Search This Blog

Tuesday, March 5, 2013

TFF YAPELEKA MAOMBI RASMI KUKUTANA NA WAZIRI KUZUNGUMZIA JUU YA SUALA LA KATIBA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewasilisha rasmi maombi ya kuonana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara ili kuzungumzia uamuzi wake wa kutengua usajili wa Katiba ya 2012.

Maombi hayo yaliwasilishwa rasmi Wizarani jana (Machi 4 mwaka huu) ambapo TFF imependekeza kikao hicho kifanyike keshokutwa (Machi 7 mwaka huu) au Machi 13 mwaka huu.

Kamati ya Utendaji ya TFF iliyokutana Machi 2 mwaka huu kujadili tamko ya Waziri kutengua matumizi ya Katiba ya 2012 ndiyo iliyopendekeza kikao hicho kwa lengo la kusikiliza upande wa TFF katika suala hilo.

2 comments:

  1. iNASHANGAZA Kuona kuwa Serikali inaandikiwa barua na TFF kuomba kikao cha kumuelezea athari za decision ya waziri kutengua katiba ya TFF. Kama waziri haelewi kuna kufungiwa basi hafai kuwa waziri wetu. Athari za hili jambo kwa wadau wote wapenda mpira ni kubwa mno.

    Inasikitisha kuona wadau wengi hawaoni hapa tatizo ni Serikali, kwani organs zake zilipitisha katiba hiyo hiyo muda mrefu uliopita. Sasa wanakurupuka kusema katiba haikufuata sheria katika usajili!

    Serikali ijirudi na kuondoa decision yake hiyo kwani haitekelezeki na italeta kufungiwa na FIFA. Njia ya waraka hutumiwa sana na FIFA kubadili katiba au vipengele. Tuepuke kufungiwa tafadhali!

    ReplyDelete
  2. Wala haishangazi, hii kitu imefanyika kwa muda mfupi, kama wewe mfutiliaji na mtetezi mzuri na imepitishwa kiujaja, ndio maana aliyepisha naye hana kazi. Pia wao TFF waliona ni sawa kwa kuwa huko nyuma walishafanikiwa kufanya madudu kama hayo, yaani siku ya uchaguzi katiba ilipitishwa. sasa uelewe hayo ni makosa. hata msingi mkubwa ni mbinu mubadala ya USULTANI wa TFF, NINYI WATU MUWE WAELEWA LINI UTAMPATA MTU MPYA HATA KWENYE ZA CHINI WAKATI KATIBA INASEMA NI MIAKA MITANO YA UZOEFU. NA BADO HAITOSHI VIKAO VYAO HIVYO VINASIGANA, TENA BILA KUPATA USHAHIDI WA UHAKIKA HUONI KUNA JAMBO

    ReplyDelete