezi ya mechi miongoni mwetu. Uimara wa timu unaanzia mazoezini na sisi hatuko imara." aliongeza staa huyo.
Nyota mwingine wa Simba anayecheza nafasi ya ushambuliaji alisema: "Kutokuwapo Emmanuel Okwi na Patrick Mafisango (marehemu), siyo sababu ya timu kufanya vibaya. Nadhani kocha (Liewig) abadili mbinu."
"Kuna mechi nyingi Okwi hakucheza na bado tulishinda. Mimi sifurahishwi na jinsi tunavyocheza kwa kumtegemea mshambuliaji mmoja mbele." alisema mshambuliaji huyo.
Nyota mwingine wa safu ya ulinzi alihoji mantiki ya viongozi na Benchi la Ufundi kumsajili kipa wakati wa dirisha dogo, huku timu ikiwa na upungufu wa wachezaji katika safu ya ushambuliaji.
Aidha, kiongozi wa msafara wa Simba na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Zacharia Hans Pope amekuja na hoja tofauti na malalamiko ya wachezaji dhidi ya kocha wao.
Hanspope amesema Simba imefungwa kwa sababu wapinzani wao Libolo walijiandaa vizuri kwa mazingira yote, ndani na nje ya uwanja kulinganisha na Simba.
"Yatasemwa mengi, lakini ukweli tumetolewa na timu yenye uwezo kuliko sisi. Wenzetu wamefanya maandalizi mazuri. Kumbuka kuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani waliwahi kuichapa Orlando Pirates ya Afrika Kusini 3-0." alisema Hans Pope.

9 comments:

  1. kufungwa kwa orando pirates sio kigezo cha kujivunia eti tumefungwa kihali kumbuka kuna wakati zamalek waliifunga madrid ya akina zidane goli mbili lakini walipocheza na simba tukashinda kimtizamo wangu uongozi bora ndio unajenga timu bora haiwezekani kwenye uongozi kuna makundi eti utegemeee matokeo mazuri mie nashauri kwa kuinusuru timu na matokeo mabaya zaidi rage na uongozi wake waachie ngazi walipotufikisha panatosha

    ReplyDelete
    Replies
    1. kweli kabisa ,hizi ni lawama za mfa maji,wakati wanaifunga yanga sio kwamba yanga ilikua mbaya la hasha ,ilikua uongozi mbaya na hili ni ukweli kabisa.

      Delete
  2. Hata akija Furgie kwa mtindo huu wa sasa wa Simba hataweza! Na mbona mlimtimua kocha aliyekuwepo? Naomba kuwasilisha. NURU SPORTS MSM.

    ReplyDelete
  3. Kwa ushauri wenu kama mnataka rage atimuliwe nani awekwe anaye weza kuongoza na team kupata matokeo mazuri!!!!!!? Kumbukeni kuna zama kupanda na kushuka simba kwasasa inabidi ifanyike kazi ya ziada kufanya usajili makini kwa ajili ya mwakani, angalia wenzetu yanga wamefanya usajili makini na leo team inafanya vizuri.

    Watu mnaishia kuwalaumu rage mara kaburu wanacheza namba ngapi uwanjani tusitarabike sie wtu tusiishie kufuata ushabiki usio na maana wa lawama tu bila kutafuta suruhisho rage mwenyewe ana muda gani ili amalize uongozi wake!!! leo mnalazimisha kung'oa viongozi itawasaidia nini

    ReplyDelete
  4. sidhan kama kocha hafai ila nadhani tuma kwa ujumla haiko vzuri, kuanzia beki na safu ya ushambuliaji, viongozi nao hawafai cjui kama huwa wanashrikiana katika kufanya maamz ya kuafany a usajil,simba waliboronga toka zaman kuafanya usajili wa maana, hvo m nadhan ni mda muafaka wa kuondoa tofauti za wanasimba kutafuta cha kufanya ili kurudsha hadhi ya simba

    ReplyDelete
  5. simba bwna tatizo nn jamani?

    ReplyDelete
  6. Simba imetolewa kwa idadi ya goli 5-0 na sio 5-1 kama ulivyoandika.

    ReplyDelete
  7. TATIZO FRIENDS OF SIMBA NI WABABE TIMU MPAKA INABOA. DAWA KUWACHAPA VIBOKO WOTE WANAOTUDHALILISHA MAANA 4BILA NI AIBU

    ReplyDelete
  8. Hizo zote kelele tu! Ubovu wa Simba ulianza kwa kuondoka kwa Phiri, na sisi washabiki hatukujiuliza sababu! Mimi niliamini,tunahitaji kupunguza matumizi,kama mpango wa kuanza kushughulikia Ujenzi wa Uwanja! Sio kwamba wakati wa Phiri, timu ilikuwa bora kama Simba kweli,ila ilikuwa tayari inashika kasi ya KUUNDWA. Tuwe wakweli, timu yetu, imeshuka UWEZO na huo mpango,tunahitaji kujipanga. Lakini kubwa kwangu mimi ni kuwa;

    1. Kocha na Uongozi, Sisi tuna phylosophy yetu,asiibadili. Mimi hata Simba ifungwe vipi,kinachoniuma sana na cha kwanza huwa ni kama simba wanacheza mpira wa hao jamaa,wa kubutuabutua na bora goli na ushindi, hata wakishinda, bila mpira wetu,huwa natoka uwanjani shingo upande!

    2. Sisi mashabiki wa Simba tudai Uwanja Tu kwa sasa!

    ReplyDelete