Search This Blog

Monday, March 4, 2013

WAKATI SANTOS IKIWA NA HALI MBAYA LIGI YA BRAZIL - NEYMAR ASEMA ATAENDA KUCHEZA ULAYA MUDA WOWOTE ATAKAOJISIKIA

Neymar

 Neymar amesema kwamba anaweza kwenda kucheza soka barani ulaya hata kabla ya mkataba wake na Santos unaoisha baada ya kombe la dunia mwakani kuisha. 

Mbrazil huyo amesema kwamba ana furaha kuwepo Santos lakini anaweza kuondoka ikiwa atajisikia yeye binafsi kwamba ni kitu sahihi kukifanya kwa muda huo. 

Mpaka sasa, Neymar amekuwa akiripotiwa kwamba hatoondoka Santos mpaka kuisha kwa 2014 World Cup litakalofanyika nchini Brazil. 

Mchezaji mwenzie wa Brazil Daniel Alves hivi karibuni aliziambia media za Spain kwamba mshambuliaji huyo amefikia makubaliano ya kujiunga na Barcelona baadae mwaka huu, lakini Neymar amekanusha taarifa hizo zilizotolewa na rafiki yake.  

Neymar aliongea kuhusu kwenda ulaya baada ya kuwa na kiwango kibovu akiichezea Santos inayoshika nafasi ya nane kwenye ligi ya Brazili. 
 

No comments:

Post a Comment