Search This Blog

Monday, March 4, 2013

MTEMI RAMADHANI AACHIA NGAZI TFF

Mtemi Ramadhani(Kulia)
Mkurugenzi wa utawala wa shirikisho la soka nchini TFF, Mtemi Ramadhani leo hii ametangaza rasmi kuwa sio muajiriwa tena wa shirikisho hilo kutokana na mkataba wake na TFF kuisha.

Mtemi ambaye ni mchezaji wa zamani wa Simba SC, amesema ameifanyia kazi TFF kwa miaka minne na sasa anaona na muda muafaka wa kuachia nafasi hiyo kwa mtu mwingine na yeye aendelee kujishughulisha ujasiriamali mwingine.

"Nimeitumikia TFF vizuri sana kwa miaka minne iliyopita, mkataba wangu umeisha jana tarehe 3 mwezi tatu. Nimeamua kuendelea na vitu vingine kuachia wengine wapeleke jahazi mbele. Umri wangu umeenda na nafikiri ni muda sahihi wa kujishughulisha na vitu vingine." - alisema Mtemi Ramadhani

3 comments:

  1. Thanks Mtemi, umeonesha njia! NURU SPORTS MSM.

    ReplyDelete
  2. Nafikiri kuna kosa kwenye utambulisho wa picha yako. Kushoto ni Nassib Ramadhani, na Kulia ni Mtemi Ramadhani.

    ReplyDelete
  3. Mtemi Ramadhani yuko kulia na si kushoto, wewe mwandishi vipi!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete